Kashaijabutege
JF-Expert Member
- Oct 20, 2010
- 2,696
- 740
Tusiende kwa mkumbo tu. Seriously ukiwauliza wana JF, at least walio na elimu ya shahada, kuwa ni wangapi wana kopi ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kitakuwa ni kichekesho kwa kugundua kuwa hawatafika hata 20.
Nunua katiba muisome, vinginevyo mtaumbuka mkijidai kuchangia mada na weledi.

Katiba iliyopo haifai kwa vile ndiyo inayowezesha watawala wasio wajibika kwa wananchi kuendelea kuhujumu rasilimali za nchi, wakipendeleana wao na ndugu zao na wapambe wao huku umma wa watanzania wakishindia mlo mmoja, elimu duni na kukosa huduma za afya. Katiba iliyopo haifai maana viongozi wezi wa mali za umma wapo tu wakidunda na V8 mitaani. Anayepinga katiba mpya aidha haelewi anachopinga au ana nufaika na mfumo wa upendeleo uliopo.
Hatuna haja ya kuisoma katiba yote ili kuunga mkono uundwaji wa katiba mpya. Watanzania wengi washa jua mapungufu ya katiba na hicho ndicho wanachokipigania. na hiyo haihitaji kuisoma katiba kujua hilo!!!!
Kwa taarifa yako hakuna nchi yeyote duniani ambayo wananchi wake walau 1 % wanaijua katiba. TZ haina tofauti na hao. Hata Kenya, au Zimbabwe siyo kuwa wananchi wake walikuwa wanaijua katiba ndiyo wakaamua kuandika mpya.
Kadi yako ya ccm ni namba ngapi vile ili uhakikiwe kabla ya kupewa Ukuu wa wilaya?
Tusiende kwa mkumbo tu. Seriously ukiwauliza wana JF, at least walio na elimu ya shahada, kuwa ni wangapi wana kopi ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kitakuwa ni kichekesho kwa kugundua kuwa hawatafika hata 20.
Nunua katiba muisome, vinginevyo mtaumbuka mkijidai kuchangia mada na weledi.
Kwa sisi tulioisoma katiba haina budi kubadilishwa-sisi tutakuwa tunawakilisha jamii nzima-si wote wataweza kuisoma-maana kuna watu huko vijijini hata kusoma hawawezi-kama unataka kila mwananchi aisome hawa wataisomaje?
Katiba mpya ni muhimu hata kama watanzania hawaijui vizuri. Ila nashauri ni vizuri watanzania wajijue hii iliyopo kusudi hata wakati wa mchakato wajue ni nini cha kubadilisha. Maana haitakuwa na maana kutaka mabadiliko na wakati wa mchakato hawajui cha kubadilisha, matokeo yake itakuwa ni kupelekeshwa na wanasiasa tu.
Pia nadhani sasa imefika wakati wa watanzania kuanza kusoma hata vitabu, katiba zinazoihusu tanzania.
Kadi yako ya ccm ni namba ngapi vile ili uhakikiwe kabla ya kupewa Ukuu wa wilaya?