Mleta mada, leo uminifurahisha sana....hivyo natanguliza shukrani zangu dhati kwako kwa jitiada unazozifanya ili kuikomboa jamii yako.
Pili, napenda kuunga mkono hoja, kiukweli hiki kinachoendelea sio kitu chema hata kidogo katika jamii zetu, na niwe tu mkweli, mimi ni miongoni wa waathirika wa hili sakata....anyway naomba niende moja kwa moja kwenye kuchangia mada.
Kiukweli siku hizi wanawake kwa wanaume, wamekuwa na dhana ya kulichukulia suala la mahusiano ya kimapenzi katika uzito mdogo mno, jambo ambalo sio sahihi hata kidogo. Na ndilo linalotufikisha hapa leo hii tulipo, ukijaribu kufatilia kwa makini kuhusu hili ninaloliongea, bila shaka utabaini kuwepo kwa utofauti mkubwa sana, ulipo kati yetu sisi vijana na wazee wetu, hasa wa miaka ya 50-70. Kutokana na hali hiyo kuibuka, tumejikuta kwenye mazingira ya kuchukulia poa hata hali ya mtu kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi leo na kesho. Na wengine wanaemda mbali zaidi, hata kufikia hatua ya kuamua kuifanya miili yao kuwa bidhaa, kwa lugha nyingine naweza sema WANAJIUZA.
Naomba nianze tu kwa kusema kwamba, hili jambo linaloendelea kuzitafuna jamii zetu, ni matokeo hasi ya mbegu nyingi sana. Mbegu zenyewe ni malezi, utandawazi, hali za kiuchumi, hali za kiafya, suala la elimu na suala zima la mapenzi yenyewe. Lakini mimi leo nitajikita zaidi kwenye hiyo mbegu ya mwisho niliyoitaja hapo juu (mapenzi).
Suala la mapenzi, ni suala moja nyeti sana....na ndio msingi mzima wa suala zima la mahusiano............(nitarudi baadae kidogo)