Mashaka Mgeta
Member
- Jul 8, 2009
- 5
- 2
Wanajamii.
Nimefuatilia historia ya nchi hii na kuona jinsi (awali) Tanzania ilivyokuwa mshirika wa karibu sana na Korea Kaskazini (kutokana na mfumo wa kikomunisti wa vyama tawala katika nchi hizo). Hata sasa ushirikiano huo bado upo. Lakini pia wapo Korea Kusini tunaoshirikiana nao katika masuala ya uchumi na maendeleo, wakitoa ama kusaidia huduma tofauti za kijamii zikiwemo afya, elimu na kilimo.
Lakini hivi sasa, Korea Kaskazini iliyo mshirika hasa wa kisiasa wa Tanzania, anatajwa kwa uvunjifu wa haki za binadamu kiasi cha kuwekewa vikwazo vya kiuchumi na Umoja wa Mataifa. Lakini ni Korea Kaskazini inayoendeleza mradi wake wa nyuklia unaodaiwa kutishia amani ya dunia.
Kwa hali hiyo, hivi Tanzania hivi sasa tunasimama upande gani kati ya mataifa hayo?
Ninawasilisha