Tunashuhudia amani kwa mara ya mwisho Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunashuhudia amani kwa mara ya mwisho Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ujengelele, Sep 24, 2010.

 1. U

  Ujengelele JF-Expert Member

  #1
  Sep 24, 2010
  Joined: Jan 14, 2008
  Messages: 1,256
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  FFU wavamia kijiji, watembeza mkong'oto

  23 September 2010 | Mahija Mpera | Mwananchi

  WATOTO wawili hawajulikani waliko huku watu kadhaa wakiwa wamejeruhiwa na mali zao kuharibiwa baada ya kundi la askari wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), kuvamia na kuwashushia kipigo kikali wananchi kwenye Kijiji cha Msongola.

  Habari zilizolifikia gazeti hili jana zimeeleza kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia jana kijiji hicho kilicho Kata ya Msongola, Ilala jijini Dar es Salaam.

  Lakini, kamanda wa polisi wa Ilala, Faustine Shilogile alikataa kuzungumzia tukio hilo akieleza kuwa litatolewa ufafanuzi na kamanda wa Kanda ya Dar es Salaam.

  Ofisa mtendaji wa Kata ya Msongola, Oliver Mwashikia aliiambia Mwananchi kuwa "askari hao waliingia nyumba moja baada ya nyingine na kuwapiga watu waliowakuta bila kujali ni wazee, vijana au watoto na kuharibu kila kitu walichokiona mbele yao".

  Ofisa huyo alisema kuwa chanzo cha tukio hilo ni askari wenzao wawili kupigwa na wanakijiji hao usiku wa kuamkia Jumanne iliyopita.

  Aliendelea kueleza kuwa askari hao walipigwa usiku wa manane baada ya kufika kijiji hapo wakimsindikiza mkazi wa Kimara jijini Dar es Salaa, aliyefika kumdai fedha zake mkazi wa kijiji hicho waliyemtaja kwa jina la Mwinga Chacha.

  Kwa mujibu wa mtendaji huyo, askari hao walifika nyumbani kwa Chacha majira ya saa 6:00 na mkazi huyo wa Kimara aliyekuwa akimdai Chacha fedha baada ya kumkopesha dawa za kuku.

  Alisema: "Baada ya mdai huyo kufika, askari walimtaka afungue mlango, lakini Chacha akakataa. Ndipo purukushani zilipoanza na kusababisha majirani kuamka na kuanza kupambana na askari hao.

  "Mwashikia alisema baada ya kuona wamezidiwa nguvu, askari hao walikimbia na kurudi kesho yake na wenzao hao wakiwa na magari manne.

  "Wakavamia kijiji hicho na kuanza kuwachapa wanakijiji," alieleza.

  Mwashikia alisema baadhi ya wanakijiji walijeruhiwa katika tukio hilo ambalo pia lilihusisha uharibifu wa mali nyingi na kusababisha watoto wawili kutoweka na hadi sasa hawajulikani walipo.

  Watoto waliopotea ni Mwita Mohano na Kasaya Mohano ambao ni wa familia moja.

  Habari zaidi zilieleza kuwa askari hao wanadaiwa kutoka kituo cha polisi Sitakishari, Ukonga na kwamba walivamia kijiji hicho wakiwa na magari manne aina ya Lanrover Defender juzi asubuhi.

  Mmoja wa wanakijiji hao, Subira Mwita alilieleza gazeti hili kuwa askari hao walifika nyumbani kwake na kumuulizia baba na mama yake.

  Alisema, alipowajibu kwamba wote wawili wako kazini, walimtishia kwa silaha kisha wakaingia ndani na kuvunja redio.

  Mkazi mwingine ambaye hakutaka kutajwa gazetini alieleza kuwa asubuhi ya siku ya tukio hilo, aliondoka na kwenda kazini kwake ambako ni karibu tu na nyumbani.

  "Ilipofika saa 4:00 asubuhi, nilisikia sauti za risasi zikilia na baadaye kidogo akasikia mtoto wake akilia,"alisema.

  Alisema baada ya matukio hayo aliamua kurudi nyumbani ambako aliwakuta askari hao wakiwa ndani ya nyumba yake na wakivunja ndoo.

  "Mpaka nimefika tayari walishavunja ndoo tatu na kuchukua fedha taslimu Sh100,000. Waliponiona wakaanza kunipiga virungu," alisema.

  Akieleza kwa uchungu, mama huyo alisema kuwa anashangaa maaskari hao kuwafanyia unyama wanakijiji hao hasa watoto na kinamama ambao hawana kosa lolote

  "Ndugu mwandishi hicho kipigo nilichokipata nikikufunulia nguo utanionea huruma. Mwili umeharibika kwa kipigo na walikuwa wananiambia twende huku nikawaambia nina mtoto mdogo wa miezi sita ndipo waliponiachia,"alisema mama huyo.

  Mwanakijiji mwingine ambaye pia hakutaka kutajwa jina lake gazetini alilaani kitendo hicho akikiita cha kinyama na kinyume na dhamana waliopewa askari ya kuwalinda wananchi.
   
 2. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #2
  Sep 24, 2010
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Nchi ya amani na utulivu lakini usiojali utawala wa sheria na haki. Polisi kazi yao kubwa inatakiwa iwe kuwalinda raia na mali zao lakini hapa nchini polisi ni kama vile wanatayarishwa kwa majukumu makuu mawili - jukumu la kwanza kuwalinda viongozi wa CCM na serikali na la pili kupambana na wananchi. Mchagueni Dr. Slaa tuweze kuondokana na huu uonevu wa vyombo vya dola na dhulma ya watawala kwa kuunda katiba mpya.
   
 3. b

  baajun JF-Expert Member

  #3
  Aug 9, 2012
  Joined: May 19, 2012
  Messages: 200
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tanzania mara kwa mara inajifanya mstari wa mbele kutatua migogoro ya wenzetu mfano Zimbabwe,Kenya,Sudan,Congo,Rwanda na Burundi.sasa inashangaza kuona sisi ndio tunataka vita.

  Inasikitisha kuona wabunge wetu ambao wamepewa dahamani wanataka kutuingiza kwenye balaa ambalo linawezekana kutatuliwa mezani.tunajua wana janja yao.kwani mambo ya siasa yamewabana sana humu nchini.wanataka watu wasiongelee mambo ya akina ulimboka,katiba,m4c,ufisadi na mengineyo.

  Jamani watanzania tuwe macho na busara.hawa wabunge waliongea au kutaka kuleta vita tusiwachague tena,kwani hawana vision na busara.akili zao zinaona hapa na si kule.mungu ibariki tanzania na watu wenye busara.
   
 4. Sakoyo

  Sakoyo Senior Member

  #4
  Aug 11, 2012
  Joined: Aug 23, 2010
  Messages: 135
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimemkumbuka mbunge mmoja ambaye alishawahi kusemakuwa huwezi kusema Tanzania kuna amani wakati kuna watu wanakufa kwa njaa,wengine wanabambikiziwa kesi, wanakosa huduma za afya, rushwa iliyokithiri nasasa nadhani imevuka mipaka mpaka imefika kwenye mhimili wa mwisho yani bunge[ilianzia Serikalini ikaenda Mahakama na sasa Bunge!]. Jamaa waliotafitiwakitumia vigezo (criteria/variables) anuwai kama “uwazi, rushwa za kimataifan.k.) wametuletea list hii kwa Afrika huku Tz tukiwa wa 56 Duniani na hatupohata 5 bora Afrika, hebu nisikuchoshe….
   

  Attached Files:

 5. Kakende

  Kakende JF-Expert Member

  #5
  Oct 16, 2012
  Joined: Aug 18, 2012
  Messages: 2,734
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kwa hali tuliyonayo sasa hivi ya udini Tanzania itageuka kuwa Nigeria muda si mrefu. Radio imani na CD za chuki zinazosambazwa kwa ajili ya chuki dhidi ya dini zingine hasa wakristu ni dalili tosha kwamba sasa inabidi tukae mkao wa vita.

  Kwa hii kasi ya Radio imani na shehe Ponda tuombe mungu serikali ijayo mwaka 2015 iwe imara katika kutafuta suluhisho za hali ilivyo sasa

  Ni jambo la hatari kuona serikali imekaa kimya huku wakijua hali inakuwa mbaya siku hadi siku, serikali imeshindwa kukaa na akina Ponda na Radio imani na kuwahoji shida yao ni nini? hivyo kuweza kuchukua hatua stahiki.

  Ni jambo la ajabu kuona udini na chuki vinachochewa adharani: Mfano ukienda kwenye mihadhara ya waislam, asilimia 90 ya muda inatumika kutukana dini ya Kikristo lakini hakuna hatua inachukuliwa.

  Waislam wamejifunza sasa kuwa wakristu ni wapole, serikali ni pole kwa hiyo wanaweza kufanya jambo lolote

  Waislam wanadai kuonewa kila kona ya dunia mfano: Mombasa Kenya, Mali, Nigeria na maeneo mengine duniani ndo maana makundi ya kigaidi yamekuja kasi.

