Tunaukaribisha uchunguzi kwa Zitto Kabwe

Tunaukaribisha uchunguzi kwa Zitto Kabwe

hahahaha tatizo sio dau tatizo dini yake

Hata Mh. Rais anatambua Hilo na ndio sababu anasema akiwa pale darajani kuwa Mnyonge mnyongeni haki yake Mpeni akimaanisha Mnyonge ni Dr Dau na Wanyongaji ni Wale wale walimyonga Galileo kwa kusimamia haki ya kusema Dunia ni Duara wakat huo msimamo wa Sinagogi ukiwa Dunia ni pembe nne!
 
Hahahhahaha kuna kampeni kubwa sana ya dau ba uzuri wake haijaanza leo hii na huu mtego watu wajinga wajinga wakina sendeka pia wanauvaa dah nchii
 
TAARIFA KWA UMMA

CHAMA cha ACT Wazalendo kimeshtushwa na tuhuma, kashfa, porojo na matusi mbalimbali yaliyotolewa jana na msemaji wa chama cha Mapinduzi(CCM), Ndugu Christopher Ole Sendeka dhidi ya Kiongozi wa chama chetu, ndugu Kabwe Z. Ruyagwa Zitto.

Kutokana na hayo chama kina masuala yafuatayo ya kusema kwa wanachama wetu na umma wa Watanzania kwa ujumla:

• Chama chetu kinakaribisha uchunguzi juu ya mali na madeni ya Kiongozi wetu, ndugu Zitto. Tutafurahi uchunguzi huo ukihusisha akaunti zake za benki pamoja na mfumo wa maisha yake binafsi (Life Style).

Tunavitaka vyombo vya uchunguzi vianze kazi hiyo mara moja kwani tunaamini kuwa Kama kuna Kiongozi ambaye Mali, Madeni, Maslahi na Akaunti zake viko wazi basi ni ndugu Zitto.

Ikumbukwe kuwa Katiba na Kanuni za chama chetu huwataka Viongozi wote wa chama kuweka hadharani tamko la mali zao na madeni, ndugu Zitto alitekeleza matakwa hayo ya kisheria, na mali pamoja na madeni yake yako hadharani na mtandaoni. Tunatambua chama tawala kinaweweseka na tunataka kiondokane na ugonjwa huo wa kuweweseka,badala yake wachukue hatua za uchunguzi dhidi ya ndugu Zitto.

• ACT Wazalendo tunayo taarifa ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, CAG. Kupitia taarifa husika CAG ametoa Hati safi Kwa Shirika la NSSF Kwa hesabu za mwaka 2014/15. Hajaona ufisadi wowote ule.

Sijui msemaji wa CCM anatumia taarifa ipi ya CAG kusema kuwa NSSF ilinunua Ardhi Kwa bei ya Shilingi Milioni 800 aliyomhusisha nayo Kiongozi wetu.

Kwa mujibu wa barua ya CAG Kwa Uongozi wa NSSF (Management letter), Shirika hilo halijanunua ardhi yoyote Kigamboni, bali Shirika limeingia ubia wa Ardhi Kwa Hisa (Land for Equity).

Hivyo ni vizuri mbwatukaji huyo wa Chama tawala akaeleza kwa undani Ufisadi anaousema juu ya manunuzi ya ardhi kwa kunukuu ripoti ya CAG kaitoa ukurasa namba ngapi katika ripoti husika.
Labda chama chake kina taarifa nyengine ya CAG tofauti na iliyowasilishwa kwenye Kamati ya PAC.

Rais Magufuli, ambaye ni Mwenyekiti wa chama tawala, amemteua aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF kuwa Balozi. Kauli za Msemaji wa chama tawala alizozitoa jana zikiaminiwa zina maana kuwa Rais na Mwenyekiti wa chama chake anateua mafisadi kuwa mabalozi. Ni vizuri nyie wanahabari muulize juu ya hili jambo.

• Ni wajibu wa Viongozi wa chama cha ACT Wazalendo kuupinga ujinga popote pale ulipo, Kiongozi wa Chama chetu, ndugu Zitto, anatekeleza wajibu huo kwa Uzalendo mkubwa kwa Taifa lake.

Chama chetu kiko pamoja naye katika kupinga Ufisadi mkubwa wa ESCROW ambao chama tawala kimeukalia kimya, ufisadi wa Mabilioni ya HATI FUNGANI na hata sasa anapowapigania Waandishi wa Habari nchini katika Kampeni yake ya kupinga MSWADA MBAYA wa Habari.

Tunajua kuwa kampeni hii ya kupinga Mswada mbaya wa Habari ndiyo ambayo imezua ubwatukaji huu wa msemaji wa chama tawala.
Ni muhimu Serikali na chama tawala wajue kuwa chama chetu kitaupinga mswada huo ambao utakwenda kuua tasnia ya habari nchini mpaka pale utakaporekebishwa. Porojo, kashfa na matusi havitaturudisha nyuma, tutaisimamia hoja hii mpaka mwisho.

• Tunamtaka msemaji wa chama tawala aache porojo, kashfa, vijembe na matusi. Ni muhimu ajikite katika kukishauri chama chake kutekeleza ahadi zake kwa wananchi. Sasa ni mwaka mmoja tangu wachaguliwe, lakini hakuna madawa hospitalini, hakuna mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu, hakuna ajira mpya, hakuna kupanda mishahara kwa watumishi wa umma, hakuna hata jiwe la msingi la Kiwanda kipya lililowekwa tokea Serikali ya awamu ya tano iapishwe, mzigo imepungua bandarini, magari makubwa ya mizigo yameamuriwa yapaki tu kwa kuwa sekta ya Usafirishaji imeuliwa, na maisha ya Watanzania yamezidi kuwa magumu.

