Tunapotembea na sehemu za miili yetu zilizokufa....!

Tunapotembea na sehemu za miili yetu zilizokufa....!

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,443
[h=3][/h]
photolibrary_rf_photo_of_grandfather_and_grandson.jpg

Mzee mmoja, Salim Keni wa Makongorosi huko Chunya mkoani Mbeya, anasema kuwa siku moja alishangazwa sana na kauli ya mtoto wake wa miaka kumi. Anasema alikuwa amekaa nje ya nyumba yake jioni. Hapo alipokuwa amekaa alikuwa akiangalia jongoo. Jongoo huyo alikuwa ameumia sehemu yake ya nyuma, ambayo sasa ilikuwa imekauka, yaani imekufa.

Sehemu ya mbele ambayo ilikuwa ni nzima iliunganishwa na sehemu hiyo ya nyuma au ya mkia kwa kiuzi kidogo sana. Tunaweza kusema kwamba sehemu hiyo ya mkia ilikuwa inakokotwa na ile ya mbele. Hali hiyo ilimfanya jongoo yule kupata shida sana ya kusogea. Ukweli ni kwamba, hata kama sehemu ile ya nyuma ya jongoo yule ingeondolewa wala asingebaini, kwani ilikuwa sio sehemu ya mwili wake tena-ilishapoteza uhai.

Lakini aliendelea kuikokota kama vile bado alikuwa akiihitaji. Wakati Mzee Salim akimshangaa jongoo yule, mtoto wake huyo ambaye ni mtundu sana alifika hapo, ambapo naye alimuona jongoo huyo. Alikaa chini karibu na baba yake na kumkodolea macho kabla hajatoa kauli hiyo ya kushangaza. ‘Sasa baba, huyu mdudu si anapata shida bure, kwa nini asiache hii sehemu ya nyuma ili atembee vizuri, kwa sababu yenyewe imekauka…..’

Kabla baba yake hajajibu, mtoto yule alichukua kijiti na kutenganisha sehemu ya mbele na ile ya nyuma ya jongoo yule. Baada ya kufanya hivyo, jongoo yule aliweza kuongeza kasi ya kutembea na alionekana wazi kwamba amekuwa huru.

Mzee Salim alishikwa na butwa kwani hakuwa amepata muda wa kufikiri hivyo wakati akimtazama yule jongoo. Ni kweli kabisa, mtoto wake alikuwa amemfunulia kitendawili kikubwa sana cha maisha. Ya nini kutembea na sehemu ya mwili ambayo haina kazi, ambayo imekufa, ambayo angeweza kuiacha na kuwa huru zaidi?

Mtoto yule aliona wazi kabisa pamoja na akili yake ya kitoto kwamba, kama mdudu yule angemudu kuiacha sehemu ya mwili wake ambayo ilikuwa tayari imekufa angeweza kuishi katika uhalisia.

Uvumbuzi wa mtoto yule ni uzumbuzi wetu sote. Ni lini nasi tutaamua kuacha sehemu zetu ambazo zimekufa ili tuweze kuishi katika uhalisia? Sehemu zetu za miili zilizokufa ni zipi? Ni maumivu ya kimaisha yaliyopita. Ni mizigo ya mashtaka ya dhamira zetu na haja yetu ya kutaka kulipiza visasi. Ni masikitiko na majuto ya mambo yaliyopita, ambayo bado yanatuumiza hadi leo, mambo ambayo hayana maana yoyote tena kwetu.

Wengi wetu tunatembea au kuishi na mizigo mizito sana ya mambo yaliyopita, mambo ambayo ukweli ni kwamba hayana maana yoyote kwetu. Lakini kwa sababu tumeamua kutembea nayo, hutuzuia kwenda kama tunavyotaka, hutuzuia kufurahia maisha na hutuzuia kuwa huru katika mambo yetu mengi kimaisha.

Bila shaka tukiwa jasiri kama mtoto yule na kubaini sisi wenyewe kwamba tunatembea na sehemu zetu ambazo zimekufa, tutakuwa tayari kuziondoa na kuwa huru. Ni vizuri kujiuliza kama kuna mambo yaliyopita ambayo yanatuzuia katika kufanya na kufikia malengo yetu, ambayo yanatunyima furaha na kutufanya tujione kama watumwa. Je mambo hayo yana maana gani kwetu wakati yameshapita? Ni wazi yamekua, tunayabeba bure.

