Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,050
- 144,456
Kwa walio katika taaluma ya ualimu wanaweza kunielewa ila kama sio mwalimu basi hutanielewa. Mimi sio mwalimu ila nimepita huko.
Kizazi cha sasa, malezi ya watoto wa siku hizi na kubadilika kwa life style yetu ni mambo yanayofanya kazi ya ualimu kuwa ngumu sana na alierudisha viboko mashuleni aliona mbali ila tuendako walimu wanaweza kuacha kabisa kuadhibu wanafunzi japo viboko vimeruhusiwa.
Watoto wa siku hizi wanalelewa tofauti na sana na zamani na wakienda mashuleni wanakuwa hivyo hivyo na mwalimu usieweza ku-control hasira zako utaishia jela kama sio kufukuzwa.
Utatumia mbinu zote za ualimu ila bado unaweza tu usifanikiwe ku-handle watoto wa siku hizi kwa mafanikio na hii ni moja ya sababu ya kushuka kwa kiwango cha elimu.
Baada ya kupitia baadhi ya comments, nimegungua kuna watu hawajanielewa ila naomba niweke ufafanuzi ufuatao juu ya hili tukio kulingana na mtazamo wangu.
Kwanza nianze kwa kusema binafsi siungi mkono tukio hili ila najaribu kuwa objective kulingana na hulka ya sisi binadamu(mimi na wewe).
Ukiangali ile clip ni wazi wale walimu walipandwa na hasira kupita kiasi na bila shaka si hivi hivi tu bali kuna sababu ingawa hakuna sababu inayohalalisha walichokifanya ila kwa nature ya sisi binadamu bado tu tunaweza kujikuta unafanya kitendo kama hicho bila kutarajia kutokana na hasira tu.
Kwa mfano,mtu anaweza kumchoma mtu kisu katika ugomvi kutokana na hasira na mtuhumiwa kufikishwa mahakamani lakini mwisho wa siku kwa mshangao wa wengi mtuhumiwa anaweza kupatikana na hatia ya kuua bila kukusudia na wala si kuua kwa kukusudia kutokana na mazingira ya tukio lenyewe.
Unaweza usiwe na nia ya kuua lakini mtu akakutibua na kutokana na hasira ukachukua kitu kama nondo au jiwe na kumpiga nacho na bahati mtu huyo akapoteza maisha na mahakamani ukahukumiwa kwa kosa la kuua bila kukusudia na sio kuua kwa kukusudia.
Kwa kesi hii ya walimu hawa,bado tunahitaji kusikia kutoka upande wa pili ni nini hasa kilitokea na kuwafanya kufikia hatua ile ya kushangaza.Si ajabu tukisikia nini kilitokea baadhi mnaweza kujikuta mnabaki katikati.
Ni kweli taaluma na maadili ya ualimu hayaruhusu kabisa walimu kufanya walichokifanya ila niwaulize jambo moja.
Hivi mtu unapomfumania mkeo au mumeo au ukahisi anaku-cheat,kuna sheria inayokuruhusu kumpiga mpaka kumjeruhi,kumpa kilema na wakati mwingine hata kumuua?
Hamjawahi sikia mtu anachinja mkewe kwasababh ya wivu tu?
Ukishakuwa na hasira na ukashindwa kuzi-control akili inakuwa sio yako tena na hutakumbuka kuna maadili ya ualimu wala sheria za nchi bali utafanya kile akili yako inachokutuma kufanya kwa wakati huo ila mwisho wa siku wengi huishia kujuta na wengine hata kujiua.
Hivi mnafikiri haya matukio yameanza leo?Haya matukio yapo tu siku zote ila hapa teknolojia ndio imetufumbua macho na bila teknolojia hii tukio pengine lingepita kama yanavyopita mengine.
Tuwe objective na tusisahau hasira ni hasara