MOI wana treatment na hospitality nzuri sana ukweli usemwe na kwa hilo nawasifu.
Ila kwenye ishu ya gharama tu kwakweli ni kipengele. Hususan ukiangalia uchumi wa mwananchi wa kawaida.
Dawa ambazo zinauzwa famasia za nje, ukiwa MOI unaweza kuuziwa kwa gharama inayozidi mara 3 hadi 4.
Na hakunaga negotiations.
Hapo hujagusa gharama za matibabu pamoja na vipimo.
At least wangepunguza gharama upande wa dawa kuwa gharama sawa tu na famasia za nje ili walau mtu ajitutumue kulipia hayo matibabu, vipimo na kitanda.