Kuna ambao wanalia hadi leo kufuatia vifo vya wapenzi wao vilivyotokea mika kumi iliyopita. Kuna wanaohangaika kutaka kulipa visasi vya yale mabaya waliyotendewa miaka kadhaa nyuma. Kuna wale ambao wanasumbuliwa na mawazo ya jinsi walivyofilisika au kusalitiwa na jamaa au wapenzi wao. Hii yote ni mizigo ya bure, ni sehemu za miili au maisha yao ambazo zimekufa, lakini wanaziburuza.

Nimekuwa nikiandika hapa mara kwa mara kwamba mambo yaliyopita hayapaswi kutuumiza, kutuondolea furaha na kutufanya tujihisi wanyonge na tusio na thamani, kwa sababu mambo haya hayana maana yoyote tena kwetu. Hata kama utafikiri kwa miaka mia kuhusu jambo fulani ambalo tayari limekutokea, huwezi kulibadili hata kwa chembe ndogo sana, sanasana unalipa uzito ili likutese zaidi.

Ili uishi hasa, uishi kwa kadiri ya utashi wa kanuni za kimaumbile, inakupasa uondoe sehemu ya mwili wako ambayo imeshakufa. Bila kuiondoa sehemu hiyo, ni lazima utaelemewa sana.
 
Word, ila l wish ingekuwa rahisi kama kukata kucha au kunyoa nywele.
Kuna past hazisahauliki na zingine zimesaidia sana watu kuwafanya wawe smart zaidi. Mjanja ni yule anayetumia bad experience ili kuboresha real time experience. I dont wanna be a naive girl l used to be, so watesi wangu wamenipandisha kwenye higher level. I mean wamenitoa kwenye comfort zone na kunifanya nifanye nisiyo yategemea.
Hata kifo cha dada yangu mpenzi kimenifanya nifanye ambayo sikuyafikiria. Maana baada ya kujiona niko mwemyewe imebidi nigangamale (as we say in nyamwezi) na kuyatazama maisha ktk mtazamo mwingine.
Kuishi kwenye past ni tofauti na kukumbuka past.
 
Mkuu mfano wako ni mzuri lakini tunaona ya kwamba jongoo pamoja na tabu yote aliyoipata hakuwa na uwezo wa kuimegua ile sehemu iliyokufa ya mwili wake hadi pale alipopata msaada...

Je kwa madhila yatupatayo sisi, je tuna uwezo wa kuyamegua wenyewe na kuyatupilia mbali ili yasitughasi?
 
Kweli, binadamu amehusika ktk kuiondoa hiyo sehemu iliyokufa. Na binadamu kwa Jongoo ni mbingu na ardhi, so kwa maneno mengine ili nasi tuondoe sehemu zetu zilizokufa tunahitaji nguvu ambayo ni kubwa zaidi yetu, ambayo ni devine intervention ili tuwe wepesi na huru.
 
Nzuri Sana,Yahitaji moyo ya utayari wa kuyaacha yaliyopiita,hasa yale yaletayo majonzi mioyoni mwetu
 
ni kweli kabisa, kuna vitu vinaweza kukuumiza sana lakini vikawa ni sababu ya mafanikio yako, kila ukivikumbuka unatamani uongeze mbio ili kufika unapotaka!
 
Kweli, binadamu amehusika ktk kuiondoa hiyo sehemu iliyokufa. Na binadamu kwa Jongoo ni mbingu na ardhi, so kwa maneno mengine ili nasi tuondoe sehemu zetu zilizokufa tunahitaji nguvu ambayo ni kubwa zaidi yetu, ambayo ni devine intervention ili tuwe wepesi na huru.

Naam ni kweli kabisa mkuu kwa hili hitimisho ulilolibainisha...

Maneno haya hapa chini ya Mtambuzi ambayo kayatumia kama hitimisho la habari yake yalinipa ushawishi wa kutaka kudadisi zaidi je kwa uwezo wa kibinadamu tunawezaje?

Ili uishi hasa, uishi kwa kadiri ya utashi wa kanuni za kimaumbile, inakupasa uondoe sehemu ya mwili wako ambayo imeshakufa. Bila kuiondoa sehemu hiyo, ni lazima utaelemewa sana.
 
Last edited by a moderator:
Naam ni kweli kabisa mkuu kwa hili hitimisho ulilolibainisha...

Maneno haya hapa chini ya Mtambuzi ambayo kayatumia kama hitimisho la habari yake yalinipa ushawishi wa kutaka kudadisi zaidi je kwa uwezo wa kibinadamu tunawezaje?

