Tunataka CHADEMA mfanye maamuzi ya kushiriki majimbo ambayo wabunge wa upinzani walijiondoa kwenda CCM

Zee la kitaa

JF-Expert Member
Oct 25, 2017
403
211
Ni jambo jema kwa chadema kufanya maamuzi sahihi kugombe majimbo ya wabunge wa upinzani waliotoka vyama vyao na kujiunga na ccm na kupewa ridhaa kugombea tena. Kikao chenu leo kigusie jambo hilo; tuone ni kwa namna gani wananchi watakubaliana na hilo.
 
Wasituyumbishe, kwani kuna kipi kimebadilika?
Tuwe watu wa misimamo,
Tena wakishiriki, ndo itakuwa aibu zaidi maana yake hawatatangazwa tu, sasa kuna haja gani ya kujisumbua?
 
Ni jambo jema kwa chadema kufanya maamuzi sahihi kugombe majimbo ya wabunge wa upinzani waliotoka vyama vyao na kujiunga na ccm na kupewa ridhaa kugombea tena. Kikao chenu leo kigusie jambo hilo; tuone ni kwa namna gani wananchi watakubaliana na hilo.
Ni nafasi ya CUF ya Lipumba kuonesha kama kweli wao wanasimamia maslahi ya CUF au ya CCM.
 
Kinachofanyika si uchaguzi kwasababu uchaguzi uñaongozwa na sheria na taratibu zake na kama hizo sheria na taratibu zinakiukwa tena kwa makusudi basi huo si uchaguzi na haustahili kuitwa uchaguzi.

Sasa kama hakuna uchaguzi,unaenda kufanya nini kama sio kwenda kugeuza haramu kuwa halali?
 
Ni jambo jema kwa chadema kufanya maamuzi sahihi kugombe majimbo ya wabunge wa upinzani waliotoka vyama vyao na kujiunga na ccm na kupewa ridhaa kugombea tena. Kikao chenu leo kigusie jambo hilo; tuone ni kwa namna gani wananchi watakubaliana na hilo.

Uko tayari kwa mapambano? Isije ikawa unasema cdm washiriki kisha wewe umekaa ofisini unasubiri wengine waumizwe na kuachiwa vilema. Ingependeza hata tungesikia umeenda mahakamani kufungua kesi ya watu waliojeruhiwa mpaka sasa, lakini kuagiza tu kama uko hotelini " wali kuku, wali ng'ombe, ugali rost" haipendezi. Tuonyeshe mchango wako kwa yale matatizo yaliyosababisha cdm kususia.
 
CCM wameanza kutoka mapangoni, vipi mbona mapicha ya kampeni zenu hamjazirusha kama tulivyo wazoea? Mr. Never told alisha sema "ole wake DC &RC alio wachagua yeye atangaze kashinda mpinzani" unaichukuliaje kauli hiyo? Tumia akili yako mkuu usijitoe ufahamu sawa?
 
Naamini hawatashiriki na uchaguzi mkuu 2020 kwa sababu hizi sababu wanazozitoa Leo za kususia zitakuwepo tu.

Nachokiona ni Mfalme anakwepa kelele za kuambiwa apishe wengine baada ya matokeo kuwa mabaya mfululizo.

Hili Ni suluhisho na muda mfupi tu.
 
Back
Top Bottom