Shikamoo Mkuu, Juzi ktk hotuba yako nilikusikia kwamba kwa sasa hivi tunakusanya wastani wa 1.2 Trillion na hapo hapo tunalipa Deni la 900 bilion, kwa kila mwezi, binafsi niliogopa sana, na bado natafakari bila kupata majibu, naomba Kama kuna watu wako ktk hii mitandao waite tujadili namna ya kujikwamua kutoka ktk hali hii ambayo kwangu Mimi naona Kama ni hatari kubwa kwa Mustakabali wa Taifa letu pendwa Tanzania
Nijuavyo Mimi mishahara peke yake kwa mwezi ni zaidi ya 520 bilion, na ktk hotuba yako Ina maana kila tukitoa Deni tunabaki na 300bilion ambayo hata mishahara haitoshi kulipa, na hapo hapo bado wanafunzi hawajapewa posho zao Kama tulivyoahidi, bado hospitali bajeti ya dawa na vifaa tiba sijaona bado miradi ya Maendeleo na mambo mengine Chungu nzima sioni hata shilingi ya kufanya hayo yote,
Mkuu, hapo hapo kuna hatari inakuja mbele yetu ya Njaa, tangu mwezi Julai 2016 mpaka sasa mwezi wa pili ktk mikoa mingi hakujanyesha tone la Mvua, that means, Kama bahati mbaya ikifika mpaka tarehe 22 ya February bila Mvua kunyesha lazima kutakuwepo na baa la njaa kubwa halijawahi kutokea.
Ushauri wangu, kwanini hao wanaotudai usiwapigie simu ukawaita ukaongea nao ukweli kwamba kuna hatari inatunyemelea, kwa hiyo watuvumilie Kama miezi mitatu hivi kwanza ili turekebishe mambo yetu kwanza?
Sasa hivi kilo moja ya unga ni 1,800 haijawahi kutokea, ni thahiri kwamba kwa kipindi kifupi kijacho kuna familia nyingi zitashindwa kumudu kununua hata kilo moja ya unga, achilia mbali mboga. So, what do we expect? Ni bora kuponya kuliko kutibu. Mitaani hali ni mbaya, biashara ziko Chini kabisa haijawahi kutokea. Tujadili tu kistaarabu kwa manufaa yetu na kwa watu wetu. Je? Mh Presdent. Kuna mbinu mbadala uliyo nayo ya kutuvusha salama ktk kipindi hiki kigumu, na Kama Huna, pia ni vizuri ukaweka wazi ili tukushauri Vizuri.