HOW; is a one million dollar question. Ni rahisi sana kusema acha hiki na hiki, lkn linapokuja kwenye swala la JINSI ya kuacha huwa ni changamoto, maana njia moja yaweza fanya kazi kwa mwingine lkn isifanye kwa mwingine lkn ukifuata NJIA (the only way ambayo pia ni kweli na uzima) basi hakuna kinachoshindikana.
 
Last edited by a moderator:
Je kwa madhila yatupatayo sisi, je tuna uwezo wa kuyamegua wenyewe na kuyatupilia mbali ili yasitughasi?

Inawezekana kabisa

Na moja kati ya namna inavyowezekana ni wewe kusoma hii kitu hapa

Kwanza umeona kuwa kuna mizigo-hilo ni jambo la msingi sana kwani kuna wenye mizigo na hawajui ni mizigo
Pili umeona kuwa inawezekana kuachwa- hilo nalo ni jambo la msingi sana kwani kuna wanaojua kuwa wana mizigo lakini hawaamini kama inaweza kuachwa
Tatu ni wewe kutafuta namna ya kuitua-hili linaweza kufanywa kwa namna nyingi tu!
 
Mizigo kwasisi wanadamu ipo ya aina nyingi Mfano Mtu hubeba Matendo aliyofanyiwa zamani labda niongelee kuhusu kitu kama msamaha, mi naamini hamna kitu kigumu kama Kusamehe na kusahau hasa kusahau pale ambapo pameachwa kovu maana kila siku wewe utakuwa waliona kovu hilo na kukukumbusha ni kwa jinsi gani ulivyopata kidonda!!! Kiukweli inahitaji nguvu ya ziada kuweza kuondoa mzigo kama huu sawa na alivyosema Kaunga..

But in reality ulichosema ni ukweli wa 100% kwani ukiweza kusamehe na kusahau inakuwa ni rahisi kwako kuendelea kwenda mbele kwa kasi nzuri zaidi

thnx Kwa uzi wako broo Mtambuzi
 
watu8 na Kaunga tupo pamoja

Kwa upande mwingine tuwe kama mtoto kusaidia wengine wanaoteseka na wameshindwa kujikwamua

Bado mimi hiyo naiita devine intervention, maana Mungu hutumia watu kuokoa au kusaidia if you may waja wake. I agree ni wito mzuri kusaidia wengine kutoa hizo sehemu zilizokufa ktk miili yao. Unapomfariji mfiwa naamini unaounguza .00001kg ya kimzigo chake, unapomsaidia yatima kumlipia ada pia unapinguza gram kadhaa za dead load ktk maisha yake.
 
Last edited by a moderator:
dat is true pia nguvu ya ziada(mungu)inahtajika sana ili kuweza kutambua hayo pia moyo ndo kila kitu ucpoponywa moyo hatutaweza.
 
Kweli, binadamu amehusika ktk kuiondoa hiyo sehemu iliyokufa. Na binadamu kwa Jongoo ni mbingu na ardhi, so kwa maneno mengine ili nasi tuondoe sehemu zetu zilizokufa tunahitaji nguvu ambayo ni kubwa zaidi yetu, ambayo ni devine intervention ili tuwe wepesi na huru.

Kuna msemo mmoja unasema kwa pale ulipoingilia mwiba ndipo unapotokea

Kwenye suala hili ni kuwa namna lilivyoingia ndivyo linavyotoka,yaani kama mambo yaliingia kwenye mawazo yako kwa njia ya kuyaamini basi na ndivyo yatakavyoondoka

Mfano:
Ulikuwa na mume/mchumba na akakuacha,kwasababu ulikuwa unampenda sana baada ya kukuacha umeona kuwa hakuna kama yeye na ukaamua kuamini hivyo na ndiyo ikawa namna yako ya kufikiri,umefanikiwa kuanzisha mahusiano mengine na yamekufa kwasababu ya imani yako kuwa hakuna kama wa mwanzo.

Ili uondoe huo mzigo ulionao ni vilevile tu kama ulivyoanza kuubeba,yaani kwa imani
Anza kujiambia kama ulivyokuwa unajiambia kuwa hakuna kama huyu,jiambie wapo wengi sana,fanya hivyo kila unapokumbuka kuwa hakuna kama huyo na taratibu utaona mabadiliko na hatimae utaondoka kwenye hiyo imani

Kuna namna nyingi sana ya kuondoa hiyo mizigo kama vile tahajudi [meditation] kuzungumza na WEWE n.k

Inawezekana kabisha!
 
