Tunalalamika sana?????? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunalalamika sana??????

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Felixonfellix, Oct 15, 2011.

 1. Felixonfellix

  Felixonfellix JF-Expert Member

  #1
  Oct 15, 2011
  Joined: Feb 16, 2010
  Messages: 1,680
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Tunalalamika? Tunapinga? Tunahoji? Tunakataa?

  Watanzania wanapojadili mapungufu ya nchi(national deficiencies), na kuyarudia na kuyarudia, tunaambiwa eti "tunalalamika tu bila kutoa suluhu ya matatizo hayo".

  Suluhu? Nani anasikiliza? Tuitolee wapi hiyo suluhu?

  Wabunge ndio wawakilishi wetu. Ndani ya Bunge?

  Kama Bungeni siasa za vyama na ushabiki wa kisiasa ndivyo vinaamua ni mawazo gani ya "suluhisho, tufanyeje?

  Tumehoji(hatuwezi kupinga maana ni siri tusizozijua) mbona mikataba ya uwekezaji haileti neema iliyotarajiwa?. Hiyo ni siri kati yao (wawekezaji-wengine uchwara-mf wanaouza maua na kufungua gereji!)na maafisa wachache wa (GNTs) na Serikali. Hapo tunatoaje suluhu?

  Hatujalalamika, bali tunapinga, matumizi ya nguvu kupita kiasi yanayofanywa na vyombo vya dola tunavyovilipia kupitia kodi zetu. Upinzani huu unalenga kutoa suluhisho la kudumu kwenye eneo la utawala bora.

  Tumesema, sio kwa kulalamika, kwamba wezi/watuhumiwa wa hujuma/wizi wa raslimali zetu, washughulikiwe haraka.Hapa tuna uwezo upi zaidi ya hapo?

  Hapo Uganda, aliyekuwa Makamu wa Rais, Mawaziri 2 na Naibu 1 wako mahakamani/rumande kwa matumizi mabaya ya madaraka, na bado mbingu hazikuanguka!! Hapa. Kwetu tuna "sacred cows".

  Kuna wanaolalamika!

  Nape Nnauye amesikika akisema kuna kundi lenye "uwezo wa kifedha" linataka kumhujumu Rais na eti linajulikana, badala ya kukamatwa Nape naye "analalamika". Kwa kufanya njama za kumhujumu Rais ni jinai. Anayehujumiwa ndiye ana mamlaka yote ya kuwashughulikia hao watu.

  Watu wanaotajwa kila mtanzania anawajua!

  Ili mradi hawajakamatwa, tutaendelea kuhoji "wanakamatwa lini?"

  Rais naye amelalamika kuhusu watendaji kutokuwa makini suala la umeme. Ana uwezo wa kuwafukuza na kuteua wengine. Naye analalama! Lol!

  Kwa kuwa njia nyingine hazituwezeshi kutoa mawazo ya suluhisho la matatizo yetu, jukwaani ni "alternative forum". Hata wawakilishi wetu (wabunge)walipoona Serikali haiwasikilizi(kwa niaba yetu) wakaanzisha "Back Bench Revolt!!"

  Hili la kusema "eti tunalalamika tu bila kutoa suluhisho" ni kauli tu yenye ghiliba ndani yake.

  Serikali kukataa kusikiliza baadhi ya yanayowekwa humu (ukiacha vitu kama "taarifa za uchunguzi binafsi") inaandaa "recipe" ya kusambaratika kwa Taifa. Hapo hakuna atakayepona. Tusifikishane huko!

  Sisi tutarudia kusema tena na tena.

  Wachina wana msemo wao unaosema:

  "Tone la mvua linapasua mwamba sio kwa sababu lina nguvu, lakini kwa sababu ya kudondoka mahali palepale kwa kurudia"

  Chonde, nchi yetu ni bora kuliko vyama na makundi ya kisiasa!

  Mungu aiwezeshe serikali kusikia!

  MJL
  Sent from my BlackBerry® smartphone provided by Airtel Tanzania.
   
 2. Mzee

  Mzee JF-Expert Member

  #2
  Oct 15, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 12,970
  Likes Received: 2,965
  Trophy Points: 280
   
Loading...