Tunakopesheka kwa kuwa tunalipa deni. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunakopesheka kwa kuwa tunalipa deni.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kiby, Jun 20, 2012.

 1. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #1
  Jun 20, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,192
  Likes Received: 997
  Trophy Points: 280
  Wana jamvi kuna jambo linatatiza sana kichwa changu toka bajeti hii ya serikali isomwe. Kitakwimu deni la taifa linakisiwa kuwa trillion 20. Na uwezo wa pato letu la ndani ni wastani wa trillion 8 kwa mwaka huu. Hapa sasa ndipo shida yangu ilipo, ambapo naomba wasomi na wajasiriamali wote waliofanikiwa katika biashara zao bila hata ulazima wa elimu ya shule. Tutawezaje kulilipa deni letu kufikia zero huku matumizi ya kawaida yakizingatiwa achilia mbali miradi ya maendeleo? Hatujauzwa kweli? Hebu tueleweshane kwa kujaribu kuweka mbali itikadi za vyama vyetu zinazotupofusha katika masuala ya msingi yanayotuhusu. Nawakilisha.
  .
   
 2. S.Liondo

  S.Liondo JF-Expert Member

  #2
  Jun 20, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 2,143
  Likes Received: 660
  Trophy Points: 280
  Hapo hakuna kulipa, labda kupunguza kidogo tu na kisha kusubiri awamu nyingine ya msamaha wa madeni kutoka kwa wahisani. Sisi ni watumwa kwasababu ya madeni tuliyonayo. Inashangaza sana kuona mbunge wa CCM mwenye akili timamu akidai kwamba hakuna kukopa kwetu hakujafikia kiwango kibaya. Kama ni hivyo basi serikali ilipe deni lote tuone kama haijaanguka.
   
 3. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #3
  Jun 20, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Huo ndiyo uchizi wa wabunge wa magamba
   
 4. nahavache

  nahavache JF-Expert Member

  #4
  Jun 20, 2012
  Joined: Apr 3, 2009
  Messages: 869
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kudaiwa sio tatizo, tatizo ni kuwa hizo ulizokopa umepeleka wapi? Sisi tatizo ni kuwa tumepeleka kwenye matumbo ya wajanja wachache
   
 5. CHEMPO

  CHEMPO JF-Expert Member

  #5
  Jun 20, 2012
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kama unalipa kwa nn deni liongezeke..kuongoza nchi inataka watu waliotulia akili wanaojua wanafanya nn tofauti ya hapo lazima ukope hata kwa ajili ya mishahara
  ,,mimi naipenda hii hali iendelee ili ukombozi wetu usichukue muda mrefu
   
 6. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #6
  Jun 20, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,985
  Likes Received: 441
  Trophy Points: 180
  Deni la taifa mpaka mimba inadaiwa sh. Laki nne na themanini elfu.
   
 7. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #7
  Jun 20, 2012
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,192
  Likes Received: 997
  Trophy Points: 280
  .
  Nini sasa kifanyike ili kushinikiza pesa zinazokopwa hasa zile za mabenk ya ndani kuwekwa wazi matumizi yake? Na ni sababu ipi inayopelekea bajeti kutofika katika baazi ya zilikokusudiwa wakati deni la kuikopea hiyo bajeti likizidi? NCHI YETU INAITWA DANGANYIKA!!
  .
   
 8. Nyalotsi

  Nyalotsi JF-Expert Member

  #8
  Jun 20, 2012
  Joined: Jul 20, 2011
  Messages: 5,104
  Likes Received: 551
  Trophy Points: 280
  tungeona fly overs japo kwenye junction za dar tu tusingekuwa tunalaumu. Shida ni pale wanapokopa kujenga barabara aafu ujenzi unasimama kwa kukosa pesa! Zimeenda wapi mlizokopa? Kuna mchwa wanakula? Kila siku wanazungumzia kupunguza matumizi,mbona ndo yanaongezeka? Pesa zinakopwa kwa ajili ya ruzuku ya pembejeo lakini hazifiki mashambani na hawajui nani kala hizo pesa! Are they serious? Hilo deni wamekopa kina wasira aafu tutalipa sisi na watoto wetu,kuna uhalisia hapo? Kwa nini tusiwachukie?
   
 9. F

  FJM JF-Expert Member

  #9
  Jun 20, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 8,088
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Ili kukuonesha jinsi wabunge wa ccm wanashangilia biashara kichaa ni hivi: budget ya mwaka huu 2012/13 ni Tsh 15 trillion. Now, zaidi ya Tshs 2 trillion zimetengwa kulipa deni! CCM wanasema ni madeni ya miaka mingi i.e 50 lakini hata kama ni miaka mia nani atalipa? Ni mzazi gani anayekopa na kujigamba watoto na wajuu ndio watalipa? Tena unakopa kununulia wanzuki na posho na sio hata kuwekeza ili huyo mtoto/mjukuu apate nyenzo ya kulipa deni alilolikuta!

  Kwa kifupi mambo sio mazuri kabisa - deni la taifa linaongezeka, inflation inapaa, industrial base is very weak, population inakuwa sana, ardhi inaanza kupewa kwa wawakezaji kwa 99 yrs lease! Na kama haitoshi aprox 90% ya nyenzo kubwa za uchumi wetu kwa sasa ziko chini ya watu wa nje (madini, gas, oil, utalii). 50 yrs of independence.
   
Loading...