Tunaomba tamko la CCM kama uongozi wa Chadema ulivyotoa tamko lao kuhusu muafaka wa Arusha. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunaomba tamko la CCM kama uongozi wa Chadema ulivyotoa tamko lao kuhusu muafaka wa Arusha.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Fasta fasta, Jun 30, 2011.

 1. Fasta fasta

  Fasta fasta JF-Expert Member

  #1
  Jun 30, 2011
  Joined: Feb 15, 2011
  Messages: 620
  Likes Received: 114
  Trophy Points: 60
  [​IMG]
  Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu tamko la kuwafukuza madiwani wote wa chama hicho Jijini Arusha ambao walishiriki kukubali muafaka wa Umeya wa jiji hilo.


  Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetangaza kuwatimua ndani ya chama madiwani wake wote watakaobainika kuhusika na mwafaka wa kilaghai kati yao na madiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na kuwafanya wakubali kupewa nafasi ya Unaibu Meya katika Jiji la Arusha.

  Kadhalika, Chama hicho kimesema kitamweka ‘kiti moto’ Mbunge wa Maswa Magharibi kwa tiketi ya Chadema, John Shibuda, kwa kukiuka makubaliano ya chama na wabunge wenzake kwa kutangaza kwamba atachukua posho za vikao vya Bunge.

  Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk. Willibrod Slaa alitangaza maamuzi hayo jijini Dar es Salaam jana kuwa kuna ushahidi unaoonyesha kwamba madiwani waliokubali mwafaka jijini Arusha walinunuliwa.

  Hata hivyo, Dk. Slaa hakusema viongozi hao walinunuliwa na nani na kwa kiasi gani, lakini alisisitiza kwamba walipewa rushwa ndiyo maana walifanya maamuzi hayo kinyume cha msimamo wa chama.

  Dk. Slaa aliwaambia waandishi wa habari kuwa Chadema kipo tayari kupoteza kitu chochote hata kama ni kitamu kiasi gani ikiwa kitabainika kilipatikana kinyume cha taratibu pamoja na demkorasia.

  MARANDO KUONGOZA UCHUNGUZI
  Dk. Slaa alisema kuwa kwa kutumia kifungu cha 11 cha Katiba ya Chadema, ameunda kamati ya watu watatu itakayoongozwa na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, na Mwanasheria gwiji, Mabere Marando, kuchunguza madiwani waliohusika na mwafaka huo na kila mmoja kwa kiasi gani ili Chama kiwachukulie hatua.

  Wajumbe wengine wa kamati hiyo ni Razaro Maasai ambaye ni Mwenyekiti wa Mameya wa Majiji na Manispaa pamoja na Wenyeviti wa Halmashauri ambazo zinaoongozwa na Chadema na Ester Dafi, wanasheria wa Chadema Makao Makuu.

  Kamati hiyo imepewa siku sita kuanzia jana ili kukamilisha uchunguzi wake na kwamba taarifa itakazopata zitasaidia kuongeza ushahidi wa kuwachukulia hatua madiwani waliohusika katika njama hizo.
  Kwa mujibu wa Dk. Slaa, kuna watu wengi wanahitaji nafasi hizo hivyo Chama hakioni tatizo kuwatimua viongozi wanaokiuka taratibu na sheria.

  Alisema Naibu Meya aliyechaguliwa kupitia mwafaka huo kwa tiketi ya Chadema, Estomiah Mallah, jina lake halikujadiliwa katika kikao chochote cha Chama kama ilivyo kawaida.

  Aliongeza kuwa Chadema ni chama kinachosema ukweli daima na kukemea maovu, hivyo hakiwezi kusita kuwachukulia hatua wanachama wake wote wakiwemo madiwani, wabunge na hata angekuwepo Rais kama watabaini amekiuka taratibu.
  Dk. Slaa alisema madiwani watatu kati ya wanane katika jiji la Arusha ndiyo walioingia kwenye mkutano ambao mwisho wake walitangaza kuwa wamefikia mwafaka na kukubali cheo cha Unaibu Meya.

  Alisema kikao hicho kiliongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mjini, Raymond Mushi, na kwamba idadi ya Madiwani wote ni 21, lakini anashangaa kusikia walioshiriki katika kupata mwafaka huo walikuwa tisa akiwemo mmoja wa TLP na wengine wanne wa CCM.

