[h=5]USALAMA WA WATANZANIA HAUPO LAKINI USALAMA WA TAIFA UPO.
Kwa mujibu wa Sheria ya Bunge namba 15 ya mwaka 1996(intelligence & security services act number 15 of 1996)iliyosainiwa na kupitishwa rasmi kuwa sheria na rais wa 3 Benjamin Mkapa tarehe 20/1/1997,pamoja na kazi nyingine na majukumu mengine ya kiusalama kazi ya taasisi hii itakuwa ni,
1:kutafuta na kukusanya taarifa zote za kijasusi kutoka nje na ndani ya nchi,
2:kuchambua,kuainisha hatari zinazo likabili taifa kutoka kwenye maadui wa ndani na nje ya nchi,
3:kutekeleza mipango ya kukabiliana na hatari hizo .
So kutokana na mambo mbalimbali yanayoendelea nchini mwetu je idala hii nyeti imekufa,imelala,imekosa weledi,imesisinzia,inatumiwa na kutumika kisiasa ama inajua kinachoendelea?matukio makubwa ambayo yalipaswa yazibitiwe na idala kama ufisad wa Richmond,Tanglord,Meremeta,EPA,DOWNS na utoroshwaji wa wanyama hai na ndege za kijeshi za nje?Mauji na vitendo vya kikatili zidi ya watu na viongozi maarufu kama kuteswa na kupigwa kwa Dk Ulimboka na
Absalom Kibanda,kupigwa risasi na kujeruhiwa kwa padri Ambros,kumwagiwa tindikali kwa shekhe huko Zanzibar,kukabiliana na mihemko ya kidini,kisiasa na kikabila ni jukumu lao pia na sasa limetokea leo huko Arusha,
kama kweli idala hii ingekuwa macho na hai ingewezekana vipi kwa mharifu wa leo aliefanya kitendo hiki kupanga na kutekeleza kitendo cha kulipua mlipuko huo bila hata kutiliwa mashaka na kukamatwa,ama watuambie imekuwaje,ama wanatufanyia ajenda setting kutusahaulisha kashfa inayomkabili katibu mkuu wa CCM bwana Kinana kutuhumiwa bungeni kwa kashfa ya ujangili wa meno ya tembo?watuambie ukweli na vipi kwa viongozi wake kuwajibika hapa namaanisha mkuu wa kitengo hiki Othman Rashidi na naibu wake Jack Zoka,wanasubiri nini kuwajibika?[/h]
ray2:Kwa hisani ya john Mnyika FB group