Tunatambua umuhimu na kutumia fursa za Ubunifu Wetu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunatambua umuhimu na kutumia fursa za Ubunifu Wetu?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by MwanaHaki, Apr 11, 2009.

 1. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #1
  Apr 11, 2009
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Waungwana,

  Nimeona niwaulize swali, kwa kuwa Jamii Forums ni Home of the Great Thinkers, nami natambua mtanipa majibu yatakayokidhi haja ya swali hili kuu. Swali ni: Je, sisi Watanzania tunatambua umuhimu na kutumia fursa za Ubunifu Wetu?

  Ninaposema hivi ninamaanisha hivi.


  1. Kuna watu ambao wana vipaji vya hali ya juu vya ubunifu, wana utundu wa asili. Mnawaona mitaani, wakibuni vitu mbali mbali. Kwa mfano, kuna jamaa mmoja nilisoma habari zake mwaka jana, yuko Kyela. Huyu kaishia Darasa la Saba, lakini kwa utundu wake ameweza kuunganisha injini ya pikipiki kwenye baiskeli, na amekwishawatengenezea watu wengi baiskeli zenye pikipiki, kwa gharama ya takriban Shs. 200,000/-. Amewawezesha watu wengi kusafiri kwa umbali mkubwa na kutumia mafuta kidogo tu ya petroli; lita 1 ya petroli inaisafirisha baiskeli hiyo (yenye injini ya pikipiki) umbali wa kilometa 42. Injini hizo zimetumika, zinaagizwa kutoka Japan, kupitia Mombasa. Yeye na nduguye ndio wenye shughuli hiyo. Ubunifu wa watu hawa unatumikaje?
  2. Wako watu wengi zaidi wenye vipaji. Niliwahi kuelezewa kuhusu kijana aliyevumbua helikopta, alikuwa akiishi Arusha, kwa mjomba wake. Alipovumbua helikopta hiyo ambayo alidai iliweza kutembea kwa kutumia mafuta ya kulainisha mitambo (grease), mjomba wake alitaka yeye ndiye atambuliwe kama mvumbuzi wa hiyo helikopta. Kijana aligoma, mjomba, kwa hasira (na ufisadi wake) aliivunjilia mbali helikopta hiyo. Kijana akasafiri hadi Dar, moja kwa moja hadi ofisini kwa aliyekuwa Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu (wakati huo Dk. Pius Ng'wandu), na kuwaambia wanunue vifaa vyenye thamani ya Shs. 5,000,000/=, wamfungie kwenye ghala, baada ya wiki 2 angekuwa ameunda helikopta hiyo. Ng'wandu akagoma! Habari za kijana zilifika hadi Israel, Waisrael wakatuona sisi wendawazimu, wakaja kumchukua kijana, yuko huko anatesa!
  Nadhani mifano hii michache inatosha kuwaelezea nini kinachonikera moyoni. Tunakaa, kutwa, kulalama kwamba sisi ni MASKINI, lakini utajiri tulionao wala hatuufanyii kazi.

  Kwa nini isiwezekane kuunda Jukwaa la Wabunifu na Ubunifu Tanzania (Tanzania Inventors and Intellectual Property Forum), ambalo lingewakusanya wabunifu/wavumbuzi wote, kuratibu kazi zao na kuzitafutia soko, ili wawekezaji waje kutengeneza vifaa vinavyoenda na wakati. Uwekezaji Tanzania usiishie kwenye viwanda vya nguo, mabati, vyombo vya nyumbani, viatu, unga, peke yake. Kuna mawazo mengi mapya, mazuri, ambayo bado hayajafanyiwa kazi, kwa kuwa wapo Watanzania wenye ubunifu mkubwa, lakini kwa sababu ya ROHO ZETU MBAYA tunawaona wao kuwa maadui wetu wakubwa, huku ukweli ni kwamba hawa ndio WAKOMBOZI WETU. Mawazo yao ndio yatakuwa ukombozi wetu, kwani, kama sisi wenyewe tumeshindwa kubuni mambo mapya, tukubali kwamba miongoni mwetu wapo vijana, watu wazima, wake kwa waume, wenye akili za ziada, wenye ujuzi usio kifani, wenye VIPAJI VIKUBWA, ambavyo vinakandamizwa na watu wasio na hiyana. HUO NI UFISADI!

  Kwa nini tunajikandamiza sisi wenyewe? Tuwatumie hawa watu? Wana JF, mmenielewa?

  ./Mwana wa Haki
   
Loading...