jerryempire
JF-Expert Member
- Jan 4, 2017
- 5,883
- 10,221
Habari wana jamvi,
Kwa sie wakazi wa kitunda tumekuwa tuna adha kubwa ya kukabwa hasa nyakati za usiku kutoka kwa vijana wadogo wenye silaha kama mapanga na visu,yani ikifika saa 4 tu ukiwa road unatembea kwa mashaka.
Tukio ambalo nililishuhudia kwa macho,
Ilikuwa mida kama ya saa 11 alfajiri kuna mama mtu mzima tu alikuwa anakwenda kivukoni kutafuta samaki wabichi,dah ile anachomoza tu mtaani vijana kama 20 wakamzunguka mmoja akamtoa ziwa then akawekea panga kwenye ziwa kama anabhela atoe au akate ziwa mama wa watoto bila hiyana alitaka kuwavulia mpaka chupi waondoke nayo then hao wakaondoka zao.
VIPI MJEDA KUPIGWA
Jioni mzee wa kazi(mjeda)katoka zake kazini mida ya saa 5 alikuwa hajavaa nguo za kazi bali amevaa kiraia huku anaongea zake na simu ghafla jamaa hawa wakamvamia,sasa kwenye kupigana nao wakamjeruhi kidogo,sasa ile siku ikapita siku ya pili jamaa wakatinga mtaani wakawachota ote waliohusika.
Na sasa naona bado operation inaendelea kwani wengine wanafatwa hadi makwao saa 7 hata 10 wakiwa wamelala na kuchukuliwa hope mnafahamu wajeda huwa wanawachukua vipi.na cha kushangaza ile habari ya kwamba unakamatwa then baada ya siku unarudi mtaani hakuna kila aliyedakwa ni mvua ya mwaka,miaka na miezi jela
USHAURI WANGU KWA SERIKALI
Tunaiomba serikali isisubiri mpka afanyiwe kitu cha hatari/uhalifu askari wao ndo wachukue hatua kwani raia wengi walikuwa wanaumia hali ya kuwa taarifa zinapelekwa polisi pasipo kufanyiwa kazi watu walikuwa wanalala saa 4 kama watoto wakihofia usalama wao
USHAURI KWA WAZAZI
Wakati hao vijana wanakamatwa wazazi wao walikuwa wanashtushwa na kushangaa baada ya kuambiwa vijana wao ni wahalifu,huku wakiuliziwa kwa majina ya ajapo kama panya,spider,rambo na mengine ya ajabu ambayo siyo waliyopewa na wazazi wao,ushauri wangu kwa kina mama na wengine ni lazima tutambue kijana wako anapokuwa chini ya himaya yako lazima ujue anafanya nini na kumsimamia kwa kila hatua usimpe huru kujichanganya na makundi ambayo yanaweza kumuharibu future yake na hata maisha kwa ujumla.
Nawasilisha
Jerrybanks