Raimundo
JF-Expert Member
- May 23, 2009
- 13,416
- 12,607
Mkuu mfano wako ni mzuri lakini tunaona ya kwamba jongoo pamoja na tabu yote aliyoipata hakuwa na uwezo wa kuimegua ile sehemu iliyokufa ya mwili wake hadi pale alipopata msaada...
Je kwa madhila yatupatayo sisi, je tuna uwezo wa kuyamegua wenyewe na kuyatupilia mbali ili yasitughasi?
Kweli, binadamu amehusika ktk kuiondoa hiyo sehemu iliyokufa. Na binadamu kwa Jongoo ni mbingu na ardhi, so kwa maneno mengine ili nasi tuondoe sehemu zetu zilizokufa tunahitaji nguvu ambayo ni kubwa zaidi yetu, ambayo ni devine intervention ili tuwe wepesi na huru.
Inawezekana kabisa
Na moja kati ya namna inavyowezekana ni wewe kusoma hii kitu hapa
Kwanza umeona kuwa kuna mizigo-hilo ni jambo la msingi sana kwani kuna wenye mizigo na hawajui ni mizigo
Pili umeona kuwa inawezekana kuachwa- hilo nalo ni jambo la msingi sana kwani kuna wanaojua kuwa wana mizigo lakini hawaamini kama inaweza kuachwa
Tatu ni wewe kutafuta namna ya kuitua-hili linaweza kufanywa kwa namna nyingi tu!
Huko kuona kwenyewe kwamba umebeba mzigo kunahitaji intervetion kama Kaunga alivyosema, achilia mbali kujitua/kuukata huo mzigo.
Mfano rahisi ni kama vile mtu akiachana na mpenzi wake anaweza kusahau hayo machungu kama atapata mpenzi mwingine, tunaona pia jinsi mtu akifiwa na mtoto wa pekee hali inavyokuwa ngumu kusahau, lakini akiweza kupata mtoto mwingine ni rahisi kusahau, kwa maana nyingine mpenzi mpya (mfano wa kwanza) au mtoto mpya (mfano wa pili) wametumika kusaidia kuitua ile mizigo kama ilivyo kwa yule mtoto aliyemsaidia jongoo.
Sisi wenyewe hatuwezi.
Last edited by a moderator: