Tunataraji sakata la Makonda kutuhumiwa kufoji cheti litinge bungeni April, Ndalichako jiandae

iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,437
14,924
Kwa kuwa hii ndio aina ya siasa tuliyoichagua,natarajia wabunge wote kwa pamoja watamtaka waziri wa elimu atoe taarifa kuhusu sakata la vyeti vya elimu ya mkuu wa mkoa huyu.

Waziri aelezee shule alizosoma mkuu huyo wa mkoa,majina aliyotumia mpaka kufikia hatua ya elimu aliyofikia

Mtu anayeshikilia ofisi ya umma anatakiwa asiwe na makandokando ya kielimu na mengineyo.

Huyu ni mtu mwenye dhamana ya kusimamia elimu katika jiji kubwa kuliko yote,jiji lenye vyuo vikuu kadhaa na likiwa na changamoto ya kutoa shule zilizofelisha zaidi kitaifa.

Ni wazi wabunge,kwa kutumia haki yao kikatiba,basi wahoji elimu ya huyu bwana,wakizuiwa,basi,wakati wa kuchangia,kila mchangiaji aweke dakika moja kuongelea sakata la huyu bwana,naamini wakifanya hivi wabunge 300, bunge la April,bunge la Bajeti,bunge la septemba,bunge la novemba,basi jibu litatolewa

PIA

Uangaliwe uwezekano wa kufungua kesi mahakamani kumlazimisha yeye,waziri wa elimu,Baraza la mitihani wauambie umma wa watanzania kuhusu uhalisia wa elimu wa mtu huyu
 
Makonda kijana wa juzi tu hana hata maclassmate waseme chochote mpaka Bungeni ?? kama Mitandao yetu haionyeshi ! vitu vya ajabu hana hata magroup ya sekondari ! mhhh
 
Kwa hiyo PhD ya mkuu imewekwa pembeni sasa wauza unga mnapambana na aliyeanzisha mapambano ya madawa ya kulevya...!!!
 
Back
Top Bottom