Tunangojea hadi wazungu waandamane kwa ajili yetu??

Angalia pia jinsia, utagundua tofauti kati ya picha hizi mbili. Sijui unajifunza nini?

Wanawake waandamanaji wa uingereza wanakerwa na wizi wa mali za watanzania walalahoi wakati wanaume wa kitanzania wanakerwa na George W. Bush kwa masuala yasiyohusiana na wizi wa mali ya walalahoi wa Tanzania. Nadhani kuna mengi mengine ya kujifunza hapa.
 
This is what I have been saying all along. Hii kitu ya radar is about TZ being ripped off!!
Lakini hukumu iliyotolewa inaonyesha ku-protect biz interests za BAE zaidi.

Let's (TZ) do something jamani....for once! Mwee!!

Hukumu iliyotolewa imeongozwa na mashitaka yaliyofunguliwa na mwendesha mashitaka wa uingereza. Waliwashitaki BAE kwa kosa dogo la kutokutunza record zao sawasawa na siyo kwa rushwa. Na hii ni baada ya makubaliano kati ya BAE na mwendesha mashitaka ambapo BAE walikubali kurudisha fidia kwa Tanzania. Mimi sina shida na hukumu hiyo kwani ni kesi ya waingereza. Tatizo hapa ni la kwetu ambapo wezi na wala rushwa ya rada bado hawahachukuliwa hatua yoyote mpaka sasa.
 
Inasikitisha sana
Sijui uzalendo wetu tumeupeleka wapi? Watz wamekaa kuchukianachukiana na kushabikia mambo ya nje, halafu ya kwetu tunayaacha.
 

Ipo siku yatatimia
 
Hawa wazungu wa BAE waliotuibia ni waislamu ? Hili ni swali kwa yule alieweka picha ya pili hapa ili afuruge kusudi la mjadala huu. Hao wanaoandamana wote kwenya picha ya kwanza na ya pili ni mashujaa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…