Tunajenga nyumba

Tunajenga nyumba

Kiongozi hili timbwili kubwa......lina historia ndefu....

Kaa pembeni tufaidi mambo...kuna watu wanapewa ujumbe hapo....usinunue kesi....

Tusubiri next episode
...

sijui hiyo next episode itatoka lini!!!!!!
 
Kumbe huyo Bwana kakukuta na watoto wako tena umeshajenga nyumba zako! safi sana, waambie kabisa hao wazabizabina wasikusumbue, huhitaji urithi wake wala huna sababu ya kumuua eti kisa mali. We endelea kuponda utamu kwa raha zako, wasikuzingue bwana, hongera kwa kupata mwanamume!

Watoto ni wa kwake. Tulipoanzana alinikuta nilishajenga nyumba zangu mbili. Ndo mwaka huu akaamua awajengee wanae.
 
haya..kwa wale wageni naomba niwatambulishe kwenu mudada anaitwa Da Sophy. tupo naye hapa tokea akiwa mjamzito mpaka sasa ivi mnavoona nyumba inajengwa. kina Zahra White wamekuja juzi tu. Umesikia amu and co?
 
Last edited by a moderator:
Jamani Tanesco wanazingua nyie acheni tu. Baba J naye na mausomi yake hataki vishoka. Leo tena atashinda huko.
 
Akili ya kusoma na ya mtaani kweli tofauti sana. Simwelewi anawakataa vishoka kwa ubaya upi. Kutwa nzima ijumaa kazungushwa ofisini kwa mainjinia huko kaambulia patupu. Leo tena yuko nao. Mi mbona hawa vishoka walinisaidia sana nikafanikiwa haraka tu, hadi leo mambo safi sijaona ubaya.
 
haya..kwa wale wageni naomba niwatambulishe kwenu mudada anaitwa Da Sophy. tupo naye hapa tokea akiwa mjamzito mpaka sasa ivi mnavoona nyumba inajengwa. kina Zahra White wamekuja juzi tu. Umesikia amu and co?
 
Last edited by a moderator:
Anawajengea wanae, msianze kuninanga mkaniharibia swaum yangu bure. Mi ninazo nyumba zangu nimejenga tangu kabla hatujafikishana hapa, moja naishi na wanangu nyingine ninapangisha. Hii nnayosema kaamua mwenyewe kuwajengea wanae kasema ipangishwe hiyo pesa isomeshe wanae. Na sijatia hata senti yangu, hapa namsubiri ofisini kwake kaenda Tanesco kufatilizia barua ya umeme. Huyu ndo mwanaume bwana.

Una mambo wewe........!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Wenye elimu za darasani hebu nisaidieni. Kwani hawa vishoka wa tanesco ubaya wao nini, mbona mimi walinifanikishia vizuri tu? Mwenzangu hawataki anang'ang'ania utaratibu wa mezani kwa mainjinia, hadi sasa ni mwezi umeisha hakuna la maana. Nimemwambia aniachie hilo nihangaike nalo nalijua vizuri kimtaani, hataki anataka ya kisomi! Nami kwa kumheshimu nimemwachia afanye anavyopenda lakini wala sijafurahi kwa kweli yani mambo ya ofisini huko ni mizenguo tu.
 
Watoto ni wa kwake. Tulipoanzana alinikuta nilishajenga nyumba zangu mbili. Ndo mwaka huu akaamua awajengee wanae.

Anhaaaaaaa kumbeeeeeeeeee! nshaelewa, endelea na mipango yako kwa raha zako mwaya!
 
Da Sophy badilisha kichwa cha habari, Umeandika "TUNAJENGA" inamaanisha mnashirikiana, kwamba na wewe unachangia pesa lakini kama la Ungeandika "ANAWAJENGEA". Asante kwa kutujulisha, tutamplekea ujumbe huu mkewe, ili afahamu kwamba mumewe anawajengea watoto wake nyumba.
 
Tunajenga ndio. Wewe unafikiri kajiamualia tu kujenga nyumba. Kuna mchango wangu wa jinsi nilivyomfurahisha hadi achukue uamuzi na kutoa fedha zake na kusimamia kazi yote. Kwani wangapi wamezalishwa watoto wanaishia kwenda kugombea urithi na watoto wa mama mwingine. Mwanaume mwenye busara huyu katumia akili ambayo wengi hamna. Kule kuna mwanamke mwenye digirii na hela nyingi za warsha na makongamano, hashindwi kuwajengea wanae hata akitaka kila mmoja na jumba lake. Tatizo hela zake anamalizia kwenye vipodozi feki, minywele bandia na dawa za kujikondesha. Mie huku najitegemea biashara zangu mwenyewe kuna kupanda na kushuka. Mwanaume akaona hawa hapa ndio wanastahili awajengee nyumba wale kule wasubiri urithi. Busara ya mwanaume inaonekana kwenye matendo yake. Ameonesha anajali.
 
Na mbona nilivowauliza kuhusu tanesco mnanichunia, au nyie mnapenda vya umbea tu vya maendeleo hamtaki
 
Wanaume wamejiumbia..... matesooo....kujihangaishaaaa.......(hapo ukute na mkewe anajengea watoto......)
 
Anawajengea wanae, msianze kuninanga mkaniharibia swaum yangu bure. Mi ninazo nyumba zangu nimejenga tangu kabla hatujafikishana hapa, moja naishi na wanangu nyingine ninapangisha. Hii nnayosema kaamua mwenyewe kuwajengea wanae kasema ipangishwe hiyo pesa isomeshe wanae. Na sijatia hata senti yangu, hapa namsubiri ofisini kwake kaenda Tanesco kufatilizia barua ya umeme. Huyu ndo mwanaume bwana.

Hata akikupa uhai wake, ni Mume wa mwenzio. Bora ametambua watoto wakuokota mtaani ni wasumbufu kama mama zao walivyo,awajengee tu ili wasijekuwa kero na usumbufu kwa watoto wa mwanamke mwenzio. Ujishededue lakini ni Mume wa mtu, angekuwa wako hata usingehangaika JF kuutangazia umma. Amani ya Moyo siyo nyumba wala mali wala Mume wa mtu labda kwa --------. Mungu akuhurumie akufungue katika hicho kifungo, maana unatapatata na hujitambui. Pole sana.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom