Tunashabikia UEFA Champions League lakini pesa anayolipwa bingwa wa EPL ni kubwa zaidi

.
mkuu samahani embu fafanua kidogo hapa,,fainali ya play off championship ni ya kumtafta mshindi wa 3 atakaepanda ligi kuu pamoja na bingwa na mshndi wa 2,sasa anapataje hela nyngi kulko bingwa wa epl!??? je mshindi wa 2 na bingwa wa championship?
Huyu jamaa kajichanganya.
 
Kwani mshindi wa UEFA analipwa sh ngapi wewe mbona hutoi mchanganuo wa bingwa wa UEFA anakusanya sh ngapi???
 
Mbona fainal ya play off ya championship ya uingereza bingwa anapata pesa nyingi kuliko bingwa wa EPL na UCL?

Stoke city wakiwa mabingwa hawawezi kupewa pesa atakazopewa United hata kama wakiwa nafasi ya 10.
Hapana sio kweli EPL wana utaratibu team zote league ikiwa inaanza team zote mgao sawa bila kujali position, mfano Milion 100, sasa pesa inazidi kutokana na position % fulani lakini kubwa team ambayo itakuwa kwenye live games nyingi pesa ina add kila mechi unaweza kukuta team ya pili inapata zaidi ya bingwa. Hii ilitokea wakati wa kina Suarez walikuwa wa pili lakini sababu walikuwa team ina burudisha na ilikuwa top pick katika live games wakapata pesa nyingi zaidi ya City. Tofauti ya Spain wakubwa wanajadili mkataba wao maana ndio wanauza zaidi ila kwa sasa wanataka kubadili wawe kama EPL. hii ndio sababu ya EPL teams kuwa tajiri.
 
Hivi ni Chelsea gani hapo unayoiongelea hapo na kwa kipindi gani?
 
Bingwa msimu huu 2017/2018 ni man city Chelsea ni wa tano huo ubingwa kauchukulia wapi
 
.
mkuu samahani embu fafanua kidogo hapa,,fainali ya play off championship ni ya kumtafta mshindi wa 3 atakaepanda ligi kuu pamoja na bingwa na mshndi wa 2,sasa anapataje hela nyngi kulko bingwa wa epl!??? je mshindi wa 2 na bingwa wa championship?
Championships ina timu 24. Mbili zinapanda daraja moja kwa moja. Hawa ni bingwa na mshindi wa pili. Mshindi wa 3,4,5,na 6 wanacheza play off kupata timu ya 3 itakayopanda daraja kucheza EPL.

Baada ya kucheza zinabaki mbili. Fainal inapigwa pale Wembley. Mshindi wa hii vame ndio anapata pesa nyingi kuliko yule bingwa wa UCL na Epl.

Kwa kuongeza. Kwenye mashindani yote ngazi za club barani ulaya fainal ya championship bingwa ndio anapata pesa nyingi kuliko mabingwa wa makombe mengine barani ulaya. Iwe laliga, Serie A, Ligue 1 na hata Bundasliga...
 
Upo sawa. Vp kwenye fainal ya championship?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…