Tunapoitafakari Siku Ya Uhuru Wa Vyombo Vya Habari Duniani...

maggid

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2006
Posts
1,084
Reaction score
1,251
Ndugu zangu,

" Maisha yetu huanza kuisha siku tunapoanza kunyamaza kwenye mambo yenye maana"- Martin Luther King Jr.

Leo Mei 3 ni Siku ya Uhuru wa Vyombo Vya Habari Duniani. Hapa Afrika Mashariki, siku hii inaazimishwa kule Arusha kwa Kongamano lililoandaliwa na Mfuko wa Ruzuku kwa Vyombo Vya Habari ( TMF).

Macho na masikio yetu yanaelekezwa Arusha. Maana, kule Arusha kunatarajiwa kuzinduliwa kwa Itifaki ya Vyombo Vya habari.

Ndio, kuna Azimio la Arusha linakuja, lakini hili linawahusu Wanahabari. Na kauli mbiu ya Siku hii ya Vyombo Vya Habari ni " Mazingira Mazuri na Salama ya Kufanyia Kazi Kwa Wanahabari wa Afrika Mashariki".

Ni ukweli, kuwa mwanahabari hawezi kuwa huru kwenye mazingira mabaya na yasiyo salama ya kufanyia kazi. Lakini, kuna maswali ya kujiuliza na kutafakari kwa kina. Ni natumaini yetu walio kule Arusha wataifanya kazi hii ya kufikiri. Wafanye hivyo ili Azimio watakalotoka nalo Arusha liwe lenye maana kwa wanahabari na umma unaowatumikia.

Na mwanahabari anapokuwa hana uhuru wa kiuchumi kimsingi anawekwa kwenye mazingira mabaya na yasiyo salama ya kufanyia kazi.

Hakika, Media ni mhimili muhimu sana katika nchi yeyote inayotaka kupiga hatua za kweli za maendeleo. Hata hivyo, katika nchi zetu hizi, media imefanywa kuwa adui wa watawala na hivyo basi, wakati mwingine kumekuwa na mahusiano ya uhasama, kuviziana na kuwindana.

Na kwa umma, media nayo ina sehemu yake ya lawama pale inaposhiriki kubomoa badala ya kujenga misingi ya Utaifa na Ujenzi wa Taifa Huru lenye nguvu za kiuchumi. Ni pale, inaponyamaza kwenye mambo ya maana na kushabikia yasiyo na maana, yenye kupotosha na kusababisha chuki na migongano katika jamii. Mathalan, udini, ukabila na mambo ya abrakadabra kama vile ndoto za Babu wa Loliondo na Kikombe chake.

Na hakika hili huchagizwa pale Media inapoingiliwa na wanasiasa, wafanyabiashara na hata baadhi ya viongozi wa dini. Ni matokeo ya Media kukosa uhuru wa kiuchumi. Ni wakati sasa wa vyombo vya habari na wanahabari kwa ujumla wake, kudai haki za kuwa na trade unions zake zenye meno. Kudai pia haki ya kupewa ruzuku na Serikali inayotokana na kodi za wananchi ili vyombo hivyo viweze kujijengea uwezo zaidi katika kuitumikia jamii. Media ya nchi haiwezi kuishi kwa kutegemea ruzuku inayotokana na walipa kodi wa Ulaya na Marekani. Ni fedheha pia.

Ndugu zangu,

Mengine tunayoyashuhudia siku hizi ni kwa baadhi ya vyombo vya habari kushabikia mambo yasiyo na maana na kunyamazia yale ya msingi. Hii ni hatari kwa mustakabali wa nchi zetu hizi.

Na tusije kusahau kuwa umma bado una imani kubwa kwa media. Hivyo, kuna umuhimu wa kuzingatia maadili. Inahusu virtue, kwa maana ya maadili na kutenda yalo ya haki. Kutenda yalo mema.

Mtu mwenye maadili mema utamwamini, ndivyo pia wasemavyo Waingereza; a virtuous person is someone you can trust.

Mzazi anapaswa kuwa a virtuous person, kiongozi wa kisiasa anapaswa kuwa a
virtuous person, kiongozi wa kidini anapaswa kuwa a virtuous person, Mwandishi wa habari anapaswa kuwa a virtuous person. Vivyo hivyo kwa mwalimu.

