Hicho unachoongelea ndio mpango mzima utakaoweza kututoa kutoka point A to B, naunga mkono hoja kwa sasa hakuna dira kama taifa na hapa hakuna wakuvuna lawama zaidi ya uongozi uliopo madarakani. Watu wengi washabiki wa serikali wanapenda kutetea maswala ya namna hii kwa kuonyesha uwingi wa vyuo na idadi ya wahitimu leo ukilinganisha na zama za nyuma.
Kitu ambacho hawakigusii ni kwamba zamani tulikuwa tukitoa wahitimu wachache lakini wengi walikuwa directed kwenye sector moja kwa moja, wasomi walizalishwa kutokana na uwezo wa uchumi na market labour zilizokuwepo. Leo idadi ya wahitimu kubwa ambao wanasoma bure na mikopo ya serikali wengi wana miaka mingi sasa ajira hawajapata kwa upande mwengine huu ni utumiaji mmbaya wa resources unless labda somebody is funding these ambitions indirectly kupitia hiyo misaada ya donors.
Kuwe na misaada kusiwe na misaada jinsi serikali inavyo fund elimu hasa ya juu kuna umuhimu wa kuwa na dira na kutoa wahitimu wengi ambao wanaweza pelekwa sehemu. Inabidi kuwe na plan ambayo hipo coordinated kati ya sera kuu, wizara ya elimu na vyuo vikuu.
Kwa mfano leo chini ya kilimo kwanza unaenda toa ma sociologist halafu ujui huwapeleke wapi kwanini wahusika hawakulifikiria hili. Nadhani inabidi sasa tuwe na coordination inayo eleweka leo wakulima wengi sana wanafaidika na sera za kilimo kwanza, matatizo ya chakula yanapungua hila sasa mazao yanaoza. Solution inayotumika nikuwafundisha wakulima ujasiriamali mara baada wanapovuna si swala baya, lakini unajiuliza kwenye nchi ambayo imejaa vijana wengi wasio na ajira kwanini serikali isiwekeze na hawa vijana ndio waingie kuwa wajasiriamali na kuongeza wigo la ushiriki katika uchumi wa taifa.
Ili kufikia huko sasa unajikuta na vyuo vinalenga sana kwenye course za kilimo kama ni uchumi au biashara course nyingi zijikite na kilimo ambapo wahitimu wataweza ona opportunities na kuweza hata kutoa mapendekezo ya kuboresha changamoto hili waweze shiriki kifaida maana watakuwa wamesoma ie upatikanaji wa mikopo, changamoto za usafiri, soko etc, hili wahusika waweze kuja na sera mbadala za ku adress hizo changamoto.
Vilevile serikali za mitaa badala ya kuendela na tamaduni za tender ni vyema wakawa na timu zao za ma-architectures, planners, na namna za kuongeza mapato yao hata kwa vijijini maana kwa sasa naona ni manispaa za mjini tu ndio zinazofaidika zaidi, vijijini changamoto wao ni kujenga mashule tu mi naona more needs to be done kuahikikisha there is inclusiveness of all tanzanians hata vijijini kuna mbinu za kujiongezea mapato katika serikali zao na kutoa ajira nyingi tu zaidi ya mabwana shamba.
Something has to be done tupo kwenye karne ambayo hatuhitaji kuwa wabunifu vile case studies zimejaa leo na there is enough archive from developed nations on the stage we are and how they evolved from there, kuwa na resources tulizokuwa nazo na kubaki maskini ni uzembe tu kutoka kwa wahusika there is no other justification.