Tunarudishwa nyuma sana na siasa za Tanzania

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
6,619
8,770
Kwa sisi ambao tuko ughaibuni tunaona TZ kwa mwanga tofauti kidogo. Badala ya kuangalia matukio ya vichekesho vya kila siku kama babau seya na hata serious issue kama Lissu kupigwa risasi vilevile tunaangalia nchi kwa ujumla. Tatizo kubwa ni swali ambalo wengi wa watu wanajiuliza ni kisiasa zaidi wa CCM wanajiuliza tunafanyaje kukabiliana na upinzani na kukaa madarakani na Upinzani wanajiuliza tufanye nini tushinde.

Sana ni nani kwenye nchi yetu anajiuliza je ili TZ tushinde tunahitaji nini? nani jamani maana tungekuwa tunajiuliza hivi tusinge gombana kabisa CCM, CUF wala Chadema ?

Mimi binafsi mfano nafikiria naangalia TZ kwa hivi. Data kutoka CIA factbook ni kwamba TZ umri wa kati ni miaka 17-18 na 66% ya watu wako chini ya miaka 25. Tujiulize hapo basi je kwa nchi yetu ilipo sasa na watu wake tufanye nini kama nchi kuendelea? Tukianzia hizi data hapo na kukubaliana basi tunaona maendeleo kwa mwanga tofauti. Mfano kwasababu ya population yetu swali la msingi ni elimu gani tuwape watoto wetu sasa ili waweze kushindana miaka 10-20 ijayo? Elimu bure haitoshi maana swala ni ushindani je watoto wetu watakuwa na kiwango gani ndiyo swali muhimu?. Swali la pili Je nchi yetu ilivyo kubwa ni jinsi gani tunaweza kupeleka maendeleo kwa watu wa chini.... tumeanza haya umeme, barabara na maji ... lakini hakuna mkazo mkubwa kwa nchi....

Watendaji wa serikali kwenye siasa jiulizeni je upinzani unaweza kutusaida vipi kwenye uongozi bora na kupunguza rushwa? . Siwezi kuelezea yote lakini niaanze na mawazo kwanza kwa riais nitarudi na mengine

"Watanzania wengi tunataka Magufuli afanikiwe. Lakini kuwa Raisi sio kazi ndogo kwasababu kuna watu wanakushauri kwa manufaa binafsi ya kichama, kuan watu wanataka kupata nguvu kupitia migongo yako, na kuna viongozi ambao wanafikiria wanajua kila kitu. Tatizo kubwa sana la Magufuli na uongozi wa sasa inaonekana hawana plan. Hawana plan ni kwasababu wanajaribu kuendesha nchi kwa jinsi wanavyofikiria wakati huo na kibaya zaidi ukifanya hivyo mara nyingi nchi itakushinda kwasababu kuna kelele nyingi sana.

Hivyo kuna wanaosema hatushauri sasa mimi najua Magufuli anatakiwa kuanzia wapi na matatizo yako ni yapi. Na ni nini kitafanya maendeleo ya nchi yaanze kuonekana na furaha kwa nchi. Kwasasa hakuna anayefurahia chochote Tanzania. Nitaandika vitu hatua moja moja kuwasaidia


1. Ajiri team ya pricewaterhousecooper ikishirikiana na Mhasibu mkuu wa nchi kufanya yafuatayo

a. Kuchunguza utendaji wa idara zote za serikali na utendaji wake

b. Kutoa report ya kuongeza ufanisi kwenye kila idara hasa kwenye kuweka technologia, kupunguza wafanyakazi wasio wa lazima, kuunganisha idara zinazofanya kazi moja n.k…

c. Kuweka hatuna za kuchukua za utekelezaji wa hiyo plan bila kujali faida za kisiasa

Hii step ya kwanza itasaidia kujua tuko wapi, idara ambazo si za lazima na kutakuwa na plan ya utekelezaji.Utaratibu wa sasa wa viongozi wa kisiasa kufanya maamuzi hautasaidia maana wengine hawana ujuzi lakini vilevile wengine hasa viongozi kuwa na budget kubwa ni faidia kwao hivyo hawawezi wenyewe kupunguza matumizi ya ofisi zao maan itakuwa ni kujipunguzia power zao kitu ambacho ni kigumu. Hii inatakiwa kufanya na sharia lisilo na siasa wala agenda nyingine ya siri.

2. Achane ya vyombo vya habari. Waache watu waongee lolote , chochote kile na serikali iwekeze kwenye kukuza uchumi tu. Uchumi ukikuwa watu wanafurahia hautahitaji polisi wala uhasama. Na kikubwa hii vita huwezi kushinda

3. Ruhusu vyama vya siasa kuwa free na kufanya mikutano. Uhasama wa sasa hausaidii nchi na vievile ujue kwamba skendo kubwa za rushwa zimeletwa na upinzani. Ukiwa na wale wanaokuita mzee kila wakati huta kaa ujue ukweli . Lakini kikubwa corruption itaongezeka badala ya kupungua. Watakaonufaika sio TZ wala wewe ni viongozi binafsi wa CCM. Be careful kwenye hili utaka nchi ifanikiwe au CCM… ni vitu tofauti hivyo.