Ndugu zangu,

Wanahabari wa Kenya kuelekea Uchaguzi Mkuu wao uliopita wameonyesha kuwa inawezekana, kwa Media kutanguliza maadili, kuachana na yasiyo na maana na kujielekeza kwenye yaliyo ya msingi na yenye kulinda Umoja na Utaifa wao.

Na katika haya ya kushabikia yasiyo na maana, kuna wakati Julius Nyerere alitua Jomo Kenyatta Airport. Hapo aliongea na wanahabari. Ni miaka ile ya mwanzoni mwa Uongozi wa Rais Mwinyi baada ya Nyerere kung'atuka. Enzi za Mwinyi kuna mambo yaliyoonekana yana nafuu zaidi. Kukawa na minong'ono, kuwa eti Julius Nyerere anamwonea wivu Mwinyi na ana mipango ya kumwondoa madarakani.

Pale Jomo Kenyatta mwanahabari wa Kenya akamwuliza Nyerere: " Mwalimu tunasikia unapanga njama za kumwondoa Mwinyi madarakani na hata Rais Moi wa hapa Kenya!"

Julius Nyerere alijibu, " Hivi wewe ukiambiwa mimi natembea na mama yako, utakimbilia kwenda kuandika habari hiyo?!"

Naam, tunajifunza nini kwenye jibu hilo la Julius Nyerere?

Kwamba kwenye falsafa tunaambiwa, kuwa unapoletewa jambo kuna matatu ya kuyaangalia na kuyazingatia: Udadisi wa uhalisia wa jambo lenyewe (Reasoning), Mantiki ( Logic) na Ulinganishi wa nadharia ( Metafisiki)

Hivyo basi, unapokutana na mtu akakuambia kuwa alipokuwa akitembea jana usiku, njiani alimwona mbwa akimtafuna mbwa mwenzake, basi, unachopaswa kufanya ni kutulia na kutafakari.

Yumkini usiku huo mtu huyo alikuwa akitoka kwenye kilabu cha pombe, na kwenye ulevi wake, paka aliyemwona akigombana na paka mwenzake, kwake ilikuwa ni mbwa anayemtafuna mbwa mwenzake!

Happy Media Freedom Day!

Maggid Mjengwa,

Iringa.

0754 678 252
http://mjengwablog.co.tz
 
Asante kutukumbusha!, kumbe siku yetu leo!. Wengine tulishaisahau siku nyingi tangu tulipoacha rasmi kazi za newsroom!.

Thanks.

Pasco.
Mwandishi wa habari wa enzi hizo.
Kwa sasa, anaandika kwa kujitegemea na kujitolea bila kulipwa, hivyo huandika chochote, na kukipeleka chombo chochote cha habari bure kabisa, na hicho chombo kinakuwa huru kutumia au kutokutumia habari/makala zangu.
Pasco.
 
RIP, David Mwangosi, huna lolote, alipofariki Mwangosi ukafanya sherehe, wanadishi wakasusia kuandika habari za Kamuhanda na za Polisi, wewe ukashadadika na kuwaponda waandishe leo ndio unakuja na vimakala vyako, ok issue ya Kibanda, umefikia wapi? ulidhani atakufa?
 
hoja zako ni za mantiki kabisa lakini tatizo la media za tanzania ni 'kuandaliwa' ajenda na wenye kunufaika na ajenda husika!
pole pole tutafika.
 
Julius Nyerere alijibu, " Hivi wewe ukiambiwa mimi natembea na mama yako, utakimbilia kwenda kuandika habari hiyo?!" tunawezaje ku prove kama hii statement kweli ni ya Nyerere? Maana siku hizi watu wanamuwekea Mwalimu maneno mengi kweli na mbaya zaidi bila source yoyote na tunaamini tu.

Mkuu maggid umetoa nasaha nzuri sana.
 
Last edited by a moderator:
Waandishi chini ya chama chao cha Iringa waliweka mgomo, juu ya mauwaji haya ya kikatili
ukatoka kuwatetea askari na kuupinga msimamo wa waandishi..

mwangosi_tanzania_misatanzania_468.jpg
 
Pasco,
Asante sana ndugu yangu. Tupoitafakari siku kama hii tunakumbuka pia tulipotoka. Bado nakumbuka kile kisa cha ziara ya Mkapa Sweden na usafiri wa kufika Uppsala.

Vinginevyo, nafuatilia sana maandiko,najifunza mengi kaka.
Maggid,
Iringa.

Asante kutukumbusha!, kumbe siku yetu leo!. Wengine tulishaisahau siku nyingi tangu tulipoacha rasmi kazi za newsroom!.

Thanks.

Pasco.
Mwandishi wa habari wa enzi hizo.
Kwa sasa, anaandika kwa kujitegemea na kujitolea bila kulipwa, hivyo huandika chochote, na kukipeleka chombo chochote cha habari bure kabisa, na hicho chombo kinakuwa huru kutumia au kutokutumia habari/makala zangu.
Pasco.
 
There are currently 6 users browsing this thread. (3 members and 3 guests)

Tatzo kubwa la mjengwa huwa ni kuset tu ajenda na kukimbia! hajawahi kuanzisha mada na kuendelea kuchangia au kuchangia mada za wenzake yeye huwa ni kuandika tu na sign out ili wenzake wachangie1 sijui alisomea chuo gani huyu jamaa. hapa anaonekana yupo online lakini baada ya dk 5 ana sign out.
 
Waandishi chini ya chama chao cha Iringa waliweka mgomo, juu ya mauwaji haya ya kikatili
ukatoka kuwatetea askari na kuupinga msimamo wa waandishi..

mwangosi_tanzania_misatanzania_468.jpg

naona ajabu kwako Mjengwa, wewe ni moja kati ya waandishi makanjanja. Mjengwa ni kama waandishi fulani wanaoandika habari katika gazeti moja la umbea.
 
There are currently 6 users browsing this thread. (3 members and 3 guests)

Tatzo kubwa la mjengwa huwa ni kuset tu ajenda na kukimbia! hajawahi kuanzisha mada na kuendelea kuchangia au kuchangia mada za wenzake yeye huwa ni kuandika tu na sign out ili wenzake wachangie1 sijui alisomea chuo gani huyu jamaa. hapa anaonekana yupo online lakini baada ya dk 5 ana sign out.

na hii ni tabia yake ya muda mrefu. Ila nadhani anatumia mbinu ya kuwa watu wajadili kwa kile alichokiandika pasipo ufafanuzi wake. Maggidi naomba ueleze vizuri hapo.
 
Pasco,
Asante sana ndugu yangu. Tupoitafakari siku kama hii tunakumbuka pia tulipotoka. Bado nakumbuka kile kisa cha ziara ya Mkapa Sweden na usafiri wa kufika Uppsala.

Vinginevyo, nafuatilia sana maandiko,najifunza mengi kaka.
Maggid,
Iringa.
Duu!, Mkuu Maggid umenikumbusha mbali!

All and all, tuko pamoja sana, hata katika hayo ambayo sio!.

Kinachokufanya wewe Maggid usimame kama wewe, ni msimamo wako usio yumba katika kusimama na kweli!. Utabezwa, utasimangwa, utanyooshewa vidole, utakashifiwa sometimes hata kuwa persecuted ila mwisho wa siku, utakaosimama ni "nothing but the truth!".

Kumbe na wewe huwa unasifia ujinga? ok hayo yenu, mnaweza kutumiana email or uka M-PM, pumba zenu..
 
Duu!, Mkuu Maggid umenikumbusha mbali!

All and all, tuko pamoja sana, hata katika hayo ambayo sio!.

Kinachokufanya wewe Maggid usimame kama wewe, ni msimamo wako usio yumba katika kusimama na kweli!. Utabezwa, utasimangwa, utanyooshewa vidole, utakashifiwa sometimes hata kuwa persecuted ila mwisho wa siku, utakaosimama ni "nothing but the truth!".
Pasco.

Ahsante sana Pasco,
Ilikuwa 1998, Septemba. Nakumbuka pale nyumbani kwa Balozi Samson Kasseka, Mkapa alituambia tulio kwenye mtandao wa kijamii wa Tanzanet kuwa ni wambea!
Social media imekua tangu wakati ule. Na hawa wenye kutukunana na kujadili yasiyo na maana ni part and parcel ya social media. Wana uhuru wa kufanya hivyo na ndio demokrasia.

Shida yangu mimi ni hawa wasiojadili hoja na kujikita kwenye yasiyo na maana na hata kutukana , kwamba mambo yao hayo yanapohamia kwenye mainstream media na hata wakati mwingine kufanyiwa kazi na tuliowapa dhamana.

