Tunataka Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi

Shocker

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
1,363
2,000
Mengine yote yatakupotezea muda mwisho wa siku hao hao wenzako watakupiga na chini na maneno kibao, hawana kheri hao

Jambo moja Rais Samia la kuwafadhaisha hao wanaokusogelea ambao hawana ukweli wanacheka ukiwepo ni kuibuka na Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya, na kuhakikishia hapo ndio utawajua ni nani CCM wanakupa sapoti kwa moyo uliowazi na sura zilizo na upendo.

Maadui hapo utawaona nje nje kama uliowasomea halalbadri.

Usirudi nyuma kuipatia nchi Katiba mpya na tume huru ya Uchaguzi,hata upinzani watakuwa pamoja nawe kukupatia mitano mingine kama bonasi, yaani watanzania watakuwa hawana cha kukulipa ila kukuongezea mitano mingine.

Tume Huru na Katiba Mpya ni halalbadri ya CCM waovu naaamini wengine watapata wazimu.
 

Matola

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
41,964
2,000
Palipo na tume huru CCM inaweza kushinda kwa njia ipi?

Kwamba huelewi Chifu Hangaya Urais umeshamnogea?
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom