Tunahitaji Viongozi na Wananchi waadilifu watakaomsaidia Rais Magufuli Kutimiza ndoto alizo nazo kwa Tanzania Regardless ni Wapinzani/ Chama Tawala

MARKYAO

JF-Expert Member
Mar 30, 2012
673
682
Nimewiwa kupost ujumbe huu maana nilivutiwa sana na baadhi ya mambo aliyoyaongelea Rais siku anakutana na Wafanyabiashara Ikulu juzi na miongoni ya mambo ni kuwaruhusu wafanyabiashara kufunguka na kuonesha uhalisia w hali ilivyo mbali na kudanganywa wa watendaji wake hapo nyuma.

Zaidi ya yote ni action kuhusu bandari ya bagamoyo ambayo ilikuwa Kitanzi kwa taifa na maono ya kuimarisha Uchumi wetu. Hongera sana Raisi kwa hilo.

Watendaji wako ndio vichaa maana ndio walikuwa wanashinikiza kuendelea na Bandari hiyo hata bungeni wakasema serikali ij na majibu.

Majibu sawia uliyatoa na naamini ulikuwa miogoni mwa baraza la mawaziri liliokaa kabla hujawa raisi na ulijua fika tulivyokuwa tunaenda kuumizwa na wachina.

Wachina ni Maadui wa Uchumi kwa nchi zinazoendelea na wanatumia kila aina ya tricky kudanganya hasa wanapokutana na viongozi wasio na maono. Werevu watakuelewa kupitia video hii..
 
Attachments

  • China Mission to Afrika.mp4
    5.4 MB
Huwezi kubadilisha mindset za watu overnigh, huyu bwana anakurupuka akidhani atayaweza kufanya yote kwa kutumia akili zake pekee bila kushirikisha bongo za watu wengine, he will never, he will fail.nahofu anaeeza akajinyonga asipotimiza malengo yake.
 
Hivi hizo ndoto zake siku akiwa hayupo Nani atazisimamia
 
"Wachina ni Maadui wa Uchumi kwa nchi zinazoendelea na wanatumia kila aina ya tricky kudanganya hasa wanapokutana na viongozi wasio na maono."!!

Sina hakika kuwa wachina ni maadui wa nchi zinazoendelea. Na video yako ni ya mtu mwenye wivu kwa wachina. Leo wachina wanaonekana watubwa ovyo, juzi ninyi mlikuwa mnawakaribisha kwa shangwe na vigelegele, kama mmewapata WENZENU watakaowafanyia kazi za nafuu!

Nawapenda sana wachina, wamewafanya watanzania kuondokana na kutumia baiskeli, vibatari, redio za gharama, kila mtanzania ana simu, na nadhani hata bandari yetu wangetufanyia ya bei powaaaa. Those people are good. Ukimwona mwenzako anakuzidi maarifa,.kazana umfikie, acheni kulia lia na kulalamika, fanyeni kazi mlingane nao.
Nimewiwa kupost ujumbe huu maana nilivutiwa sana na baadhi ya mambo aliyoyaongelea Rais siku anakutana na Wafanyabiashara Ikulu juzi na miongoni ya mambo ni kuwaruhusu wafanyabiashara kufunguka na kuonesha uhalisia w hali ilivyo mbali na kudanganywa wa watendaji wake hapo nyuma.

Zaidi ya yote ni action kuhusu bandari ya bagamoyo ambayo ilikuwa Kitanzi kwa taifa na maono ya kuimarisha Uchumi wetu. Hongera sana Raisi kwa hilo.

Watendaji wako ndio vichaa maana ndio walikuwa wanashinikiza kuendelea na Bandari hiyo hata bungeni wakasema serikali ij na majibu.

Majibu sawia uliyatoa na naamini ulikuwa miogoni mwa baraza la mawaziri liliokaa kabla hujawa raisi na ulijua fika tulivyokuwa tunaenda kuumizwa na wachina.

Wachina ni Maadui wa Uchumi kwa nchi zinazoendelea na wanatumia kila aina ya tricky kudanganya hasa wanapokutana na viongozi wasio na maono. Werevu watakuelewa kupitia video hii..
 
Utamsaiadiaje mtu ambaye kurudi reverse kwa kasi huku amefumba macho anaamini kwa dhati kabisa kuwa ndo kusonga mbele?
Ninalielewa hilo ila angalao angepata washauri wazuri wakatenda kama kina Lukuvi at least tungeweza kusonga mbele. Ardhi ilikuwa tatizo at least kuna kamwanga na vivyo hivyo kuhusu uwekezaji tungekuwa na Mawaziri sahihi tungesonga mbele pia.. Magu akipata washauri wazuri najua fika atabadili kitu maana ana uthubutu poteleambali maamuzi mengine yanayoligarimu Taifa. Anajenga Discepline kiasi fulani na akikosea anajisahaulisha anafaya tofauti.. Mfano mzuri tena ni Majadiliano yanayoendelea kuhusu bomba la mafuta ambapo walijikuta kuigia cha kike sasa wananegotiate baada ya kujikuta wataamba hasara. Sasa Mazingira kama haya at least yanaleta tumaini flani. Mchina anayonga chumi zetu na anatumi walafi kama kina Ndyughai kupentrate ..
 
Kumbe tunakimbizana na ndoto za mtu!
Ni kweli Katika Sifa za Kiongozi bora i azima awe Visionary/ Focused, awe na Uthubutu, decision maker not leaser-fair na anasimamia maamuzi yake regardless kakosea ila right way. So kwa Maamuzi mengi alofanya naamini yaikuwa na nia njema na japo mengine ya kukomoa.. Kwa tulipokuwa tulihitaji sana kuvaa miwai ya Mbao. Tunasuburia Mkataba wa bomba la gesi tena na Bashite ndio nitakuwa nimejenga imani yangu zaidi kwake..
 
