Tunatengeneza aina mpya ya upinzani

Tunatekeleza ilani
Yawezekana hiki ndo kipindi mlicho enda kinyume na ilani yenu kuliko kipindi chochote. Kwenye ilani mkasema mtasomesha watakao pata ujauzito wakiwa shule,.....mkasema kipaumbele ni umeme wa gesi,......
 

Yaani kama watu wataamua kusema amini nakwambia utawala huu ndio unaopigika mawe kiwepesi mno, Jiwe anapigika mapema sema ameshaonyesha ukatili uliopitiliza ndio maana watu wanavuta pumzi kusubiri kipyenga ukisema sasa watu wake watakuumiza bure.
 
Majaribio ya kuipindua serikari kabla ya mfumo wa vyama vingi yalikuwa mengi.Sijui tunaelekea wapi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hicho hicho kinachokununulia Dreamliner 787
Hivi hiyo dreamliner imenunuliwa na chama au ni serikali kwa fedha ya kodi za wananchi wote?
Tutofautishe fedha ya serikali na ya vyama vya siasa. Chama chochote kikitawala haina maana kwamba ndicho kinatumia fedha zake kwa uchumi wa nchi, hata kidogo. Kwenye halmashauri moja hapa nchini, chama tawala kilileta mizengwe hadi kikachukua standi ya magari pamoja na vibanda vyake vyote na jambo hilo likaifanya halmashauri kupungukiwa kabisa na kipato vyanzo vya mapato yake kwani kodi na ushuru wote wa hiyo standi uligeuka na kuwa in mapato ya chama kwa ajili ya shughuli za kichama tu.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Iliandikwa mwezi Februari, uchambuzi kuelekea uchaguzi mkuu
 
Mtazamo murua kabisa ndicho kilichotokea na kitaendelea kutimilika.

Uzi wa February na Leo Ni November!
 
Mtoa mada ni kama vile ni mtu wa Kitengo, alinena kile walichokusudia kukifanya na kimetimia.
Inawezekana Jakaya alikuwa na udhaifu ndio sababu wakampa nchi huyu mwenye staili ya kibabe.
 
Bila upinzani imara ccm hawawezi kujitambua. Wanapambana kufanya yote wanayo jaribu wakijua mguu kwa mguu, neno kwa neno 24/7; Wapo nyuma yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
Bahati mbaya upinzani imara haupo tz labda tuanze upya. CHADEMA ilitegemewa iwe chama pinzani imara lakini wamepoteza fursa. Hivyo vingine vidogovidogo vimekaa kama vicoba.
 
Mtoa mada ni kama vile ni mtu wa Kitengo, alinena kile walichokusudia kukifanya na kimetimia.
Inawezekana Jakaya alikuwa na udhaifu ndio sababu wakampa nchi huyu mwenye staili ya kibabe.
Wala sivyo mkuu, ni uchambuzi tu
 
Bila upinzani imara ccm hawawezi kujitambua. Wanapambana kufanya yote wanayo jaribu wakijua mguu kwa mguu, neno kwa neno 24/7; Wapo nyuma yao.

Sent using Jamii Forums mobile app
Bahati mbaya upinzani imara haupo tz labda tuanze upya. CHADEMA ilitegemewa iwe chama pinzani imara lakini wamepoteza fursa. Hivyo vingine vidogovidogo vimekaa kama vicoba.
Nadhani upinzani wa kweli kabisa toka moyoni upo tayari hapa Tanzania. Kinachokosekana kwa sasa ni ujasiri kwa sababu ya kitawaliwa na hofu. Watanzania wa leo bado wanaongozwa na hofu ya kufikirika ndio maana hawajawa tayari kuwekeza kwa ajili ya kesho. Ni kundi linaloishi kwa kutazama Leo tu. Udhaifu huu ndio kete pekee iliyosalia kwa watawala. Lakini ukweli ni kuwa siku zinakuna nazo haziko mbali utafika wakati watu wataamua kwamba hakuna tofauti kati ya kufa na kuishi kama hakuna uhuru binafsi. Tofauti kati ya maiti na mtumwa asiye huru ni kuwa mmoja akili zake zimelala fofofo, lakini mwingine HUJIDHANI kuwa anaishi kwa akili zake wakati ukweli ni kuwa ameshakufa siku nyingi bali mwili wake unaongozwa kwa akili za watawala. Hana jambo analoweza kuamua kwa kutumia akili yake bali amekuwa kama kompyuta ambayo hutekeleza kile inachoamriwa.
 
Umeeleweka. Ingawa ulikuwa ni aina ya utabiri, kwasasa unaweza kuufanyia update. Hasa kwenye hitimisho. Walau tupate mwongozo wa nini mwelekeo wa wapinzani ili waje kushika dola. Kwani lengo la chama chochote vikiwemo vya upinzani ni kishika dola. Hivyo kwa uoni wako unadhani upinzani huu mpya utawezaje kushika dola iwapo walio kwenye mamlaka wanatumia udhalim kubaki madarakani.
 
Safety valve!
 
Familia moja ikimaliza kuua ujirani na familia zinazoizunguka ! Basi itafuata familia hiyo pia kusambaratika..
 
Huwezi kuwanyamazisha watu kwa kuwaondolea platform ya kutolea dukuduku zao. Ni heri kuwapa uhuru wa kusema wakatuliza nafsi kuliko kuchukizwa na maneno yao na hivyo kuwataka wafunge midomo na kukaa kimya!
Mkuu, uliona mbali sana. Uliandika uzi huu mwezi February, lkn karibu yote uliyonena ndo yametokea.

Huko ccm kuna watu ambao wanadhaniwa kuwa wanataaluma ya siasa, akina Bashiru Ally, lkn wamefanya mambo ya ajabu sana.

Nadhani watakuwa wanajua kuwa wananchi wengi ni wapinzani mioyoni na ndo sabb wakafanya rafu nyingi kwny uchaguzi, maana walijua fika bila hivyo hawashindi.

Matendo waliyofanya kwny uchaguzi mkuu mwaka huu, sijui Kama wanafahamu yalivyoathiri nafasi yao ktk mioyo ya wananchi walio wengi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…