Uzi mzuri, na wachangiaji wamejitahidi kutoa mazuri..nimefurahia hii topic..
Jongoo hakuficha dead part or mzigo wake unaomsumbua, aliuonesha na akapata msaada. Hivyo sisi Binadamu tusifiche matatizo yetu share na shirikisha watu waliokuzidi kama sio umri basi hata busara, sio rahisi kushare matatizo yetu kwa sababu binadamu tuna aibu ndio maana mtu ni rahisi kuja kupost thread hapa jf kuliko kuliko kumfuata mtu kumwomba ushauri. Tusaidiane kwa kila hali ili kujikwamua kwa matatizo yaliyopita ambayo yanatuganda na kutusumbua katika maisha yetu.
 
mi naamini hamna kitu kigumu kama Kusamehe na kusahau hasa kusahau pale ambapo pameachwa kovu maana kila siku wewe utakuwa waliona kovu hilo na kukukumbusha ni kwa jinsi gani ulivyopata kidonda!!!
Siku zote matatizo yanaanzia hapo

Umetoa wapi hii kitu?
Ukijiuliza hilo swali tu utagundua kuwa umelitengeneza wewe mwenyewe na umeamua kuliamini

Hakuna kitu rahisi kama kusamehe ndugu yangu,hiyo imani yako ifute tu na utaona kila kitu ni rahisi.Tunachokosea ni kule kutengeneza imani sisi wenyewe na kuzikubali kuwa ni kitu halisi utadhani hata zina ushahidi wa hali halisi

Huwa tunajidanganya sana kwenye eneo hili!
 
Kuna msemo mmoja unasema kwa pale ulipoingilia mwiba ndipo unapotokea

Kwenye suala hili ni kuwa namna lilivyoingia ndivyo linavyotoka,yaani kama mambo yaliingia kwenye mawazo yako kwa njia ya kuyaamini basi na ndivyo yatakavyoondoka

Mfano:
Ulikuwa na mume/mchumba na akakuacha,kwasababu ulikuwa unampenda sana baada ya kukuacha umeona kuwa hakuna kama yeye na ukaamua kuamini hivyo na ndiyo ikawa namna yako ya kufikiri,umefanikiwa kuanzisha mahusiano mengine na yamekufa kwasababu ya imani yako kuwa hakuna kama wa mwanzo.

Ili uondoe huo mzigo ulionao ni vilevile tu kama ulivyoanza kuubeba,yaani kwa imani
Anza kujiambia kama ulivyokuwa unajiambia kuwa hakuna kama huyu,jiambie wapo wengi sana,fanya hivyo kila unapokumbuka kuwa hakuna kama huyo na taratibu utaona mabadiliko na hatimae utaondoka kwenye hiyo imani

Kuna namna nyingi sana ya kuondoa hiyo mizigo kama vile tahajudi [meditation] kuzungumza na WEWE n.k

Inawezekana kabisha!

Kijana wa miaka 9 kapoteza wazazi wake wote wawili, atajiambiaje kuwa hawajafariki au kwamba atapata wazazi wengine?

Maumivu ya mapenzi sio sawa na ya kupoteza mtu uliyekuwa unamtegemea au kupoteza kiungo muhimu cha mwili.

Sikubishii kuwa hiyo yaweza kuwa moja ya njia inayoweza fanya kazi kwa baadhi ya watu.
 
Kijana wa miaka 9 kapoteza wazazi wake wote wawili, atajiambiaje kuwa hawajafariki au kwamba atapata wazazi wengine?
Ukishasema mtoto tayari unakuwa unazungumzia binadamu ambae uwezo wake wa kufikiri sio sawa
Hajui uchungu wa kufiwa

Halafu sijui ni kwanini unasema kuwa anahitajika ajiambie kuwa hawajafariki
Pia sijui ni kwanini unafikiri ni jukumu lake kufikiria kuhusiana na wazazi wengine

Ukisha sema mtoto kila kitu kinaondoka
Maumivu ya mapenzi sio sawa na ya kupoteza mtu uliyekuwa unamtegemea au kupoteza kiungo muhimu cha mwili.
Kuna jambo unatakiwa ulijue

Jambo lenyewe ni kuwa kiwango cha maumivu ni wewe unakipanga na wala sio mwingine hivyo hata kusema maumivu ya tukio A sio sawa na maumivu ya tukio B ni wewe umepanga kwani kuna mtu anaona vise versa na wewe kwenye hayo matukio hayo mawili

Sio sawa kudhani kuna kikubwa na kidogo bali jichagulie kile ambacho hakikuumizi
Sikubishii kuwa hiyo yaweza kuwa moja ya njia inayoweza fanya kazi kwa baadhi ya watu.
Siyo baadhi ya watu ni kwa kila mtu!
 
Back
Top Bottom