Bila bila
JF-Expert Member
- Dec 20, 2016
- 22,880
- 40,517
Kuandaa Mechi moja ya soka hata uwanja ni pale shamba la Bibi ni gharama kubwa maana inahusisha vitu vingi ikiwemo matangazo, gharama za kukodi uwanja, kuandaa timu, kusafirisha Wachezaji na kualika wageni mashuhuri nk.
Vivyo hivyo kwenye siasa kuandaa Mkutano mmoja wa hadhara si Jambo dogo kama ambavyo Mtu mwenye kichwa chepesi kama Maulid Kitenge "Zwazwa" anavyodhani.
Wakati maandalizi ya Mkutano wa hadhara wa CHADEMA pale viwanja vya Bulyaga Temeke yakiwa yamekamilika Kwa asilimia zaidi ya 90% ikiwemo Taarifa toka Polisi, ghafla Leo alfajiri anaibuka Dalali wa DP WORLD Maulid Kitenge kupitia Kiblog chake anamzulia Msajili wa vyama vya Siasa Jaji Mutungi kwamba amezuia Mkutano huo na kwamba amewataka viongozi wa CDM kufika ofisini kwake kesho kujieleza.
Kama kweli Jaji Mutungi angefanya hivyo angekuwa bonge la bogus. Unamuitaje Mtu kujieleza Kwa kosa ambalo halijakamilika?
Baada ya Muda imegundulika maneno ya Kitenge ni uongo na Hakuna mamlaka ndani ya ofisi ya Msajili wa vyama vya Siasa iliyotoa habari hiyo.
Mheshimiwa Nape, Iwe aliongea na Mutungi kishikaji au kajitungia mwenyewe, tunataka kuona hatua za kikanuni zikichukuliwa dhidi ya Kitenge na Kiblog chake kama ambavyo imekuwa rahisi Kwa wengine àmbao hutoa maoni kinzani na serikali.