Tunakemea udini, tunatenda udini!

Tunakemea udini, tunatenda udini!

Jacobus

JF-Expert Member
Joined
Mar 29, 2011
Posts
4,711
Reaction score
1,738
Watanzania tumekuwa wepesi mno kukemea jambo ambalo ukweli tunalitenda. Wakati wa awamu ya kwanza ya viongozi wetu (Nyerere na Karume) maneno yalikuwa machache ila vitendo vingi na hasahasa suala hili la udini. Wakati ule shuleni huwezi mkuta mwanafunzi kavaa alama ya imani yake ya dini (wakristu-misalaba na rosari, waislam- mavazi kama kanzu nyeupe, baragashia, buibui na hijabu). Upande wa Zanzibar ilikuwa mwanafunzi wa kike anakuja na buibui lake ila ni marufuku kuvaa akiwa maeneo ya shule, siku hizi tena shule za serikali wanafunzi wa kike wanaruhusiwa kuvaa hijabu! Hata wabunge na mawaziri wetu (baadhi) tena wawapo kazini wanavaa alama hizo za imani zao za dini halafu WANAKEMEA udini. Juzijuzi tu mwanaJF mwenzetu, Yahya Mohamed, alitushangaza kweli alipoamua kuvaa kanzu nyeupe na koti na kuendesha kipindi Startv sasa tuliokuwa tunaangalia hicho kipindi (tena hakihusiki na mada ya dini) tukajiuliza kama watangazaji wanafanya hivo hizi kauli za kukemea udini zitokazo kwa viongozi wa dini na watawala wetu si kiini macho tu nchi hii?
 
Back
Top Bottom