Mapambano Yetu
JF-Expert Member
- Aug 14, 2012
- 1,124
- 2,092
Kwanza nitoe pole kwa Mbunge wa Arusha Ndg Godbles Lema, wana - Arusha na Serikali kwa tukio la kuondokewa na wanafunzi, walimu na Dreva kwenye ajali ya gari. Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.
Nirejee kwenye lengo la thread hii, Serikali imetoa orodha ya wafanyakazi wa umma ambao vyeti vyao vya kitaaluma ama ni Feki, vinatumika sehemu tofauti (vyenye utata) au hawakuwakilisha baadhi ya vyeti kwaajili ya uhakiki.
Katika taarifa iliyotolewa na Serikali haikuelezwa kama wazi kama upungufu huo ni kizuio kwenye sekta za umma tu au na za binafsi.
Tuchukulie mfano wale walioko sekta za Afya (madaktari & manesi) wengine walifikia hatua kubwa kiutaalamu kama madaktari bingwa. Sasa hawa watu wakiondoka serikalini na kuelekea sekta binafsi watambuliwe au ndo safari yao imeishia hapo?
Hapa Kuna utata, kama jibu ni wasitambuliwe, Je, Serikali inampango gani dhidi ya kuhakiki vyeti vya wafanyakazi kwenye sekta binafsi?
Kama jibu ni wanaruhusiwa kwenye sekta binafsi basi itakuwa ni kihoja cha mwaka.
Kutokana na utata huu, tunaiomba Serikali itoe ufafanuzi ili ijulikane wazi kama hawa binadamu wanafukuzwa Kazi na utumishi au wamepoteza Kazi tu lakini in other way wanaweza kutumika kwenye sekta binafsi. Pia ieleweke kama uhakiki utafanyika kwenye sekta binafsi na hatua stahiki.