Tunahitaji Udikteta zaidi ya huu? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tunahitaji Udikteta zaidi ya huu?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Speaker, Jan 9, 2012.

 1. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #1
  Jan 9, 2012
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Toka raisi JK azomewe mwaka jana (2011) pale UDSM kwenye maadhimisho
  ya miaka 50 ya kuanzishwa UDSM,kumekua na udikteta unao endelea kila kukicha
  nchi nzima kwa vyuo takribani vyote.

  Kwa mfano,UDSM walifukuzwa wanachuo 43,bila sababu za msingi,...sababu ya kiubabaishaji
  ikiwa ni kufanya fujo na mikusanyiko isiyokuwa halali.

  UDOM week iliyo pita,baada ya kuwa wame cheleweshewa hela zao takribani mwezi mzima waliamua
  kuandamana kwenda utawala kujua hatma ya hela zao,waliambiwa wangepata kesho yake.
  Lakini siku hiyo hiyo waliyo goma kidogo walipata hela zao,na kesho yake wanafunzi zaidi ya 15
  walifukuzwa kwa sababu ya "kuchochea mgomo na uvunjifu wa amani"

  St.John chuo walikua na matatizo kama ya vyuo vyote kwa wanafunzi wanaopata mkopo,walipo goma
  kudai haki yao,walifukuzwa wote na kurudishwa kwa masharti magumu sana.

  Yanayo endelea Muhimbili kila mtu anayajua,magazeti yameelezea kwa undani zaidi.

  Seikali ya wanafunzi pale UDSM huwa na kikao kimoja cha bunge (kikao halali) mara moja kwa semester.
  Jumamosi iliyopita 7/1/2012 walikaa na kuamua ku-question wenzao kufukuzwa bila sababu za msingi
  wakidai ni uonevu.
  Kikao kile alihudhuria dean of students,kwa hiyo kilikua halali na maazimio yake ilikua ni kuwa na shinikizo la kutaka wanafunzi walio
  fukuzwa warudishwe,....utawala ulipata habari hizi na kwa haraka sana,prof.Mgaya akatoa karipio kali na vitisho
  kwamba atakaye shiriki mara moja atarudishwa kwao,...na hakuna ruksa ya kukusanyika maana utakuwa defined kwamba
  una hamasisha mgomo.

  Viongozi wa serikali ya wanafunzi walitoa maazimio ya kikao chao cha bunge tarehe 9/1/2012 asubuhi,...wakiwa wana
  tafuta uungwaji mkono wa 2/3 ya wanachuo wote katika kushinikiza walio fukuzwa kwa kuonewa warudishwe.

  Usiku huu,wame pigiwa simu wakitakiwa kwenda kuchokua barua zao warudi makwao haraka sana....kwa style ya UDSM
  ya sasa,hii ni 3/4 ya kufukuzwa mazima maaana utasubiri kuitwa chuo hadi Yesu arudi.

  Uko wapi uhuru wa kujieleza,?
  Iko wapi haki ya kukusanyika?
  Je,hii ndio adhabu anayotoa JK kwa wanafunzi baada ya kudhalilishwa?

  Hali itakuaje/ikoje mtaani watu wanapodai haki zao?

  Huu ni udikteta.
   
 2. kaburungu

  kaburungu JF-Expert Member

  #2
  Jan 9, 2012
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 1,608
  Likes Received: 2,461
  Trophy Points: 280
  Mkuu wanaotakiwa kuchukua barua ni viongozi au?
   
 3. Speaker

  Speaker JF-Expert Member

  #3
  Jan 9, 2012
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 6,357
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Yeah,kwa kesho viongozi woote wanaenda kuchukua barua za kwenda nyumbani.
  Naona wanataka kuwa fukuza ili common wanachuo waogope kufanya mgomo wowote.
  OR
  Ikitokea kesho wanachuo wote wakagoma,basi wote watapewa barua kwenda makwao.
   
 4. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #4
  Jan 10, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,154
  Likes Received: 2,406
  Trophy Points: 280
  Wanafunzi wa sasa waoga sana yani me ningekuwa mwanafunzi leo ningelipua makazi ya mkandara hapo,na kuna kipindi ticha flani hapo alikua ananizingua na nilipanga nilipue utawala sema tulienda nae sawa,hawa washenzi dawa yao ni kulipua yani mnashindwa kujioganaiz wanafunzi hata wa5 mkanunua guruneti na kulipua utawala? Kama mbwai mbwai tu hii nchi mbele haitotawalika biliv dat I'm tellin y'all buddiez
   
 5. R

  RMA JF-Expert Member

  #5
  Jan 11, 2012
  Joined: Oct 10, 2010
  Messages: 409
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni vema hizo shida mlizo nazo watanzania zikaendelea kwa kasi, tena mara saba zaidi ili mjifunze!!! Hayo ndio matunda ya kupiga kura kama vipofu!! Hiyo serikali mnayoilalamikia kwani iliingia msituni na kutwaa madaraka?? Si mliichagua kwa kura zenu wenyewe? Tulieni hadi mtakapopata akili na mang'amuzi!!
   
Loading...