Tunapenda kudanganywa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunapenda kudanganywa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Felixonfellix, Jun 19, 2010.

 1. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #1
  Jun 19, 2010
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Je watanzania wanapenda kudanganywa?
  Je watanzania ni wavivu kweli wa kufikiri?
  Je watanzania hawana uwezo wa tenganisha ukweli na uwongo?

  Nimesukumwa na hasira kuleta maswali haya, baada ya kusoma kwenye gazeti moja kuhusu ndoto mpya ya Raisi Kikwete. Ndoto yenyewe inahusu mpango wa serikali (ambao tayari umekamilika) wa kumwezesha kila mwalimu katika nchi hii kuwa na laptop yake, katika kipindi cha miaka mitano ijayo. Hivyo ndivyo serikali inapanga vipaumbele.
  Laptop kwa mwalimu wa Iponyaholo, Bulungwa, Ushetu kwa mfano itamsaidia nini?
  Laptop kwa mwalimu asiye na nyumba imara itaitunza wapi?
  Laptop kwa mwalimu ambaye bado hajafunza matumizi yake?
  Ni Laptop isiyotumia umeme?
  Laptop itachangia asilia ngapi katika kuboresha elimu?
  Hivi kumbe tatizo kubwa la walimu wetu ni ukosefu wa computer?

  Binafsi naelewa kuwa hiyo ni siasa tu ya kutafuta kura za walimu. Lakini swali ni je walimu wetu wanapenda kudanganywa? Kwanini mtu atumia a very cheap lie kuwanasa walimu? Maana yake viongozi wetu wanajua kuna tatizo la ujinga na uvivu wa kufikiri na kutenganisha uwongo na ukweli.

  Mimi naona "Tanzania beyond tomorrow" kama inavyoitwa ndoto hiyo ya Raisi ni tusi kwa walimu wetu na kwa watanzania.

  Nafikiri tunahitaji wakina "Kamau" wengi na "matusi" yao.
   
Loading...