  Waislam wa Tanzania bado kidogo wanatafuta confidence ya kuunda kikundi maalum cha kivita, kama hakuna hatua inachukuliwa Tanzania itakuwa sehemu hatari kuishi, tegemea mtu kulipuka muda wowote kwenye daladala
   
 6. SENGANITU

  SENGANITU Member

  #6
  Oct 16, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 50
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hongera kwa mada yako nzuri sana.Nakushauri uipeleke kwenye jukwaa la siasa,hapa ni mambo ya elimu tu!!! sawa mkuu?
   
 7. m

  mbish Member

  #7
  Oct 16, 2012
  Joined: Oct 27, 2011
  Messages: 85
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  hakuna vita bana, we kama unataka vita tafuta nchi yako ukapigane tz hakuna vita, hayo yalikuwepo tangu zamani na yatapita tu.
   
 8. m

  mpigauzi JF-Expert Member

  #8
  Oct 16, 2012
  Joined: Jul 17, 2012
  Messages: 275
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu CCM wanaona ndo mtaji
   
 9. Bartazar

  Bartazar JF-Expert Member

  #9
  Oct 16, 2012
  Joined: Oct 4, 2011
  Messages: 805
  Likes Received: 95
  Trophy Points: 45
  Umechanganya madesa mkuu, hili ni jukwaa la elimu?
   
 10. I

  IKORI Member

  #10
  Oct 17, 2012
  Joined: Oct 9, 2012
  Messages: 72
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  amani tz ipo na itaendelea kuwepo sana tu wasiwasi chadema ikiingia ikulu duuhh!! Vita itakuwepo maana wanauchu wa madaraka na vijana tunasukumwa tu na wanasiasa wala hata hakuna sera na mawazo ya vijana ila ni kufuata tu!
   
 11. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #11
  Oct 17, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,339
  Likes Received: 19,517
  Trophy Points: 280
  kwani vita si vimeshaanza? Kitendo cha kushambulia makanisa sio vita? Kwa nini waliingia kanisania na kuiba sadaka na kuchana chana biblia?
   
 12. mtumishidc

  mtumishidc JF-Expert Member

  #12
  Oct 19, 2012
  Joined: Mar 7, 2012
  Messages: 488
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Ndugu wanajamvi matukio ya hivi karibuni ya upotevu wa amani yanaliondolea taifa letu ile sifa yake adhimu ya kutambulika kama kisiwa cha amani, lengo la uzi huu ni kutaka kuweka kumbukumbu sawa kuwa haya yanatokea nchi ikiwa mikononi mwa CCM na hivyo ni vyema tukaliweka bayana kuwa ile amani iliyojengwa kwa ushirikiano mkubwa kati ya wananchi na mpendwa wetu baba wa Taifa, mwl Nyerere ndiyo hiyo inayoteketezwa rasmi katika utawala huu dhaifu wa awamu hii.yafuatayo yanadhihirisha hilo;

  1.kwa nini utawala hasa taasisi ya urais imekuwa ikishindwa kukemea na kuzuia mapema yale yote yanayoiweka amani yetu rehani?
  2.Kwa nini utawala hasa viongozi wetu wamendelea kuwadanganya wananchi, mfano katika usimamizi makini wa sheria na utoaji wa haki?
  3.kwa nini utawala huu wa ccm umeamua kwa makusudi kuwanyima wananchi huduma za msingi, mfano elimu bora na hivyo kuzalisha Taifa lisilofikiri wala kuona thamani ya maisha yao?
  4. pengo kubwa la kiuchumi kati ya wananchi lengo na matokeo yake ni nini?
  5.tukio la leo tarehe 19/10/2012 la kuruhusu Jeshi la wananchi kuranda randa barabarani lina maanisha nini na lina uhalali kisheria au ndio kazi imekamilika ya kuiondoa amani tz na sasa jeshi linajiandaa?

  majibu ya maswali haya yanahitimisha kwa mtazamo wangu kuwa amani iliyozaliwa wakati wa awamu ya kwanza imekufa rasmi katika utawala wa awamu ya nne!

  hivyo ni vyema tukaelewa tunaelekea 2015 amani tukiwa tuimeizika rasmi 2012 na kwa sababu hiyo hata mwaka 2015
  hakutakuwa na chama kingine cha kulaumiwa isipokuwa kile kilichoiua amani mapema, CCM MNAWAJIBIKA!

  tafakari pamoja nami!
   