Mtu alisha sema hashauriki, yeye sio mwana siasa, sasa hao viongozi watashirikiana nae vipi?
 
Nimewiwa kupost ujumbe huu maana nilivutiwa sana na baadhi ya mambo aliyoyaongelea Rais siku anakutana na Wafanyabiashara Ikulu juzi na miongoni ya mambo ni kuwaruhusu wafanyabiashara kufunguka na kuonesha uhalisia w hali ilivyo mbali na kudanganywa wa watendaji wake hapo nyuma.

Zaidi ya yote ni action kuhusu bandari ya bagamoyo ambayo ilikuwa Kitanzi kwa taifa na maono ya kuimarisha Uchumi wetu. Hongera sana Raisi kwa hilo.

Watendaji wako ndio vichaa maana ndio walikuwa wanashinikiza kuendelea na Bandari hiyo hata bungeni wakasema serikali ij na majibu.

Majibu sawia uliyatoa na naamini ulikuwa miogoni mwa baraza la mawaziri liliokaa kabla hujawa raisi na ulijua fika tulivyokuwa tunaenda kuumizwa na wachina.

Wachina ni Maadui wa Uchumi kwa nchi zinazoendelea na wanatumia kila aina ya tricky kudanganya hasa wanapokutana na viongozi wasio na maono. Werevu watakuelewa kupitia video hii..
Magufuli alisign huo mkataba kwa niaba ya nchi akiwa ujenzi hata china alienda harafu miezi sita iliyopita alisema wachina wazuri sana ni rafiki ni wema wanatoa misaada bila masharti magumu haya anayoyasema yanatoka wapi
 
Ningumu kufanya kazi na mtu asiyeeleweka na asiye na specific direction...
Leo tunaambiwa kusanya Kodi kikamilifu kesho unafukuzwa kwa kupush ikusanywe kikamilifu.
Leo unaahidi milioni hamsini kila kijiji,kesho unasema umeona ubadili ununue ndege so ulitapeli watu kwa ahadi hewa?
Leo tunatekeleza miradi kwa pesa zetu,kesho ni mkopo toka BOA au WB.
Leo nashkuru katiba imefikia pazuri tutaimalizia,kesho sitowapeleka kuunda katiba mtafaidi posho.
Leo nitaamia Dom mwaka huu kesho bado namtibu mamaangu!?
 
kirengased bwana!
 
JPM anamapungufu yake lakini nashukuru Mungu yuko makini sana na wachina, yaani hao jamaa ukiwa mjingamjinga unawauzia nchi mchana kweupe.
Mzee wa msoga ametuangusha sana kwa hao wachina, tumepigwa hadi gesi.
 
Ili Rais Magufuli atimize ndoto zake kwa ajili ya maendeleo ya nchi hii Ni muhimu azingatie:
1. Kuheshimu taasisi zilizowekwa kisheria na kufanya nazo kazi.
2. Kupata ushauri kutoka katika taasisi na jumuiya za kijamii kabla ya kutafuta ushauri kutoka kwa makundi yaliyotawanyika. Mfano, amekutana na wafanyabiashara ambao kila mmoja analalamika kivyake. Matokeo yake ni uchonganishi kwa wasaidizi wa Rais na kusababisha kutumbuliwa kwao. Hapa nazungumzia Jumuiya ya wafanyabiashara kama taasisi ilipaswa kuchukua jukumu lake kuliko wafanyabiashara kuchaguliwa na MaDC.
Hata alipokutana na viongozi wa dini,hali ilikuwa ni hiyo hiyo. Hatukuona viongozi wa TEC CCT, Pentecostals, Wasabato na BAKWATA. Walikuwepo baadhi ya viongozi wanaoongoza makanisa yao,
Kwa Nini Rais anakwepa taasisi zinazotambulika!!?
Binafsi nafikiri anatumia mtndo wa ki Machiavelli wa wagawanye upate kuwatawala kiulaini.
3. Mapambano ya kuiendeleza nchi yanahitaji ushirika mpana wa Jamii nzima iliyo huru: Bunge huru, Media huru, Vyama vya Siasa huru na vya kidemokrasia, Asasi huru za kijamii, Dini na madhehebu huru, Mahakama huru, Wasimamizi wa vyombo vya dola wanaoshirikishwa lakini wakiwa huru katika kutoa maamuzi, na mwisho Katiba nzuri itakayosimamia kila taasisi katika Taifa.
Bila hayo, juhudi zote za kugawanya ili kutawala hazitasaidia chochote Cha maendeleo, badala yake itakuwa Ni kujitafutia sifa nyuma ya migongo ya mawaziri na watendaji wanaogeuzwa mbuzi wa kafara kwa kutumbuliwa!!!!
 
Ni kweli Katika Sifa za Kiongozi bora i azima awe Visionary/ Focused, awe na Uthubutu, decision maker not leaser-fair na anasimamia maamuzi yake regardless kakosea ila right way. So kwa Maamuzi mengi alofanya naamini yaikuwa na nia njema na japo mengine ya kukomoa.. Kwa tulipokuwa tulihitaji sana kuvaa miwai ya Mbao. Tunasuburia Mkataba wa bomba la gesi tena na Bashite ndio nitakuwa nimejenga imani yangu zaidi kwake..
Ndoto? Yaani ameota kakiona choo ameingia kukitumia wewe unamsifu
 
Back
Top Bottom