Tunapoteza na kuchezea rasilimali

Victor Mlaki

JF-Expert Member
May 1, 2016
3,564
3,472
Sijafanya utafiti ila kwa haraka tu hili linaonekana, hatujafikia hatua ya kuheshimu na kutumia rasilimali zetu katika mfumo ambao unaweza kutufanya tupige hatua kimaendeleo ingawa tunaimba maendeleo kila siku.

Mathalani suala la rasilimali muda; Tumekuwa wachezeaji wakubwa wa muda kuanzia ngazi ya familia mpaka Taifa kwa mfano tukiangalia hata masaa ya kazi kwa watumishi bado ni machache ukilinganisha na Nchi nyingine lakini pamoja na uchache huo"masaa 9 kwa siku na masaa 45 kwa wiki"bado wengi tunalalamika na kuyaona ni mengi ingawa ndani ya masaa hayohayo ya kazi ukifuatilia kwa makini kuna upotevu mkubwa sana wa muda unafanyika

Suala la raslimali watu: Katika maeneo ambayo bado Taifa letu linapata hasara kubwa pia ni suala la raslimali watu, kuna upotevu mkubwa ambao kuuelezea bila utafiti inawezekana ukapunguza picha halisi ya uhalisia upotevu ambao unakua kila siku.

Kuna rasilimaliwatu kubwa ambayo imekaa kama akiba na haifanyi lolote katika wakati huu ambao tunahitaji wazo na matumizi ya wazo la kila mtu nchini ili kuifanya Tanzania kuwa bora zaidi, so hivyo tu kuna "brain drain" kubwa sana katika Taifa letu Rasilimali watu ambayo ilipaswa kabisa kuwepo ndani ya Nchi yetu tunaona ikitafuta malisho mabichi nje ya Nchi huku remmitance inayorudi ni kama haisadii na mchango wao mkubwa ni huko waendako na siyo walipotoka.

Mazingira mazuri ya ndani ni muhimu sana katika kupunguza makali ya tatizo hili.

Uwekezaji Mkubwa nje ya Nchi: Hili ni jambo mojawapo linalosababisha kuchelewa sana kupiga hatua kwa Nchi yetu kimaendeleo, uwekezajivwa ndani na wazawa ni muhimu sana kuliko kukimbiakia kuwekeza nje kabla ya ndani, hii itasadia sana kuimarisha Investment base ya eneo, hata mataifa ya nje wanaokuja kuwekeza Nchini ukifuatilia utamaizi kuwa wana msingi imara wa kiuwekezaji ndani ya Nchi zao "investment base" kumiliki mahoteli Dubai, Marekani na Ulaya huku Nchi yako ina msingi dhaifu wa kiuwekezaji ni kukosa UZALENDO NA UCHELEWESHAJI WA HATUA MUHIMU ZA KIMAENDELEO.

Msingi mbovu wa Ujasiriamali: Katika Mataifa ambayo yanapaswa kujiangalia vizuri kwenye suala la ujasiriamali Tanzania haipaswi kukwepa, Watu wengi wanapoteza fursa zinazotolewavna kumbo la wakati kila siku kutokana na aina ya fikra walizonazo zilizowafanya hata wasomi wengi hususani wahitimu wa vyuo vikuu kuwa watu wanaowaza Mara zote kusubiri ajira badala ya kutengeneza ajira, jambo hili limelitia Taifa hasara kubwa kuliko hata ile ya "Wafanyakazi hewa" kwa sababu watu wamekuwa watu wa kisubiri huku wakati umeendelea kupita na kuacha fursa nyingi mno lakini kwa sababu walio wengi tujikuta tunawaza kusubiri

Fursa zimekuwa zikipita mbele yetu na sisi tunasubiri Ajira.
Tumeduwaa mahali pamoja kwa muda mrefu sana huku tukimtafuta wa kumlaumu na kusahau kuwa hata sisi ni wa kulaumiwa, ukitaka kuhakikisha juu ya hili fanya utafiti juu ya idadi ya wananchi waliowaza na kutengeneza ajira (waajiri) halafubangaliabwaajiriwa na wanaosubiri kuajiriwa ni wangapi)utaona tuna tatizo kubwa kiasi gani.

Itaendelea...​
 
Back
Top Bottom