Tunakumbushana tu wala sina jipya sana!

Tunakumbushana tu wala sina jipya sana!

Manyanza

Platinum Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
20,255
Reaction score
48,111
Denis Mpagaze

Moja

Wema na ubaya vyote ni mbegu. Ukivipanda vinaota na mvunaji ni wewe uliyevipanda! Tunakumbushana tu ukipanda bangi huwezi kuvuna mahindi!

Mbili

Kutumia nguvu nyingi bila akili ni mateso kwa mwili na faida kwa wenye akili. Tunakumbushana tu kuwekeza katika akili maana nguvu zina ukomo, akili haina ukomo!

Tatu

Unapozinguana na mpenzi wako usimshitaki kwa ndugu zako maana siku utakapomsamehe ndugu zako hawatamsamehe! Tunakumbushana tu kwamba kama ukiona mahusiano yenu hayasongi, songa wewe!

Nne

Kupanga matumizi kwa pesa za watu ni utapeli. Tunakumbushana tu kwamba ukila vya watu usilalamike na vyako vikiliwa maana lazima viliwe tu!

Tano

Utajiri hauji kwa uchoyo, utajiri unakuja kwa utoaji ndiyo maana watoaji wanaendelea kutajirika na wachoyo vyuma vinaendelea kuwakazia! Tunakumbushana tu kwamba asiyepoteza haokoti.

Sita

Kama hauna pesa ukiona mtu kanunua kigari cha watoto wake utasema ni matumizi mabaya ya pesa bora angenunua chakula. Tunakumbushana tu kutafuta pesa ili tuache kuumia kwa matumizi ya watu!

Saba

Mungu ni wa kila kitu, siyo magumu tu. Tunakumbushana kumkumbuka Mungu wakati wa magumu tu, magumu yatakuwa sehemu ya maisha yako maana akiyaondoa utamkimbia!

1. Malezi: Muandae Mwanao Kuwa na Hadhi
2. Biashara Huanzia Kichwani Siyo Mfukoni
3. Fikra Tunduizi: Tungo za Kufikirisha
3. Ukombozi wa Fikra
4. Wasomi Huru Gerezani
5. Maisha ni Kutafuta Siyo Kutafutana
6. Ukombizi wa Fikra za Mwafrika
7. Fungua Ubongo
8. Miamba ya Afrika
9. Viongozi Walioandika Majina yao Vibaya
10. Mbinu 16 Alizotumia Yesu Kutoboa
11. Viongozi Wanaoishi Baada ya Kufa
12. Fahamu ya Ndoa Kabla ya Ndoa!

Cheers
Mwl. Denis Mpagaze
Muhenga wa Karne ya 21!
 
Back
Top Bottom