Tuna safari ndefu, lakini naamini tunapiga hatua za maana.
Maggid
 
we unawajibu wanaokusifia tu? Hujibu wanaojenga hoja ya kukukosoa?
 
CCM,

Ahsante,

Ningependa sana kuziona hoja nikazijibu, lakini kama hakuna hoja za kujibu unafanyaje?Au kama zimeshajibiwa na wengine? Hata hivyo, nikuhakikishie, kuwa nasoma kila kinachoandikwa.
Maggid
 
Ndugu zangu,

" Maisha yetu huanza kuisha siku tunapoanza kunyamaza kwenye mambo yenye maana"- Martin Luther King Jr.

Leo Mei 3 ni Siku ya Uhuru wa Vyombo Vya Habari Duniani. Hapa Afrika Mashariki, siku hii inaazimishwa kule Arusha kwa Kongamano lililoandaliwa na Mfuko wa Ruzuku kwa Vyombo Vya Habari ( TMF).

Macho na masikio yetu yanaelekezwa Arusha. Maana, kule Arusha kunatarajiwa kuzinduliwa kwa Itifaki ya Vyombo Vya habari.

Ndio, kuna Azimio la Arusha linakuja, lakini hili linawahusu Wanahabari. Na kauli mbiu ya Siku hii ya Vyombo Vya Habari ni " Mazingira Mazuri na Salama ya Kufanyia Kazi Kwa Wanahabari wa Afrika Mashariki".

Ni ukweli, kuwa mwanahabari hawezi kuwa huru kwenye mazingira mabaya na yasiyo salama ya kufanyia kazi. Lakini, kuna maswali ya kujiuliza na kutafakari kwa kina. Ni natumaini yetu walio kule Arusha wataifanya kazi hii ya kufikiri. Wafanye hivyo ili Azimio watakalotoka nalo Arusha liwe lenye maana kwa wanahabari na umma unaowatumikia.

Na mwanahabari anapokuwa hana uhuru wa kiuchumi kimsingi anawekwa kwenye mazingira mabaya na yasiyo salama ya kufanyia kazi.

Hakika, Media ni mhimili muhimu sana katika nchi yeyote inayotaka kupiga hatua za kweli za maendeleo. Hata hivyo, katika nchi zetu hizi, media imefanywa kuwa adui wa watawala na hivyo basi, wakati mwingine kumekuwa na mahusiano ya uhasama, kuviziana na kuwindana.

Na kwa umma, media nayo ina sehemu yake ya lawama pale inaposhiriki kubomoa badala ya kujenga misingi ya Utaifa na Ujenzi wa Taifa Huru lenye nguvu za kiuchumi. Ni pale, inaponyamaza kwenye mambo ya maana na kushabikia yasiyo na maana, yenye kupotosha na kusababisha chuki na migongano katika jamii. Mathalan, udini, ukabila na mambo ya abrakadabra kama vile ndoto za Babu wa Loliondo na Kikombe chake.

Na hakika hili huchagizwa pale Media inapoingiliwa na wanasiasa, wafanyabiashara na hata baadhi ya viongozi wa dini. Ni matokeo ya Media kukosa uhuru wa kiuchumi. Ni wakati sasa wa vyombo vya habari na wanahabari kwa ujumla wake, kudai haki za kuwa na trade unions zake zenye meno. Kudai pia haki ya kupewa ruzuku na Serikali inayotokana na kodi za wananchi ili vyombo hivyo viweze kujijengea uwezo zaidi katika kuitumikia jamii. Media ya nchi haiwezi kuishi kwa kutegemea ruzuku inayotokana na walipa kodi wa Ulaya na Marekani. Ni fedheha pia.

Ndugu zangu,

Mengine tunayoyashuhudia siku hizi ni kwa baadhi ya vyombo vya habari kushabikia mambo yasiyo na maana na kunyamazia yale ya msingi. Hii ni hatari kwa mustakabali wa nchi zetu hizi.

Na tusije kusahau kuwa umma bado una imani kubwa kwa media. Hivyo, kuna umuhimu wa kuzingatia maadili. Inahusu virtue, kwa maana ya maadili na kutenda yalo ya haki. Kutenda yalo mema.

