Tunasubiri kuona hatua kali zinachukuliwa na BASATA dhidi ya msanii Diamond Platnumz.

mpimamstaafu

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
4,445
4,704
Juzi juzi BASATA ilitangaza kumfungia Msanii Diamond Platinumz na mwenzake kwa muda usiojulikana kutokana na kukiukaa sheria kwa kuimba wimbo wenye matusi wimbo uliopigwa marufuku.

Kufungo hicho ni cha ndani ya nchi na nje ya nchi, pamoja na adhabu hiyo lakini Msanii huyo amekaidi amri hiyo na amesafiri kwenda Embu Kenya kufanya Tamasha. Kukiuka amri hiyo tayari kuna mvutano kati ya serikali BASATA na msanii huyo, hivyo tunasubiri mshindi wa mvutano huo.

Rai yangu kwa Wasanii wetu Waheshimu Sheria za Nchi.
 
BASATA ina nguvu gani au uhalali gani kumfungua msanii kufanya kazi nje ya nchi.

Mamlaka ya BASATA (Jurisdiction) ingepaswa kuishia ndani ya nchi tena huko Tanganyika.

Kama kuna sheria kama hiyo ni ya kipuuzi na kandamizi.
 
Sio tuna subiri sema nasubri... Usubiri we na nani sa
naijatwittersavages-20181221-0001.jpeg
 
Watamsamehe Mtoto wao mtiifu Kama yule aliyegoma kutoa kodi makontena yake bandarini anaendelea kula keki ya taifa .Fanya yako usidhani kuna la maana hata wakitoa tamko kwamba diamond hawamtambui Basata baada ya muda watalikana tamko Lao. La muhimu uhai!!

Watanzania waleo wengi wao wanaendeshwa kwa mihemko., huyu msanii kudharau mamlaka kutapelekea ukaidi kwa baadhi ya wasanii pia kwa BASATA. Leo mtanzania anamtetea msanii huyu kisa et ni mlipa kodi shame!
 
Juzi juzi BASATA ilitangaza kumfungia Msanii Diamond Platinumz na mwenzake kwa muda usiojulikana kutokana na kukiukaa sheria kwa kuimba wimbo wenye matusi wimbo uliopigwa marufuku.

Kufungo hicho ni cha ndani ya nchi na nje ya nchi, pamoja na adhabu hiyo lakini Msanii huyo amekaidi amri hiyo na amesafiri kwenda Embu Kenya kufanya Tamasha. Kukiuka amri hiyo tayari kuna mvutano kati ya serikali BASATA na msanii huyo, hivyo tunasubiri mshindi wa mvutano huo.

Rai yangu kwa Wasanii wetu Waheshimu Sheria za Nchi.
Duh siyajui vizuri haya ya sheria,ila swali langu hii imekaaje ki diplomasia?
 
Hilo linaweza lisilete utata sana Maana si unajua ukiwa bega kwa bega Na serikali hakuna shida!

Utata utaanza pale mwingine atakapofungiwa halafu akaendelea kufanya yake kama kawaida kwasababu Diamond aliachwa aendelee!

Nadhani busara zaidi itumike kuliko nguvu
 
Kwani anaweza kufungwa jela,na asipolipa fine watamfanyeje? Na akiamua kuishi Kenya ama SA basata watamfanyeje?
 
  • Thanks
Reactions: Qwy
Acha upumbavu bas kwahiyo akichukuliwa hatua Kali wewe utafaidika na nini

Watu kama nyie unakuta mnaish kwa shemeji zenu kuanzia asubuh had jion miguu umemyosha kwenye sofa huku ukicheza na watoto Wa Dada yako
Unafurahishwa na matusi ya Diamond? Huna aibu wewe
 
jamani mlivyomkomalia Dai??????

Nilichogundua mimi mkuu,shida sio kosa alilofanya huyu dogo,bali ni wivu tu kwa huyu mtu. Wabongo tuna nongwa za kipuuzi sana na ndio maana tupo hivi hivi tulivyo,hatusogei,tunapenda kuona mtu kadondoka ili tumseme.

Kosa alilofanya sio la kufungiwa kwa muda usiojulikana,ni mihemuko tu ya kuharibia watu maisha yao ndio iliyotumika hapa.
 
Hapa kuna kupimana nguvu Kati ya Mwakyembe , Shonza na Makonda. Ngoja tuone nani ataibuka mshindi.
Kwanini ungoje wakati mshindi anajulikana? Tangu lini Bashite akashindwa na kiongozi yoyote yule nchii hii zaidi ya akiyemteua tup?
 
Nilichogundua mimi mkuu,shida sio kosa alilofanya huyu dogo,bali ni wivu tu kwa huyu mtu. Wabongo tuna nongwa za kipuuzi sana na ndio maana tupo hivi hivi tulivyo,hatusogei,tunapenda kuona mtu kadondoka ili tumseme.

Kosa alilofanya sio la kufungiwa kwa muda usiojulikana,ni mihemuko tu ya kuharibia watu maisha yao ndio iliyotumika hapa.

uko sahihi mkuu,afadhali hata ingekua kwa miezi miwili mitatu...eti muda usiojulikana...huku ni kukomoana per se!...kama ni matusi watu wanacheza vigodoro huku kwetu uswahilini...waje wawakamate..lol
 
Back
Top Bottom