Tunahitaji kilicho bora kama watanz

Kiraka Kikuu

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
5,904
1,976
Wasalaam wana JF!

Kwa muda sasa kumekuwa na msukumo mkubwa wa kujaribu kulinganisha juu ya yupi miongoni ya viongozi wa CCM
ana "uafadhali" katika ugombea wa urais mwaka 2015.Wengi wametajwa na kulinganishwa hapa kama LOWASSA, MEMBE, SITTA hadi MAGUFULI!!!!

Lakini sisi kama watanzania lazima tukumbuke jambo moja: Tunahitaji rais bora na si mwenye uafadhali! Si lazima sana nchi hii iongozwe na CCM, ndio maana vyama vingi vikaanzishwa.

Ni lazima sasa tufikirie kupata uongozi utakao tuvusha toka hapa tulipo kama watanzania.Uongozi utakao weza kubadili mfumo wa uongozi serikalini toka mfumo wa kifisadi hadi mfumo wa UADILIFU;

Viongozi watakao himiza utamaduni wa uwajabikaji serikalini na kuhimiza watanzania kufanya kazi kwa bidii;Viongozi watakao linda mali asili za taifa letu,na kutetea utu wetu kama watanzania.

Kwa sasa sioni mwingine, bali Dr W.P. SLAA kama chaguo sahihi.

Ni mtazamo wangu, nakaribisha maoni!
 
Back
Top Bottom