Hayo ndiyo mambo ya msingi ya Watanzania, chama chetu kitaendelea kuisimamia serikali katika mambo hayo Bungeni kama anavyofanya mbunge na Kiongozi wetu wa Chama.
Mwisho kabisa, tunapenda kujua kama haya aliyoyasema Ole Sendeka ndiyo msimamo rasmi wa Chama chake au ni maneno yake mwenyewe,maana kama ni msimamo wa chama chake,tutakuwa na mengine ya kusema.

"Taifa Kwanza, Leo na Kesho"

Habibu Mchange
Katibu wa Bunge na Serikali za Mitaa
ACT Wazalendo

Oktoba 29, 2016
ivi ule mjengo pale dom ulishaisha? ume mgorofa sijui wa shopping mall sijui?
 
Mambo mengine bwana, mnakumbushia kwani ni nyie mliouomba au kuuanzisha?

Na washawasha!
 
Maswali ya kujiuliza

1. Kwanini ACT inamtetea sana Dr Dau ?
2. Kwanini tuhuma dhidi ya Zitto zinajibiwa na Chama ?
3. Kwanini kwenye majibu hayo hoja ya msingi imekwepwa ?

Au tuhuma alizotoa Afande Sele ni za kweli ?
 
hahahaha tatizo sio dau tatizo dini yake

Hata aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU hakuwa na tatizo walimtumbua kwasababu ya dini yake.Pia alikuwa Mkuu wa Mkoa fulani Mama Anna Kilango alitumbuliwa kwasababu ya dini yake.Wapo wengi walitumbuliwa kwasababu za kidini zaidi kuliko ufisadi mwingine ni DG wa Bandari,DG wa vitambulisho vya taifa,aliyekuwa mkurugenzi wa Jiji Marehemu nani vile.... .Haaa haaaa hao wote hatukusikia dini zao zikiguswa bali ufisadi wao iweje Dr Dau akiguswa wasako tonge povu linawatoka.

Tunaweza kwenda mbali kuanzia kina Mramba,Yona list ni ndefu sana yupo aliyekuwa Commissioner General wa TRA mpaka leo yuko na ndoo yake mahabusu hakuna cha dini yake wala nini inashangaza Dr Dau akiongelewa wazee wa futari wanatetemeka.
 
Maswali ya kujiuliza

1. Kwanini ACT inamtetea sana Dr Dau ?
2. Kwanini tuhuma dhidi ya Zitto zinajibiwa na Chama ?
3. Kwanini kwenye majibu hayo hoja ya msingi imekwepwa ?

Au tuhuma alizotoa Afande Sele ni za kweli ?
Ni wajibu wa mpenda haki kutetea pale mtu anapoonewa. Kwa hilo, ACT wako sahihi.
 
Hata aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa TAKUKURU hakuwa na tatizo walimtumbua kwasababu ya dini yake.Pia alikuwa Mkuu wa Mkoa fulani Mama Anna Kilango alitumbuliwa kwasababu ya dini yake.Wapo wengi walitumbuliwa kwasababu za kidini zaidi kuliko ufisadi mwingine ni DG wa Bandari,DG wa vitambulisho vya taifa,aliyekuwa mkurugenzi wa Jiji Marehemu nani vile.... .Haaa haaaa hao wote hatukusikia dini zao zikiguswa bali ufisadi wao iweje Dr Dau akiguswa wasako tonge povu linawatoka.

Tunaweza kwenda mbali kuanzia kina Mramba,Yona list ni ndefu sana yupo aliyekuwa Commissioner General wa TRA mpaka leo yuko na ndoo yake mahabusu hakuna cha dini yake wala nini inashangaza Dr Dau akiongelewa wazee wa futari wanatetemeka.
Kweli we hujitambui. Toka Nyerere aape kulitoa kanisa kwenye matope hajapatikana fisadi mkubwa kutoka kwa waislamu. Jaribu kuorodhesha majina ya watuhumiwa wa ufisadi uone
Hapo kanisa linatafuta kwa nguvu ili Dau aingizwe kwenye orodha ila uongo wao unachemsha
 
Ni kweli hata yule Prof wenu alificha mijifedha nje ziliponaswa na mkono mrefu wa serekali akabadili dini kabla hajafa akaitwa Prof Kighoma Malima Joseph.
 
Ni kweli hata yule Prof wenu alificha mijifedha nje ziliponaswa na mkono mrefu wa serekali akabadili dini kabla hajafa akaitwa Prof Kighoma Malima Joseph.
Ndo nakwambia hujitambui. Divai unayonyeshwa kanisani inakuzidia.
Kila unacholishwa hutafakari unakimbia kuandika. Huenda wakati wa Malima wewe ulikuwa bado mtoto.
Kwa taarifa yako, yote yaliyompata Kighoma Malima ni kwa sababu ya dini yake
 
Alikwapua fedha kwasababu ya dini yake 😵
 
Huwezi jua kwani kuna uwezekano wakati huo we ulikuwa ukichunga mabata

Tukiwapeleka Kisutu wagalatia sawa,mtoto wa mama mdogo nongwa haaa haaa hii nchi Forojo Ganze kafungia akili zetu kwenye mapango Bagamoyo sishangai arguments zako si kosa lako.
 
Back
Top Bottom