Tunataka katiba mpya

Swelana

JF-Expert Member
Sep 24, 2016
418
1,259
Hili sio ombi ni haki yetu ya msingi,tunataka katiba mpya iliyopitishwa na tume ya Jaji warioba.
Huu upuuzi na ujinga wa hawa wanaojifanya miungu watu yaani ma-rc uchwara,dc uchwara na uchwara wengineo wafutike katika fikra na macho yetu.
Tumechoka sana kuona mijitu ikijiona ina haki na nchi hii kuliko wengine na kujifanya malaika wakati ni mishetani.
Ninawashauri viongozi wa upinzani waitishe maandamano nchi nzima kushinikiza upatikanaji wa katiba mpya.

Pia nyinyi viongozi wa upinzani kama mnaona tabu kupigwa mabomu sababu ya kudai haki ya msingi basi tangazeni maandamano na msiyatengue kisha nyie kaeni majumbani kwenu sisi wananchi tulio na shida na dhiki za kimaisha za kukosa ajira,watoto kukosa mikopo ya elimu ya juu tutaandamana na wala hatutarudi nyuma.

Yani nchi hii uonevu sasa umezidi mpaka inafikia mahali tunamkosea MUNGU tukiomba hata isis,al shabaab na vikundi vingine viingie labda wenye nchi wanaweza amka na kuona kwamba hii nchi ni yetu sote,mateso yamezidi tunaumia ndani kwa ndani hatuna pakusemea na miaka kumi ijayo watz wanaougua magonjwa ya moyo watakuwa wengi mno kwa sababu ya maumivu ya ndani kwa ndani..

Liwalo na liwe msema kweli ni..............
 
Katiba mpya ni muhimu mno ingawa kusema kwali watawala haiwavutii tena!

Tunaitaka, Tunaihitaji, Tunaidai katiba ile ya Warioba.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom