AUGUSTINO CHIWINGA
JF-Expert Member
- Apr 23, 2017
- 222
- 695
TUNAIONA MILIONI 50 KWA KILA KIJIJI/MTAA?
Na;
Augustino Chiwinga
(Sauti ya Korosho)
Mzazi anaweza fikiria kuwapa pesa watoto wake kila mmoja akaamue anachofanya, lakini mzazi anaweza pia akabadili uamuzi na kufanya kitu au jambo jingine lenye tija kwa watoto pengine hata na wajukuu.
Kata zina Vijiji/mitaa mingi ya wastani wa Minne hivyo basi endapo tungepewa M50 kila mtaa ingekua Milioni 200.Lakini kilichofanywa katika kata zetu vijiji/mitaa yetu kina thamani ya zaidi ya M200.
Wapo waliopata barabara za lami na zimefungwa taa, tumejengewa na kuboreshewa vituo vya Afya, Hospitali, Zahanati, masoko, elimu bure, stendi wapo wanufaika wa mikopo itolewayo na halmashauri %4/%4/%2.
Tumeboreshewa shule zetu kongwe na sasa mandhari yake yanaipendezesha Kata vijiji/mitaa yetu na inawavutia watoto kusoma hapo bado sijagusia maji na umeme.
Tuna kila sababu yakusema Ahsante Rais Magufuli, ahsante serikali awamu ya tano na asante Chama tawala.
0624070026
Lindi.