4. Fanya mpango wa uangalizi upya wa kodi. Kodi zetu sio zote nzuri na nyingi ziko juu sana na kupunguza uwekezaji. Kodi ziwe zina stimulate maendeleo

5. Fanya kufungua biashara iwe rahisi. Tuachane na milolongo ya kufungua biashara hakuna sababu maana wafanyabiashara ni walipa kodi.

6. Bank: Serikali isikope kutoka bank za ndani hii itapunguza riba za bank

7. Kila Mtanzania awe na kitambulisho na vitumike kila mahali hii itasadia sehemu nyingi sana. Vilevile kuwe na address za nyumba wanazoishi kwenye vitambulisho.

8. Ajiri watu wenye uzoefu sio wasomi wasio na uzoefu mfano hakuna wafanyabiashara kwenye baraza lako na wengi wa Dr, Prof hawajui chochote kuhusu utendaji wa kazi. Research za kishue hazisaidii sana kwenye utendaji.

9. Unda team maalumu za mapendekezo ya mabadiliko ya mifumo kama Afya, Elimu, Land, Kilimo….. mifumo ya sasa imepitwa na wakati sana. Unda team ambayo tena… ina watu wenye uzoefu wa hizo sehemu sio wasomi wasio na uzoefu na ziweke utendaji na plan zote.

10. Sikiliza ushauri sio kutoka kwa wana siasa pekee bali wapinzani, wafanyabiashara, wanafunzi, NGO’s na wengine wengi

11. Achana na vyombo vya sheria . acha view huru sasa tunaona mahaka ya rushwa inachagua makossa, kuna video za rushwa lakini hakuna washitakiwa! Polisi kwenye siasa achana na haya itaweka future mbaya ni si ya lazima.


Kikubwa Magufuli angalia sana sera zako. Ili Tanzania iende mbele haihitaji wewe kuwa na nguvu zaidi bali wewe kuwa na nguvu pungufu. Maana kesho na kesho kutwa akija mwingine na ana power zote uliyofanya yote anaweza kufuta kwa mwaka mmoja tu. Hivyo kama unapenda TZ ni lazima upende demokrasia kwa manufaa ya nc"

Kamundu
 
Kilimo kinadidia na kuelekea Shimoni

Tunafuata Sera za ujenzi tu.....HAPA KAZI Tu

Kuna viwanda Bila Malighafi?

Wingi wa vijana wako kwenye Boda Boda na hata viongozi wakuu wanatoa boda boda kuwaunga mkono..Nani anafanya Kilimo?

Vijana wengi ni walinzi...Mgambo, JKT etc

Wachache wanaolima mazao ya chakula wataacha, maana kuna bugudha ya kuuza mazao yao....

Kila mkulima atakimbilia mazao ya biashara

Bora niache kulima mahindi, ili nilime Kahawa, Katani au Tumbaku


Hao Wanyonge wanaosemwa watajikwamua vipi kiuchumi?

Wanyonge ni kina nani?

FAO LA KUJITOA - ni fursa kwa mtanzania kupata mtaji na kuanzisha Kilimo....Mabenki masharti yake ni magumu mno

Hii Slogan ya "Tanzania ya Viwanda" ni kauli ya kuombea kura

Wanyonge ni mtaji wa wanasiasa uchwara

Kuwa masikini ni sifa nzuri Tanzania

Tanzania tunafuata Ujamaa?
 
Mawazo mazuri lakini hakuna wa kusikiliza. Hasa hiyo ya kuwaondoa maprof na madoctor darasani na kuwapeleka field ni dhambi kubwa. Mkuu anaharibu kote kote. Anaondoa utaalamu vyuo vikuu na kufanya ofisi za serikali ziendeshwe na maprof ambao ni kama interns ambao wako ktk mazoezi kutoka darasani! Shame on Tz yetu.
 
Mkuu Kamundu , nimesoma tu kidogo ila ntarudi.

Kwa harakaharaka, population ya Tanzania, majority ni bijana.(66% Of population is below age 25)

Halafu pia nchini mwetu, kila kinacholipa kwa hao vijana ni siasa. Kwahiyo wote wanakimbilia huko, haijalishi kama wana uwezo au la, alimradi ndipo pesa zinapopatikana kwasasa.

Viongozi wetu wa awamu hii, hususan mh rais, wameshutumiwa kutumia mamilioni kununua wanachama wa upinzani! Hilo linaconfirm fikra za hao vijana kuwa kuna pesa kwenye siasa.

Na pia wanafahamu kwenye siasa kuna michongo mikubwa mikubwa ya mafisadi ambao wanawndelea kula mema ya nchi hata baada ya kufanya ufisadi.

Ushauri unaoutoa, ni mzuri sana towards fixing this problem.

Ni ushauri utakaosaidia kuondokana na ujinga ulioligubika Taifa kwasasa!
 
Back
Top Bottom