Magoiga SN
Member
- Oct 15, 2016
- 15
- 61
Magoiga SN-Mwanza
Mara kadhaa vijana wengi Tanzania (nami nikiwemo) tumekuwa tukijadili masuala mbalimbali ya kijamii, kiuchumi, kisiasa na kielimu kuhusiana na taifa letu huku tukitafuta 'weak point' ya kuisifia itikadi ya Chama chako cha kisiasa, au hata kutafuta namna ya kukidhihaki chama kingine cha siasa. Majibu mengi yanayotolewa huwa yanalenga kukuza itikadi ya chama chake na kudidimiza itikadi ya chama kingine.
Katika majibu yao wanataka watu waamini kuwa njia pakee ya tatizo hilo kumalizika ni lazima chama flani cha siasa kife au kiondoke madarakani na chama chake kiingie madarakani, kitu ambacho siyo kweli. Haijawahi kutokea kuwa jawabu la tatizo flani ni kwasababu wewe hujawa kiongozi.
Maana Tunaposhauri serikali, tunataka serikali ifanikiwe ktk kuliletea taifa maendeleo. Sasa ikiwa tunawaza kuwa taifa likipata maendeleo chini ya chama flani cha siasa basi chama kilichotoa ushauri hakitapata fursa ya kuingia IKULU hapo ndipo huwa tunalipoteza taifa bila kujua.
Kuna watu wanataka mambo mazuri yafanywe na chama chao pekee, na ikitokea chama kingine kinafanya vyema basi hilo linakuwa ni kosa na wanatafuta namna ya kudhihaki na hata kukwamisha kwa uchonganishi kwa umma.
Kiufupi vijana wengi hudhani kuwa suluhu ya tatizo flani linaloikumba nchi ni kwasababu ya chama flani cha siasa. Wanasahau kuwa, tunapojadili mambo kwa maslahi ya Taifa huwa hakuna nafasi ya vyama vya siasa ktk mijadala hiyo. Tunapojadili namna ya kupambana na ujangilii au ufisadi, tunapaswa kutafuta majibu na mbinu ambazo serikali inaweza kuzitumia ktk kupambana na tatizo husika.
Kwasasa hali ni mbaya sana, imefikia hatua likitokea tatizo kuna baadhi ya wafuasi na hata viongozi wa vya vya siasa wanaofurahia matatizo maana yanawasaidia ktk kusema kuwa serikali ya chama flani imeshindwa ktk suala flani.
Imefikia hatua hata wapinzani wakitoa yshauri bungeni, unaweza kutupiliwa mbali na hata kuonekana hauna maana kisa umetolewa na upinzani, mana imezoeleka kuwa wapinzani siku zote huwa wanataka serikalini ishindwe. Kwa hiyo hata wakitoa ushauri mzuri serikali inauona kama mtego ilihali ni ushauri
Tunaposhauri kwa manufaa na maslahi ya taifa, hatufanyi hivyo ili kujiimalisha kama chama bali tunafanya hivyo ili kujiimalisha kama taifa ili kuyafikia malengo ya pamoja kama taifa kwa mujibu wa mpango wa maendeleo wa nchi.