 13. Mkwawa

  Mkwawa JF-Expert Member

  #13
  Oct 25, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 195
  Trophy Points: 160
  Nimekuwa leo nikisikiliza mahojiano ya BBC/swahili yaliowahusisha Bi kijo kisimba, J. Makamba, Mjengwa, na prof abdula kutoka Zanzibar na wachangiaji mbali mbali kuhusu hali ya amani nchini hasa vurugu za Mbagala, na Uamsho Zanzibar. majibu ya wote yanaonyesha kukataa tamaa na kuchoka huku kila mmoja akimkumbuka Nyerere kwa kazi kubwa aliyofanya ya kujenga Taifa la watu wamoja kama mataifa ya Ulaya na nchi nyingi zilizoendeleo miaka ya 60. ila leo viongozi wetu wameshindwa kabisa.

  Kila mmoja ameonekana kuogopa sana kuzungumzia tatizo lililopo kwa undani wakibakia kuligusia juu juu kwani ni hulka ya watanzania kuogopa kuongelea mambo muhimu kwa kisingizio cha yanagusa hisia kubwa za dini za watu.

  Ukweli ni kwamba Mbagala tatizo ni mtoto kukojelea kitabu kitukufu cha dini ya kiislamu. Hili ni kosa tena ni kukosa la watoto wa siku hizi kukosa malezi bora, heshima kwa wakubwa na ibada. Kizazi cha sasa waislamu kwa wakristu hawawalei watoto wao kwenye misingi ya dini, heshima, na nidhamu. Leo hii mwalimu shuleni akimwadhibu mtoto asubuhi mzazi atakuja kama mbogo kwa mwalimu. Watoto hawaendi misikini wala makanisani wamejaa mitaani kucha kutwa.

  Dini zimekuwa vitega uchumi mwenye fedha anawekeza miiko na maadili yote pamoja na mafundisho ya dini yamepotea kabisa. Viongozi wa dini wanahubiri chuki, utengano, uhasama, na kila aina ya maovu dhidi ya wanadamu wenzao na kupandikiza mbegu ya uhasama badala ya upendo, amani na kuvumiliana.

  Misikiti ilitumika kuhubiri udini badala ya kuona tatizo lilikuwa ni la kitoto lilofanywa na mtoto tena mtaani, lilikuwa limalizwe kwa kumkemea mtoto na kumfundisha kuwa kile ni kitabu kitakatifu wasikichezee wala kukitumia vibaya. Baada ya mahubiri yale yaliyozaa kwenda polisi kumchukua mtoto ili kumpa adhabu, hasira zikaishia makanisani kwa kuchoma, kuiba, kuharibu sehemu ya kuabudu. Hapa busara haikutumika kabisa.

  Zanzibar wao wanadai muungano uvunjike prof. kasema kule dini na siasa ni kitu kimoja. Na wanadai matatizo yao yanaanzishwa napolisi. Ila bado tatizo linakuja pale pale kila hasira inapotawala na kikundi cha uamsho hupelekwa kuchomwa makanisa.

  Polisi nao wamelaumiwa kwa kushindwa kufuata sheria za nchi kutoa ulinzi kwenye mikutano na maandamano ya mani ili wananchi kufikisha jumbe zao bila kubughudhiwa.

  Wanasiasa wameonekana ni chanzo kikubwa cha amani tete TZ kwani hutumia nyumba za ibada ili kushinda na kupandikiza chuki za kidini ili kupata kura za dini husika. Hili limeanza miaka ya hivi karibuni ila limeota mizizi tangia uchaguzi wa 2010. Wakati wa kampeni walitumia utengano wa kiimani kuwagawa watanzania kwa faida ya kura sasa wameweza kutugawa na kuacha balaa mitaani. Siasa na dini zimezaa chuki, fujo, na kasheshe za kutosha.

  Tufanyeje: Kila mtanzania ambaye anaona amani ni muhimu lazima ashiriki kulijenga upya taifa hili linalozama, bila kujali dini yake au itikadi yake ya kisiasa.

  Lazima tushiriki kwa uwingi kueleimishana kuhusu umuhimu wa kuvumiliana na kuendelea kuishi kama ndugu huku tukisherehekea idd, xmass, nk pamoja kama zamani.

  Tuheshimu dini za wengine tusiingilie uhuru wa kuabudu wa wengine.
  Mihadhara yote ya dini isitumike kukashifu dini nyingine au hata wale wasio na dini.

