Tunaotafuta wachumba/mke kazi tunayo

Bismack

JF-Expert Member
Mar 12, 2018
387
487
Huyu mrembo kwa mara ya kwanza nilikutana naye jana Jumapili kwa lengo la kufahamiana mana tulikua hatjawahi kuonana, tumekua tukiwasiliana kwa njia ya simu tu.

Sasa mwanaume jana nikajikoki vizuri japo vyuma vimekaza nikampeleka sehemu nzuri yenye hadhi, tukaketi mhudumu akaja akatusikliza akatuleta vinywaji huku nyuma chakula kikiandaliwa tukaanza kupiga story za hapa na pale tukisubili chakula kiwe tayari.

Baada ya mda kidogo huyu mrembo akaniomba simu yangu nikampa alivoishika akaniambia kwanini una simu ya gharama hivi wakati mimi mchumba wako ninatumia tochi? Akaendelea kusema, ninahitaji simu nimechoka kutumia tochi.

Kiukweli yale maneno yalinikera ingawa Mungu alinipa hekima ya kuyajibu vizuri ili asione kama nimeyapokea vibaya, ingawa nilijiuliza maswali kadhaa kichwani kwangu nikajiuliza kwanini asingevumilia siku ya leo ikapita then siku nyingine ndo akaniambia shida zake?

Halafu ndo kwanza tumefika kwanini asingevumilia ukapita hata mda? Inamana kilicho mleta ni kupata simu tu? Sikupata majibu. Baada ya mda chakula kikaja tukala japo nilikula huku kichwa changu hakiko vizuri kabisa.

Kifupi nisiwachoshe wakuu ila nawaomba wadada mjaribu kua wavumilivu, mwanaume rijari lazima atajua unahitaji nini hata kabla hujasema ila siyo kulazimisha kama vile unamkomoa mtu.

Nawasilisha, asanteni.
 
Mm nmeamua kusogeza umri wa kuoa, kwa sasa nawabutua tu ,
Kama huyo wa kwako, unamuahidi utamununulia hiyo smartphone mwisho wa mwezi, then unabaki unabutua mwezi mzima thereafter una mdamp kwenye dustbin!!
 
Kuna kitu umekosea siku ya kwanza ukutakiwa kumpeleka hiyo sehemu na kupata vinywaji mpaka chakula. Tafuta eneo zuri ambalo hakuna vinywaji wala chakula. Hakikisha usikae naye muda mrefu.
 
Tanzania ndo Nchi pekee duniani ambapo ukimtomgoza demu ghafla tumbo lake linaunguruma njaa ya chipsi kuku
 
Bismack
Una bahati huyo kakwambia hitaji lake asee.
...
But natamani utembelee Arusha ukutane na vichwa ngumu vibaka wa kimeru.

Hawa kwanza hawajali kukwambia sijui smart, sijui nini, ila anakuvutia kasi umpeleke mahali unapoishi na ukifanikiwa kumpeleka siku si nyingi.. .

Ukimwamini na kuanza kumuachia funguo, utakuta amefyagia room kaiba vitu...
DADADEKI
 
Mm nmeamua kusogeza umri wa kuoa, kwa sasa nawabutua tu ,
Kama huyo wa kwako, unamuahidi utamununulia hiyo smartphone mwisho wa mwezi, then unabaki unabutua mwezi mzima thereafter una mdamp kwenye dustbin!!
Hakika mkuu
 
Warembo wanapenda vitu vizuri. Well, who doesn't.

Cha kufanya hapo sio kumkimbilia kumla na kumtema. Utawatema wangapi?

Hajakushikia gun, ni kiherehere chako tu kitakacho kuponza.

Cha kufanya, kama unampenda jaribu ku create balance kati ya penzi lako kwake hasa kama unamhitaji kwa future na pia katika kumzowesha kukuthamini na kukuelewa zaidi ya pesa.

Sijui umeelewa?

Strike a balance between letting her know you love her, but cannot always give an arm and a leg to please her.
 
Bismack
Una bahati huyo kakwambia hitaji lake asee.
...
But natamani utembelee Arusha ukutane na vichwa ngumu vibaka wa kimeru.

Hawa kwanza hawajali kukwambia sijui smart, sijui nini, ila anakuvutia kasi umpeleke mahali unapoishi na ukifanikiwa kumpeleka siku si nyingi.. .

Ukimwamini na kuanza kumuachia funguo, utakuta amefyagia room kaiba vitu...
DADADEKI
Ha haha poleee
 
Warembo wanapenda vitu vizuri. Well, who doesn't.

Cha kufanya hapo sio kumkimbilia kumla na kumtema. Utawatema wangapi?

Hajakushikia gun, ni kiherehere chako tu kitakacho kuponza.

Cha kufanya, kama unampenda jaribu ku create balance kati ya penzi lako kwake hasa kama unamhitaji kwa future na pia katika kumzowesha kukuthamini na kukuelewa zaidi ya pesa.

Sijui umeelewa?

Strike a balance between letting her know you love her, but cannot always give an arm and a leg to please her.
nimekusoma sana mkuu, ila nafsi imesha 6
 
Ndugu wala mke usimtafute yeye yupo atakuja tu ila hawa wapenda vizuri watafute nawe uongezemo uzoefu mkuu.
 
Aliyekuambieni kuwa mchumba au mke anatafutwa ninani ""?

hapo ndio huwa mnajichanganya""" MPENZI SAHIHI HUWA ANALETWA MWENYEWE NA MUDA/WAKATI STAHIKI""
SASA KUJIFNYA Mnavamia vamia kama hvyo ""matokeo YAKE ndio hayo ""

pole sana
Mkuu na huyo anaeletwa je amefikaje kwako kama hajakutafuta?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom