Tunastaafisha 70 tu atcl-mh nyanganyi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunastaafisha 70 tu atcl-mh nyanganyi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Pdidy, Mar 18, 2009.

 1. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #1
  Mar 18, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,227
  Likes Received: 5,618
  Trophy Points: 280
  Habari za Kitaifa Habari zaidi!

  ATCL yaomba kustaafisha 70
  Gloria Tesha
  Daily News; Tuesday,March 17, 2009 @20:19


  Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL) imepeleka serikalini mchanganuo wa maombi ya fedha kwa ajili ya kustaafisha kwa maslahi ya umma wafanyakazi wapatao 70 wa kampuni hiyo, kutokana na kuelemewa kiutendaji kwa idadi kubwa ya wafanyakazi.

  ATCL yenye wafanyakazi 300 ina jumla ya ndege tano na mbili kati ya hizo aina ya Bombadia Dash 8 zenye uwezo wa kubeba abiria 50 ndizo zinazofanya kazi kwa sasa, jambo lililoelezwa kutowiana na uwezo wa gharama za uendeshaji.

  Mchanganuo huo utakapokubalika serikalini, utahusu wafanyakazi wenye umri mkubwa, wanaokaribia kustaafu, wasio na taaluma yoyote na wakatisha tiketi, watu wa mapokezi bila kugusa wataalamu, wakiwamo marubani na wahandisi.

  Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa ATCL,ambae ni amekuwa msemaji wetu wa kampuni;baada ya mkurugenzi kutoonyesha yshirikiano, Balozi Mustafa Nyang’anyi alisema leo bila kutaja kiasi walichoomba serikalini, kuwa tayari wamewasilisha mchanganuo wa fedha zinazohitajika kwa kazi hiyo na kwamba wanasubiri na kuwa habari zilizoandikwa juzi na gazeti moja la kila siku (si HabariLeo) kuwa wanapeleka likizo na kustaafisha wafanyakazi takriban 150, si za kweli.

  “Hakuna mazungumzo wala hatua yoyote iliyofikiwa ya kupeleka watu likizo bila malipo na hatua ya kustaafisha watu ni kwa maslahi ya umma na si ya sasa, maana inahitaji fedha nyingi, hatujui Serikali itatoa fedha lini, pengine mwaka ujao wa fedha,” alisema Balozi Nyang’anyi.

  Kwa upande wake, kiongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Mawasiliano na Uchukuzi Tanzania (COTWU), tawi la ATCL, ambaye hakuwa tayari kutaja jina lake, alithibitisha kufanyika vikao vya mchakato wa kupunguza wafanyakazi kwa kuwastaafisha na kukazia kuwa mpango wa likizo bila malipo walishaukataa na endapo ukiibuliwa, watagoma upya.

  Mwishoni mwa mwaka jana, ATCL ilipata msukosuko baada ya kunyang’anywa leseni ya kurusha ndege na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) kutokana na kubainika dosari katika nyaraka muhimu na baada ya kufunguliwa, ilipewa na Serikali Sh bilioni 4.5 za uendeshaji, lakini ulizuka mzozo baada ya menejimenti kuwatangazia wafanyakazi kuwa watapewa likizo bila malipo, kutokana na uhaba wa fedha.

  Baada ya suala hilo kufutiliwa mbali kwa vikao vya ndani vya kampuni, Bodi na wafanyakazi, hivi sasa Serikali ipo katika mazungumzo na kampuni ya China iitwayo China Sonangol International Limited (CSIL) kwa ajili ya kuingia nayo ubia baada ya kuvunja mkataba na Kampuni ya Afrika Kusini (SAA) miaka mitatu iliyopita kutokana na kubaini hali ya kampuni hiyo kuwa hatarini
   
 2. Pundamilia07

  Pundamilia07 JF-Expert Member

  #2
  Mar 18, 2009
  Joined: Oct 29, 2007
  Messages: 1,433
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Naunga mkono wafanyakazi kupunguzwa kwa kufuata taratibu na makubaliano yaliyopo baina ya Kampuni na Wafanyakazi.

  Ni mategemeo yangu kuwa wafanyakazi watalipwa stahili zao zote. Lakini hata hivyo nadhani ingelikuwa vema wakati wa kumaptia mwekezaji mpya, wafanyakazi wote walipwe malipo yao yote na iwe waajiriwe kwa mkataba mpya badala ya kuwahamisha kama mizigo kwa mwekezaji huyo mtarajiwa.
   
 3. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #3
  Mar 18, 2009
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,227
  Likes Received: 5,618
  Trophy Points: 280
  ni kweli punda ,lakini tatizo linaloonekana hapa kwamba management na bodi awataki kusema ukweli halisi...jana mkurugenzi mkuu alikataa kuhhusu hilo swala ,mwenyekiti wa bodi ambae unaona ndio msemaji wa kampuni;nilipita pale majuzi nikaona wegi wa wafanyakazi wana hamu ya kustaafu sema wanakosa uhakika wa mafao yao;
  TETESI
  Kuna tetesi menejimenti inataka kubadilisha sheria za mafao ya wastaafu ili kupata idadi nyingi ya wafanyakzi wa kupunguza,nawashauri shirikisho la wafanyakazi muwe makini na hili.mko kwa ajili ya wafanyakazi...natumaini huu upuuzi autafanyika..wasaidien watanzania ndio maana nasema jamani wacha tu pamoja na mabox yetu...uwezi fikiria na upuuzi unaofanyika nyumbani
   
 4. Modereta

  Modereta Senior Member

  #4
  Mar 18, 2009
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 163
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Nilidhani na Uongozi wa juu ungestaafishwa pia ili tupate damu mpya na changa itakayoleta mabadiliko. Wengi wamekuwepo siku nyingi, ukisema kitu wanakwambia """ tumeanza na shirika sisi""" hivyo hawasikii la mtu.
  Dunia imebadilika sana kibiashara, shirika linahitaji MWANAMAPINDUZI kulizindua na kujenga "confidence" ya wawekezaji/wakopeshaji na watumiaji pia.

  Ni vizuri Mwajiri mkuu akaangalia na hao wanawastaafisha wenzao.
   
 5. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #5
  Mar 18, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  Mbona waliobaki bado wengi sana kwa ndege walizonazo?
   
Loading...