Tunataka kile usichokuwa nacho

miss chagga

JF-Expert Member
Jun 7, 2013
57,821
48,976
Habari zenu wana jf
….kuna swali huwa wengi wetu tunapenda kujiuliza au kuwauliza wapenzi wetu au hata marafiki hivi wanawake wanataka nini ? au hivi wanaume wanataka nini?

Hili swali huwa halina majibu ambayo ni ya moja kwa moja ila unaweza kuweka akilini mambo yafuatayo kuchoka, kukinai mazoea na pia kila jambo lina kupanda na kushuka..

Binadamu tuna kawaida ya kupenda kitu kiwe kinaenda katika mstari mzuri na kusahau kila kitu duniani kina pande mbili uzuri na ubaya. Matokeo ya ubaya hapo ndiyo wengi hatupo tayari..

Kwa upande wetu sisi wanawake tupo tunaopenda PESA, MAPENZI YA KWELI, MUONEKANO MZURI WA MWANAUME na wengine vyote .

Ni rahisi sana mwanaume kupata mwanamke amtakaye na asiye kuwa na mapenzi ya kweli akiwa na pesa na anayejua kutumia pesa ukiona unataka wanawake wanakukimbia unatatizo lingine. Viashiria vya pesa kwetu sisi wa dada anaenda kazini, gari,maeneo unayopenda kukaa, nyumba uanyoishi kama akibahatika kuona na hata mwonekano wako ….

Sasa ukinipata kwa njia hizi na mi nitakupenda kwa namna hiyo hiyo ukiishiwa baba niliyoyafuata hayapo kwa nini nisiojiondokee zangu nakukuacha sababu wakati we unaishiwa kuna mwingine anazipata na bahati mbaya labda ananifukuzia …

Wanaume wengi mna tabia mbaya ya kuanza na mabinti wa kawaida tu wakati hamna pesa mkishazipata mnaanza kufukuzana na siye wachunaji na kumuacha Yule aliyekuvumilia unamapeleka kagest cha 3000 na bado yupo na wewe .. unakuja kukimbizana na kina sampuli ya miss thubutu unitoe kwenye hotel ya dola kadhaa unipeleke ya ya 35,000 nasubiri nini kwako labda?

Pendeni wanawake waliowavumilia mkiwa hamnacho wajali waheshimuni labda kama hayupo hapo sawa ila analia wewe huku wewe unajilia bata subiri ufilisike tutoke nduki….. wekeni akilini baadhi ya wanawake huamini mwanaume wenye pesa wengi ni maplayer japo wapo ambao siyo maplayer kabisa huwa atuweki roho na mioyo yetu yote kwenu …kwa hiyo ukipata demu kwenye hali hiyo possibility kubwa ya kuachwa uatakaposhuka ni kubwa japo wapo mademu wanaowapenda kweli..

Mapenzi ya kweli mimi sina maana sana ya mapenzi ya kweli huwa sijui ipoje ila nitaelezea namna navyoona mimi mwanume kunijali na kunipa pesa … sasa jamani tuwe wa kweli tu siku zinavyozidi kwenda binadamu huwa tunachoka kukinai na hata kumzoea mwenzio ikishafika hatua hii lazima kuna vitu hupunguza pole pole sasa hapo mtu anaanza ooh au kapata mwingine kumbe wala..

Mnajua mapenzi mapya siku zote ni matamu sababu ya kubembelezwa kujaliwa najua mnajua yanavyonoga .. katika kipindi hiki huwa hatujiandai kisaikolojia kuwa ipo siku mambo yatabadilika wala huwa tunataka vile vile na tulivyo wabinafsi tunaanza kunyoosheana vidole badala ya kila mmoja wetu kujichunguza kaacha gape wapi ili mrekebishe ..

Mnalaumiana mwisho na kutegeana hata kutumiana salamu kwa kuendekeza mahisia yetu ooh kwa nini mi kila siku nianze .. mbona wakati uanaitongoza ulikuwa uanatuma salamu mia mia … any way tutumie nafasi zetu vizuri bwana na mjue hatuwezi kuwa sawa ukilegeza jua inakula kwako..

Nina roommate wangu hosteli moja hapa mjini ni mzanzibar Yule mwanaume wakati anamfukuzia huyu demu alikuwa anapanda boti kutoka Zanzibar na urojo sijui wa kwa babu nani mpaka external pale anamletea demu urojo na hapo analala na mzigo hapati… baada ya miezi kufukuzia demu akaiingia kingi akaliwa wacha jamaa akate hakuna cha urojo wala ice cream..

Mbona alipigwa chini kwa nini siku hizi uniletei urojo na ice cream hapo watu wa nje watalaumu mbona kamuacha mademu hawajui wanataka nini? kumbe jamaa haleti tena urojo na ice cream.. tufanye yale tunayoweza kuendeleza,,..

Muonekano mzuri mwanaume kama huna pesaa mmhh sijui inakuwaje Mario hawa ni wengi… hahahaha hata jogoo kabla ya kugonga huwa anawaitia vimtetea vivyakula vyakula wakati wanadonoa yeye ndiyo anakamata mmoja anapiga .. sasa wewe kama huna vitu vya kuita mademu duh utakuwa unaachika kila uchao na mwonekano wako huo,,…

Kwa maelezo hayo hapo juu tunatakiwa kukubaliana na mabadiliko binadamu haturidhiki na huwezi kuturidhisha ,, binadamu tuna hulka ya kutafuta kile ambacho hatuna na si kile ulichonacho.. ila jambo jema kujifunza kurekebisha kile ulichonacho tayari sababu vile unavyovitafuta probably havipo.


Absence makes the heart grow fonder”
 
Mademu hawajuagi nini wanataka, kile unachohisi ukimpa kitamfanya akupende daima ipo siku utashangaa na dunia atapokugeuka ukawa fwala na mbaya zaidi kukusaliti juu.
Wanawake ni viumbe wa hovyo sana kuwahi kutokea ulimwenguni. Mazee tusipoteze muda kuwekeza kwa mapenzi na hawa wadudu. Hawaridhikagi hataaa umpe dunia.
 
Back
Top Bottom