Mtu mwenye maadili mema utamwamini, ndivyo pia wasemavyo Waingereza; a virtuous person is someone you can trust.

Mzazi anapaswa kuwa a virtuous person, kiongozi wa kisiasa anapaswa kuwa a
virtuous person, kiongozi wa kidini anapaswa kuwa a virtuous person, Mwandishi wa habari anapaswa kuwa a virtuous person. Vivyo hivyo kwa mwalimu.

Ndugu zangu,

Wanahabari wa Kenya kuelekea Uchaguzi Mkuu wao uliopita wameonyesha kuwa inawezekana, kwa Media kutanguliza maadili, kuachana na yasiyo na maana na kujielekeza kwenye yaliyo ya msingi na yenye kulinda Umoja na Utaifa wao.

Na katika haya ya kushabikia yasiyo na maana, kuna wakati Julius Nyerere alitua Jomo Kenyatta Airport. Hapo aliongea na wanahabari. Ni miaka ile ya mwanzoni mwa Uongozi wa Rais Mwinyi baada ya Nyerere kung'atuka. Enzi za Mwinyi kuna mambo yaliyoonekana yana nafuu zaidi. Kukawa na minong'ono, kuwa eti Julius Nyerere anamwonea wivu Mwinyi na ana mipango ya kumwondoa madarakani.

Pale Jomo Kenyatta mwanahabari wa Kenya akamwuliza Nyerere: " Mwalimu tunasikia unapanga njama za kumwondoa Mwinyi madarakani na hata Rais Moi wa hapa Kenya!"

Julius Nyerere alijibu, " Hivi wewe ukiambiwa mimi natembea na mama yako, utakimbilia kwenda kuandika habari hiyo?!"

Naam, tunajifunza nini kwenye jibu hilo la Julius Nyerere?

Kwamba kwenye falsafa tunaambiwa, kuwa unapoletewa jambo kuna matatu ya kuyaangalia na kuyazingatia: Udadisi wa uhalisia wa jambo lenyewe (Reasoning), Mantiki ( Logic) na Ulinganishi wa nadharia ( Metafisiki)

Hivyo basi, unapokutana na mtu akakuambia kuwa alipokuwa akitembea jana usiku, njiani alimwona mbwa akimtafuna mbwa mwenzake, basi, unachopaswa kufanya ni kutulia na kutafakari.

Yumkini usiku huo mtu huyo alikuwa akitoka kwenye kilabu cha pombe, na kwenye ulevi wake, paka aliyemwona akigombana na paka mwenzake, kwake ilikuwa ni mbwa anayemtafuna mbwa mwenzake!

Happy Media Freedom Day!

Maggid Mjengwa,

Iringa.

0754 678 252
http://mjengwablog.co.tz
Wanabodi,
Leo ni siku ya kimataifa ya uhuru wa habari, kila mwaka sisi waandishi huwa tunakutana mahali kwa siku 2 na kujadili mambo mbalimbali kuhusu uhuru wa habari, na katika mkusanyiko huo, serikali, vyama vya habari na Taasisi za habari hutoa matamko kede kede kuhusu uhuru wa habari, lakini kwa mwaka huu, kufuatia janga la Corona, hakuna maadhimisho yoyote rasmi ya kukutana, ila nilitegemea wizara ya habari, vyama vya habari na mashirika na Taasisi za habari zitoe matamko mbalimbali.

Bado sijabahatika kuona tamko lolote!, ila usikute zile speech huwa zinaandaliwa kwa ajili ya presentations kwenye kongamano hotelini, safari na per diem!, leo hakuna safari, no trip, no per diem, no hotel gathering, hivyo this time hata speech tuu hakuna?!.

Nawatakia waandishi wenzangu, maadhimisho haya ya kimya kimya, nawashauri wale wafadhili mbalimbali wa tukio hili, kwa vile hatukusafiri, wala kula na kulala hotelini, then naomba hao wafadhili watutumie tuu hizo per diem, tutahama majumbani mwetu na kuhamia hotelini 3 days kisha tutatoa matamko.

Paskali
 
Ndugu zangu,

" Maisha yetu huanza kuisha siku tunapoanza kunyamaza kwenye mambo yenye maana"- Martin Luther King Jr.

Leo Mei 3 ni Siku ya Uhuru wa Vyombo Vya Habari Duniani. Hapa Afrika Mashariki, siku hii inaazimishwa kule Arusha !

