Tunajipanga - Pinda

Crucifix

JF-Expert Member
Feb 20, 2011
1,651
588
Wangefuta tu hii session ya papo kwa papo, haina tija japo nimeangalia kwa siku moja tu.

Leo nilikuwa sina kazi na kwa mara ya kwanza nikatazama TBC kutoka bungeni, kipindi cha maswali na majibu ya papo kwa papo. karibu kila swali lililoulizwa; spika Makinda alikuwa anatanguliza kwanza, "ah! hili liko specific sana, WM hataweza kulijibu lakini sijui WM labda unaweza, teh teh teh," na kisha waziri mkuu anatoa maelezo na sio majibu. Na kila muuliza swali ambaye hakuridhika na majibu hayo ya WM na kuuliza la nyongeza, jibu la Pinda kwa maswali karibu yote lilikuwa ni....
.........................
........................
........................
"TUNAJIPANGA"

Kwa mtazamo wangu kama wanajipanga kwa kila kitu, basi hiyo foleni itakuwa ndefu sana!
 
Gombea Uwaziri Mkuu utashinda. Mpaka sasa Jk ana majina matatu anahitaji matano column itimie wahi peleka la kwako lango la Ikulu asubuhi.
 
Kila siku wao ni KUJIPANGA tu sijui UTEKELEZAJI utaanza lini? kwa mipango tu iko mingi sana
 
uwezo wake wa kufkiri kwa sasa unatia shaka,baada ya kushndwa ktatua mgomo wa madaktar na posho zao,bnafs cna iman naye tena,awam hii ndo imekula kwetu
 
Gombea Uwaziri Mkuu utashinda. Mpaka sasa Jk ana majina matatu anahitaji matano column itimie wahi peleka la kwako lango la Ikulu asubuhi.

Kwani cheo cha uwaziri mkuu kinagombaniwa??au upo usingizini!!!!?
 
Wanajipanga kuanzia Mkuu wa kaya hadi Mwenyekiti wa serikali ya mtaa...waondoke tu
 
Wangefuta tu hii session ya papo kwa papo, haina tija japo nimeangalia kwa siku moja tu.

Leo nilikuwa sina kazi na kwa mara ya kwanza nikatazama TBC kutoka bungeni, kipindi cha maswali na majibu ya papo kwa papo. karibu kila swali lililoulizwa; spika Makinda alikuwa anatanguliza kwanza, "ah! hili liko specific sana, WM hataweza kulijibu lakini sijui WM labda unaweza, teh teh teh," na kisha waziri mkuu anatoa maelezo na sio majibu. Na kila muuliza swali asiyeridhika na majibu hayo ya WM na kuuliza la nyongeza, jibu la Pinda kwa maswali karibu yote ni....
.........................
........................
........................
"TUNAJIPANGA"

Kwa mtazamo wangu kama wanajipanga kwa kila kitu, basi hiyo foleni itakuwa ndefu sana!

Nashukuru umesema kuwa ulikuwa hauna kazi ndiyo ukaangalia hicho kipindi!!nami uwa nakutana nacho kwa bahati mbaya mfano nipo hotelini nikajua hakina maana hata kidogo na majibu mengine uliyosahau ni kuwa 'mimi nafikiri' huku bibi kiroboto anamkingia kifua kama bwanake vile,ni kichefuchefu.
 
Gombea Uwaziri Mkuu utashinda. Mpaka sasa Jk ana majina matatu anahitaji matano column itimie wahi peleka la kwako lango la Ikulu asubuhi.

Ndugu si lazima kila hoja uchangie. Si kama unafahamu, lakini binadamu huwa anatambulika uwezo wake wa akili kupitia mambo anayoyafanya na anayafanyaje vilevile maneno yake.
You are genuinely ridiculous, childish and outright immature, try a little harder to smarten up.
 
Gombea Uwaziri Mkuu utashinda. Mpaka sasa Jk ana majina matatu anahitaji matano column itimie wahi peleka la kwako lango la Ikulu asubuhi.

Nani kakuambia uwaziri mkuu unagombewa au unapeleka jina iki uteuliwa?kweli JF imeingiliwa,hadi watu wa vijiwe vwa gahawa nao wajifanya wapo gud upstairs sasa
 
Hayo ndiyo majibu ya viongozi wasiowajibika wa nchi hii. TUNAJIPANGA......... TUKO KWENYE MCHAKATO...........
 
Mtoto wa mkulima naye ameshajiingiza kwenye
kundi la hao walioshindikana, akiongea mara
aingize sentensi za kizungu au atoe majibu ya
mkato, ili mradi naye kachoka.
 
Mtoto wa mkulima naye ameshajiingiza kwenye
kundi la hao walioshindikana, akiongea mara
aingize sentensi za kizungu au atoe majibu ya
mkato, ili mradi naye kachoka.

alipoteuliwa badala ya Lowassa alidhani atamtumikia malaika.....sasa kajikuta anamtumikia shetani na hawezi kukiuka kiapo chake kwa ibilisi JK. Akijibu swali anachezea kipete chake nahisi ni juju kutoka kwao "kasumba-wanga" jobtruetrue
 
Siasa ni kujipanga na kujipanga ni siasa wapi tatizo?

mungu wangu! Mods si munaona wenyewe! Halafu mtu kama huyu eti naye tunamwita great thinker! Aaaaah! Kama ndo hivyo mi naomba msinijumuishe kwenye kundi la great thinker kama vigezo vyenyewe vya u-great thinker ndo kama vya huyu jamaa.
 
Back
Top Bottom