Tunakwenda au tunarudi? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunakwenda au tunarudi?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by JENSENE, Jul 11, 2011.

 1. J

  JENSENE Member

  #1
  Jul 11, 2011
  Joined: Mar 7, 2011
  Messages: 52
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hivi karibuni tumeshuhudia mijadala mbalimbali ya bageti ikiendelea bungeni. kitu cha kushangaza wabunge wengi wameonekana wakiwasahau wapiga kura wao na kujita ktk kutetea maslahi yao. Wabunge wengi wa sisi emu wamekuwa wakitumia wingi wao/nguvu kupinga hoja muhim zenye manufaa kwa taifa na wananchi wa hali ya chini. Hii inaonesha ni jinsi gani watu tuliowachagua si kwa ajili yetu. Katika hali wazi kabisa tazama akina Mnyika, Tundu Lisu,Zitto wanavyopambana. Watz tuamke tupambanue hoja na si ushabiki tu tuangalie maisha yetu tunapelekwa wapi.
   
 2. Mufiyakicheko

  Mufiyakicheko JF-Expert Member

  #2
  Jul 11, 2011
  Joined: Mar 24, 2011
  Messages: 893
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  bado hawajanawa uso
   
 3. F

  FUSO JF-Expert Member

  #3
  Jul 11, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,867
  Likes Received: 2,340
  Trophy Points: 280
  nchi haina mwenyewe, hata wewe kama una uwezo wa kuila usifanye ajizi - ikifikia point mwakilishi wa watu bungeni anatetea posho yake ya kukalia kiti bungeni wakati wapiga kura wake wanakufa hawana hata matibabu - think twice.
   
 4. Komeo

  Komeo JF-Expert Member

  #4
  Jul 11, 2011
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 2,396
  Likes Received: 423
  Trophy Points: 180
  Wakati wa uchaguzi tuliwatahadharisha wananchi hatari ya kuwachagua wana ccm ambao wanawagawia pesa huko majimboni, kuwa kamwe hawataenda bungeni kuwatetea kwavile wametumia pesa zao kununua kura kutoka kwenu. Kwa maneno rahisi ya kibiashara ni kwamba "mlishamalizana" kwa kuwauzia kura zenu ambazo mliziona thamani yake ni doti 1 ya khanga na kapero. Wananchi hawana tena haki ya kuwalalamikia watu ambao walishamalizana nao, kwani walishafanya kosa ambalo kwalo wanapata maumivu, hadi jamaa warudishe fedha zao na faida juu. Hiyo ndo kanuni ya biashara. Maumivu yakizidi subiri sanduku jingine la kura 2015, pengine akili za wapiga kura wengi zitajua kosa walilolifanya kipindi hiki. Sipendi kabisa kusikia wananchi wakilalamikia jambo ambalo lilikuwa ndani ya uwezo wao!
   
 5. F

  FUSO JF-Expert Member

  #5
  Jul 11, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 11,867
  Likes Received: 2,340
  Trophy Points: 280
  elimu ya uraia ndiyo tatizo kuu, sipendi sana kuwatupia lawama wapiga kura kwa asilimia mia. Hili la elimu ya uraia, ufukara na umaskini uliokithiri wa baadhi ya koo vijijini ndiyo mtaji mku wa CCM.

  Lazima tusaidiane kufikisha elimu hii vijijini, vinginevyo yatakuwa haya haya ifikapo 2015.
   
Loading...