  Alisema wananchi wa Jiji la Arusha wanachotaka ni kuona haki inatendeka na sio kupata viongozi ambao wamepatikana kinyume cha kanuni, taratibu na sheria za uchaguzi wa meya na naibu wake.
  Aidha, alisema Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe, na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema, waliomba kufanya mazungumzo na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ili kupata ufumbuzi wa suala hilo, lakini wameshangaa kusikia watu wachache wamerubuniwa na kukubali mwafaka kwa njia za mkato.
  Mgogoro wa uchaguzi wa Meya katika Jiji la Arusha ulianza Januari mwaka huu baada ya Chadema walilalamikia mchakato wa kumpa kiongozi huyo.

  Chadema walisema zoezi la upigaji kura kwa ajili ya kumpata Meya liliendeshwa vibaya ikiwemo mjumbe asiyekuwa na sifa za kupiga kura, Mary Chatanda, Mbunge Maalum wa Viti Maalum (CCM), kushiriki kumchagua kiongozi huyo.

  Kutokana na hali hiyo, Chadema kilipinga hatua hiyo na kuandaa maandamano Januari 5, mwaka huu jijini Arusha, ambayo mwisho wake yalisababisha mauaji ya watu watatu yaliyofanywa na Jeshi la Polisi na wengine kujeruhiwa.
  Kutokana na hali kuwa tete na watu kupoteza maisha, Dk. Slaa alisema Chama hakiwezi kukubali kuona mambo yakimalizika kinyemela kwa kivuli cha mwafaka na kwamba kinachotakiwa ni haki na sio kitu kingine.

  Wiki iliyopita, madiwani wa Jiji la Arusha kutoka vyama vya CCM, Chadema na TLP, walitangaza kufikia mwafaka ambapo walikubaliana kwamba Gaudence Lyimo (CCM) aendelee kuwa Meya na Estomiah Mallah (Chadema) ashike Unaibu Meya hadi mwaka 2014 kisha diwani wa TLP achukue Unaibu Meya hadi mwaka 2015 kabla ya kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu.

  Katika mwafaka huo pia waligawana kamati za Baraza la Madiwani.

  Kamati ya Uchumi, Elimu na Afya itaongozwa na diwani wa Chadema; kamati ya Fedha na Utawala itakuwa na wajumbe tisa, wanne kutoka Chadema na mmoja wa TLP, huku CCM ikiwa na wajumbe wanne tu, itakuwa chini ya Meya (CCM) na kamati ya Mipango Miji na Mazingira itaongozwa na diwani wa CCM.

  Taarifa za mwafaka huo ziliwekwa hadharani Juni 20, mwaka huu katika mkutano wa Baraza la Madiwani wa Jiji la Arusha ukihusisha madiwani wote wa CCM, Chadema na TLP.   
 2. N

  Ngekewa JF-Expert Member

  #2
  Jun 30, 2011
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 7,730
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kusema kwa ajili ya kusema tu sidhali CCM watakuwa na wakati?
   
 3. POSHO MAVYEO

  POSHO MAVYEO JF-Expert Member

  #3
  Jun 30, 2011
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 377
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  magamba kupitia kwa Nape wanasema hayo hapo chini mkuu tulisha ambiwa na mwenyekiti anachosema Naye ni sauti ya chama  [​IMG] Nnauye Jr
  Today 02:57 PM
  #1 [​IMG]

  [​IMG]

  Nchi kwanza chama baadae na kinachoendelea Arusha

  Mtazamo WANGU binafsi Arusha madiwani ambao kwakweli NI wawakilishi WA wananchi na bahati mzuri hakuna aliyepinga kuchaguliwa Kwai udiwani, wamekaa na kuamua KUMALIZA tofauti zao, Leo viongozi wao wanapokataa muafaka ule maana yake UZALENDO KWA CHAMA NI MKUBWA KULIKO KWA WANANCHI WA ARUSHA?

  Kwa hili la ARUSHA NILIDHANI INGEKUWA WANANCHI KWANZA, CHAMA BAADAE​

   
 4. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #4
  Jun 30, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,372
  Likes Received: 3,136
  Trophy Points: 280
  Zile sio tofauti za arusha ni tofauti za ccm na chadema yaani ni tofauti ya dhruma na ubabe wa ccm dhidi ya haki ya chadema wala sio mwafaka wa watu21 km ilivyofanyika......ni umbumbu na utovu wa nidhamu kusema ni suala la arusha......ccm haohao watasema suala la watz kuuliwa na polisi kule mara ni suala la mara na si la watz wote w3apenda amani.....huu ndio umbumbu wa ccm na viongozi wao

   
 5. POSHO MAVYEO

  POSHO MAVYEO JF-Expert Member

  #5
  Jun 30, 2011
  Joined: Jun 28, 2011
  Messages: 377
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  well
  ndio magamba wana weka hoja yao subiria watakuja hapa sio muda
   
Loading...