Tunahakiki qualifications au vyeti feki?

Tunahakiki qualifications au vyeti feki?

M
Binafsi nilistushwa na Kujihami kwa Bi. Angela Kairuki. Nilicho kiona si Prof. Ndalichako wala Angela Kairuki wala Simbachawene yupo tiyar kuona kitumbua chake ki kiingia mchanga.

Heading (Title) ya Majina yaliyo chapishwa ktk report ni Orodha ya watumishi walioghushi vyeti vya Elimu. Maajabu Wakati wa kukabidhi report hiyo huyu Bibi Mnafiki anasema Viongozi wa Kisiasa (Wabunge, mawaziri, Ma RCs na Ma DCs) hawakuhakikiwa kwa sababu sifa yao ya kuchaguliwa au kuajiriwa ni kujua kusoma na kuandika tu. Karne ya 21!!!
Hata Wabunge tuna taka sifa iwe Bachelor Degree. Form 4 Div 3 Form 6 Div 3. Ikumbukwe UHAKIKI haukuwa wa SIFA ZA MTU (Qualifications) bali U FEKI wa VYETI!! Huo wa sifa mtafanya baadae baada ya huu wa vyeti kuisha.

Lengo langu hapa ni kumrekebisha. Zoezi halikuhusisha kuangalia sifa za Wa ajiriwa bali uhakiki wa cheti kama ni halali (ORIGINAL) au ni cha kughushi (FAKE).

Kwa mantiki hiyo zoezi tunaomba liguse watu wote hasa wanao lipwa kwa kodi za wananchi. IWEJE ZOEZI LISHINDWE ma DC 130, ma RCs 26, Wabunge 320 ili hali wameweza watu 500,000.

Pia naomba zoezi hili lielekezwe na Private Sector.

Kwani kati ya watumishi wa serikali laki 5 watu 9,929 wana vyeti feki huku 1,532 wanatumia cheti kimoja zaidi ya mtu mmoja. Je Private sector iliyo ajiri takribani watu 2M hali ikoje? Je hakuna watumishi wa umma (serikali) wanaomiliki vyeti vya watu walioko Private Sector? Ili zoezi liwe na ufanisi mkubwa angalau by 80% ina paswa nchi nzima ihakikiwe.

Ni wajibu wa serikali kuwataka wa ajiri wote watume taarifa (Majina ya mtu, Index no za vyeti vya secondary, na chuo) za Waajiriwa wao ( TCU, NECTA, NACTE, UTUMISHI, nk). Kwa huu mzunguko hakuna atakae pona (kukwepa).

Hili zoezi pia lisi ishie vyeti vya Form 4 na form 6 tu waende hadi na vya chuo kikuu.

Tz haina tatizo la ajira nchini. Tatizo ni watu kukalia nafasi/ajira zisizo za kwao.

Mhe: ANGELA KAIRUKI TUOMBE RADHI WATANZANIA kwa kutufanya sisi wajinga na tunaomba umhakiki Specifically PAUL C. MAKONDA . Mnamuogopa yy ni nani hapa Tz? Hivi unafahamu ktk hii Loophole ya Makonda ni wangapi wenye vyeti feki wamepenya?

HAKI SAWA KWA WOTE.
Mwanasiasa sio Mwanataaluma na Mwanasiasa anaweza kuwa hata cheti kimoja hana lakini ana sifa ya kujua kusoma na kuandika ndugu.

Na ndiyo maana ktk uteuzi wa Rais hana mpaka. Sasa ulitaka Angela Kairuki aende kwa mwanasiasa kuhakiki kama wanajua kusoma na kuandika??

Zoezi lilikuwa ni uhakiki wa uhalali wako wa mtumishi wa umma! Vyeti ilikuwa ni sehemu tu kuna mambo mengi yameangaliwa.

Kuna watu wameondolewa kwasababu sio RAIA wa nchi na wameajiriwa kama watanzania ila wameshindwa kuthibitisha utanzania wao.
 
Nisome vizuri,sijasema Private Sector hawatakiwi kukagua vyeti, bali waajiri wenyewe kwenye Private Sector ndio wenye jukumu la kujiridhisha na uhalali wa vyeti vya wafanyakazi wao.
Lakini pia Private Sector, performance na delivery ni vitu muhimu zaidi kwao.
Hii ni requirements za nchi siyo upende (inakuwa sheria). Serikali inawajibu wa kulinda taaluma, ajira za Wasomi na ujuzi wa watu. Hakuna nchi duniani imewahi kufanikiwa au kuwa na ubunifu bila kuwa na wasomi walio bobea. Hii dhana ya performance ni historical concept, ktk mazingira ya karne ya 21 huwezi jigamba una ujuzi bila kuwa na elimu yake huenda uwe fundi majiko mkaa na ndio maana Mwanahabari Diploma ndio minimum Qualifications.

Hivyo hivyo sekta ya Afya, Engineer-BODI yao, Wahasibu-NBAA, na kila sekta na vigezo vyao.
 
M

Mwanasiasa sio Mwanataaluma na Mwanasiasa anaweza kuwa hata cheti kimoja hana lakini ana sifa ya kujua kusoma na kuandika ndugu.

Na ndiyo maana ktk uteuzi wa Rais hana mpaka. Sasa ulitaka Angela Kairuki aende kwa mwanasiasa kuhakiki kama wanajua kusoma na kuandika??

Zoezi lilikuwa ni uhakiki wa uhalali wako wa mtumishi wa umma! Vyeti ilikuwa ni sehemu tu kuna mambo mengi yameangaliwa.

Kuna watu wameondolewa kwasababu sio RAIA wa nchi na wameajiriwa kama watanzania ila wameshindwa kuthibitisha utanzania wao.
Uwe unasoma heading na kuelewa. Hoja: uhakiki ulikuwa wa vyeti au wa sifa?
 
Uwe unasoma heading na kuelewa. Hoja: uhakiki ulikuwa wa vyeti au wa sifa?
Siyo lazima heading yako iendane na zoezi lilivyokuwa ktk ground.

Usilazimishe mambo yako na mawazo yako tuyajadili tu

Zoezi lilikuwa ni comprehensive mambo mengi sana yameangaliwa ndani ya zoezi hilo sio kila kitu utawekewa mezani
 
Siyo lazima heading yako iendane na zoezi lilivyokuwa ktk ground
Jadili mada tajwa hapa.

Kwann ww pekee ndio uliehakikiwa tu?

Report imeandikwaje? Sifa au vyeti feki?
 
Ila Mkuu kwanini no.1 wasiangaliwe japo kwa kupigwa fine kisha taaluma zao zikarasmishwa kihalali japo walizipata kwa njia ya panya? ikizingatiwa nyuma yao kuna wengi wanawategemea??
Mkuu hata wauza ngada na o kuna wanao wategemea nyuma na wameanza zaman biashara hiyo lakin wakikamtwa sheria inachukua mkondo, kufanya kazi kwa ufanisi sio sababu za kuhalalisha kosa la kupata kazi hiyo isivyo halali.
 
Back
Top Bottom