Kwa vyovyote zito ni mzoefu sana kuliko huyo deo, Zito ni mwanasiasa makini sana na ukimtuatilia sana utagundua kuwa zito anaakili sana na nimzalendo. Nimemfuatilia sana zito na siasa zake ni mzuri nimemkubali.
Nimemfuatilia sana pia huyu dogo baada ya kugundua chama changu cd hakina mgombea ludewa na kugundua huyu kijana kumbe alikuwa anagumbea kwa mara ya pili, na alianza mapema sana kujiandaa.
Anashomesha watoto wengi sana sekondari, takribani 500 lkn ada ni elfu (20 day) na elfu ishirini (boarding) kwa biashara zake anaweza. Alisaidia karibu kitu fulani kila kijiji, vitu kama vile, computers, kuezeka mashule, misaada makanisani na misikitini.
Kwa vyeo hivi alivyonavyo hamhitaji zito kabwe au yeyete ambebeL-
1. Ni katibu wa uchumi na fedha ccm wilaya Ludewa
2. Ni kamanda vijana wilaya Ludewa
3. Mjumbe wa kamati siasa mkoa Iringa (naafasi ya Mungai) Niligundua alimshinda mungai katika uchaguzi
4. Ni mlezi wa chipukizi Taifa kamati nadhani watu 5 mwenye taarifa anijuze. Yumo na kigoda, kinana nk
5. Sasa hivi ni mjumbe kamati fedha mashirika ya umma
6. Makamu mwenyekiti kamati tajwa hapo juu
7. Sito shangaa akichaguliwa mbunge bunge la afrika
Nilikutana naye Australia alikuja kututembelea, anaonesha kuipenda nchi yake, anaongea kiingereza kizuri sana na kiswahili fasaha.
Hautakiwi kuwa prof. kuona maendeleo endelevu na mipango ya muda mrefu. Naweza nisimpende yeye, lakini ninapenda hiyo profile jinsi anavyoipika. Tumshauri tu asimezwe na makundi kwani kweli hayatamsaidia.
Sio yeye tu, hata kama kuna kijana mwingine wa hulka yake mleteni jamvini ili tumjadili na kumuungoza kwa namna tofauti. Ukiufukia ukweli hapa, utaibukia pale.
4.