  Wahalifu waonwe wahalifu na vyombo vya sheria badala ya kuwaona dini fulani ndio chanzo cha fujo.

  Chief Mkwawa wa Kalenga
  Dini ziwe chanzo cha furaha na kumtafuta Mungu.
   
 14. O

  Otorong'ong'o JF-Expert Member

  #14
  Oct 25, 2012
  Joined: Aug 17, 2011
  Messages: 31,111
  Likes Received: 10,468
  Trophy Points: 280
  Wale wa raia Burundi wameongea kwa uchungu sana..Wanaionea Tanzania huruma jamani..
   
 15. Columbus

  Columbus JF-Expert Member

  #15
  Oct 25, 2012
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 2,010
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Hii hali sasa ni tete kweli, nilikuwa najenga nyumba yangu hapa Dar nimeamua kuacha kuendelea na ujenzi kwa sababu nimegundua siku sio nyingi watanzania tutakuwa wakimbizi. Sijui watanzania tukiwa wakimbizi tutakimbilia wapi?hakuna nchi inayotuzunguka ambayo inaweza kuubeba mzigo huu.

  Hali hii nadhani inamhusu mtu yeyote mzawa wa Tanzania ukiachilia hao akina Farid na Ponda ambao tumeelezwa sio wazawa, Farid ni Myemen na Ponda ni Mkongo sasa wao wanauchungu gani wakati ndugu zao hawako hapa, nyumba,mashamba na mali zao haziko hapa, mashemeji,mashangazi na wazazi wao hawako hapa.

  Ndugu zangu watanzania tuamke, tujitambue kwamba tusitumiwe na mamluki hawa kwa sababu yoyote ile. Sababu ya kuhatarisha amani yetu haiwezi kuwa kubwa kwani ni akili zetu ndio zinazokuza haya pamoja na uchochezi wa mamluki.

  Serikali hii tuliyoiweka madarakani tunaiambia kudumisha usalama wa nchi hii mlioukuta muulinde, hili sio ombi imeelezwa kwenye katiba iliyowaweka madarakani.
   
 16. Mkwawa

  Mkwawa JF-Expert Member

  #16
  Oct 25, 2012
  Joined: Jun 8, 2011
  Messages: 1,291
  Likes Received: 195
  Trophy Points: 160
  Viongozi wa kasheshe hizi sio wazawa kumbe wa TZ ??? Mhh kweli changanya na zako. Mimi naamini bado tunaweza kuilinda amani yetu. Ila ukweli kabisa serikali inahusika kabisa kuvuraga amani hii. Lazima wote tuheshimu sheria za nchi na uhuru wa kuabudu. Vikundi vyote vya kichochezi na ambavyo havifanyi kazi kwa mujibu ya maombi ya usajili wao vifutwe. Na wale wote wanaotumia dini kuvunja sheria waathibiwe kwa kosa lao sio kosa la kidini. Mungu atusaidie kwani wote walianza hivi hivi mwisho wakimbizi. Hauna sehemu nzuri ya kuishi kama TZ kama hamwamini leteni kasheshe tuwe wakimbizi halafu tutasomanamba.
   
 17. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #17
  Oct 25, 2012
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,031
  Likes Received: 3,228
  Trophy Points: 280
  Dini ziache kuwandanganya waumini kuwa kitabu kimeshushwa, na ukikojolea unageuka mjusi au tembo.
   
 18. M

  MLO Senior Member

  #18
  Oct 25, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 120
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Tarehe 14/03/1995 Nyerere alisema tunataka mtuchagulie mtu anayewiwa na haya
  1 rushwa
  2 umaskini
  3 udini
  4 ukabila
  Nyerere amekufa nayo
  asante
  lakini viongozi tunaowachekea ndiyo wanatuua huku wakicheka
   
 19. J

  John W. Mlacha Verified User

  #19
  Oct 25, 2012
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 3,515
  Likes Received: 540
  Trophy Points: 280
  wale waburundi waliongea kwa uchungu na kwa huzuni sana kana kwamba nchi ni yao
   
 20. T

  Ti Go JF-Expert Member

  #20
  Oct 25, 2012
  Joined: Jun 28, 2012
  Messages: 361
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 60
  Pia watoto wetu ni wadadisi, tunapofundisha dini, tusiwatishe kwa maelezo ya uongo. watataka kujaribu kuona ukweli wake ukoje? Yule mtoto alichofanya si kudharau kitabu kitakatifu, alijaribu kuona ukweli ukoje.
   
Loading...