Happy Media Freedom Day!

Maggid Mjengwa,

Iringa.

0754 678 252
http://mjengwablog.co.tz
Mkuu maggid,
Asante nakuangalia mubashara hapo TBC
MEI 3 ya kila mwaka ni Siku ya Kimataifa ya Uhuru wa vyombo vya habari, Mimi Pascal Mayalla, kwa niaba yangu kama mwanahabari na kwa niaba ya kampuni yangu ya PPR as chombo cha habari, niwatakie wanahabari wenzangu wote, maadhimisho mema ya siku hii, huku nikidurusu, niliwahi kusema nini kuhusu uhuru wa habari Kwa media za Tanzania yetu.

Nawatakia uhuru wa habari mwema.
Paskali.
 
Ndugu zangu,

" Maisha yetu huanza kuisha siku tunapoanza kunyamaza kwenye mambo yenye maana"- Martin Luther King Jr.

Leo Mei 3 ni Siku ya Uhuru wa Vyombo Vya Habari Duniani. Hapa Afrika

Happy Media Freedom Day!

Maggid Mjengwa,

Iringa.

0754 678 252
http://mjengwablog.co.tz
Mkuu maggid, hebu waeleze madogo humu jinsi viongozi Sweden wanavyotumia public transport.

Watu wanapiga kelele Rais Samia kupandishwa basi, hawajui kisa hiki
Mkuu Kishina cha Mshahara, naunga mkono hoja.

Nchi za kiafrika mtu akiishachaguliwa kuwa rais badala ya kuwa humble and down to earth kwa heshima kubwa aliopewa na wananchi wake kuwatumikia kama rais wao, huku ndio kwanza anavimba bichwa, ajajisikia yeye ndio yeye na ndio kila kitu kufikia hatua hata katiba aliyoapa kuilinda inakuwa sio kitu tena! .

Wakati fulani nikiwa nchini Sweden, rais Mkapa akaja katika ziara ya kiserikali, mimi kama mwandishi Mtanzania on working visit to Sweden, nikaribishwa kwenye ziara hiyo ya Rais Mkapa.

Wakati huku rais ananyenyekewa utafikiri Mungu, kule hakuna upuuzi kama huo. Kule Waziri Mkuu (Sawa na rais huku), anaheshimiwa tuu na sio kuabudiwa.

Wakati tunasafiri kutoka Stockholm kwenda Uppsala umbali kama wa kilometers 60 kama Dar -Mlandizi, Mkapa na msafara wake wote na mwenyeji wake na sisi waandishi wote tulipandishwa kwenye basi moja kama dala dala la mwendo kasi. Njiani hakuna kufunga njia bali piki piki mbili zinatangulia ku block njia only few minutes kabla huku pikipiki nyingine mbili zikiwa mbele ya msafara. Msafara ukiishapita road block zile piki piki mbili za msafara zinaongeza mwendo kutangulia mbele ku block the next road block na zile za nyuma zina kabaroff. Kule hakuna upuuzi wa kufunga njia saa nzima kusubiria rais apite!.

Mwenyeji wetu akatueleza kule viongozi wa Kitaifa hadi Waziri Mkuu wao wanatumia usafiri wa serikali kwa kazi za kiserikali na hutumia usafiri wa public or wao binafsi wanapokuwa kwenye safari za binafsi na hakuna escorts. Tena ulinzi uliimarishwa kutokana na kifo cha Olof Palme lakini zamani ukiisha toka kazini Ijumaa ulinzi ni mpaka Jumatatu asubuhi only on working days on working times. Sisi tunaokaa Bagamoyo Rd. zile safari za Msoga enzi za Kikwete, kiukweli tulikoma! . Sijui kwa nini asingekuwa anatumia helcopter! .

Paskali
P
 
Pasco,
Asante sana ndugu yangu. Tupoitafakari siku kama hii tunakumbuka pia tulipotoka. Bado nakumbuka kile kisa cha ziara ya Mkapa Sweden na usafiri wa kufika Uppsala.

Vinginevyo, nafuatilia sana maandiko,najifunza mengi kaka.
Maggid,
Iringa.
Mkuu maggid, hebu wahadithie madogo humu jinsi viongozi wanavyotumia public transport Sweden.
P
 
Back
Top Bottom