Tunafunga milango ya rushwa ni kufungua milango ya ujambazi

Tunafunga milango ya rushwa ni kufungua milango ya ujambazi

chikub

Senior Member
Joined
Oct 15, 2015
Posts
110
Reaction score
28
"Hapa ni kazi tu" kazi kwa wananchi zipo?
Ni jambo zuri sana kutokomeza vyanzo na mazalia yote ya rushwa nchini, LAKINI hali yetu ilivyo sasa hairuhusu kabisa kuiondoa rushwa kwenye jamii. Jamii yetu haijaandaliwa kuishi bila kutoa na kupokea rushwa kutokana na uhaba mkubwa uliopo wa rasilimali watu, vitu na fedha. Watu wachache wanaiba fedha, vitu, na muda wa waajiri wao ili kujihudumia na kuwahudumia watu wengine walio wengi ndani ya jamii. Mishahara ya watumishi ni midogo saana, wakulima wanalima kidogo sana, wafugaji wanafuga kidogo sana, wavuvi wanavua kidogo saana tena bila ya utaalamu wa aina yoyote. Vyuo na hospitali za watu binafsi nchini huwa pia vinategemea sana majizi yanayoiba muda wa mwajiri wao (serikali) na kwenda kufundisha na kutoa huduma kwenye taasisi hizo za private (part-time).

Hivyo, majizi ya fedha, mali na muda wa waajiri ndo wanaokwapua mali, muda na fedha walivyoiba na kuzipeleka kwa wananchi wa kawaida kwa njia mbalimbali kama vile kutoa huduma, kutoa ajira kwa wananchi pale wanapotumia pesa za wizi kujenga majumba, kulima mashamba, kununua magari, kufanya biashara, kunywa bia na nyama choma kupita kiasi na kuwahudumia ndugu zao walioko vijijini.

Unapokomesha rushwa na ubadhilifu maana yake unakomesha pia ajira kwa mafundi washi, rangi, mbao, umeme, madereva, hivyo utawanyima fedha pia mama ntilie, wazazi vijijini, wauza njama, mchele na vifaa vya ujenzi. Hii maana yake nini? maana yake mzunguuko wa hela ndani ya jamii utapungua sana hivyo ujazo wa fedha kwenye jamii utapungua pia. Maana yake nini? ukosefu wa pesa utasababisha wanunuzi wawe wachache, hivyo bidhaa zitashuka bei, ada za shule na matibabu hazitalipwa na watu watalazimika kutafuta mbinu zingine za kuishi. Mbinu hizo ni kama zipi? miongoni mwa mbinu hizo ni pamoja na kufanya kazi kwa bidii ili kuongeza kipato, kurudi vijijini na kulima/kufuga/kuvua/kuchimba madini/kuchoma mkaa, kuacha kusomesha watoto wao NA kujiingiza kwenye vitendo vya uhalifu kama vile wizi na ujambazi.

Kuziba mianya ya rushwa nchini lazima kuende sambamba na kuongeza fursa za ajira kwa vijana, kuongeza mishahara ya watumishi ili ikidhi kuhudumia familia na wazazi walioko vijijini wanaowategemea watoto wao na kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo, ufugaji na uvuvi na masoko ya bidhaa zao na kuzalisha wataalamu wengi sana katika fani mbalimbali. Vinginevyo tutachemsha tu, nchi hii ilishavurugwa sana na lile Azimio la Zanzibar. Hivyo taifa lazima tupambane na wezi wa mali za wengi lakini pia tusisahau kujipanga kukabiliana na ombwe litakaloachwa na kuzibwa kwa mianya ya ukwepaji kodi, rushwa na wizi wa muda na mali za waajiri.
 
Kazi ni shughuli yoyote ya halali inayompatia mtu kipato chake

Source: Mwalimu wa siasa Darasa la NNE.

Hakuna ombwe lolote kama wezi wote wakijitambua
 
Kumbuka Serikali inapobana mianya na Rushwa na kukusanya Kodi inavyotakiwa ,hiyo hela hurudi tena kwenye kufanya huduma za jamii kama kujenga barabara,huduma za afya shule nk.Huo ndo mzunguko chanya ambao unakua na impact ya moja kwa moja kwa jamii nzima.Hakuna taifa limeendelea duniani kwa kutegemea wala rushwa walete hela izunguke.

Kama hao wala rushwa wangekua wanajenga barabara hapo ningekubaliana na wewe.Chukua mfano wa safari za nje za bajeti mbili zilizopita tiketi za ndege tu ilikua Tsh bilioni 150,hapo waliofadika na mashirika ya ndege kama Emirates,maana yake hela ilienda uarabuni.Sasa tumezuia safari za nje,hiyo hela itabaki Tanzania kuendeleza nchi.Acheni majibu yatumbuliwe .
 
"hapa ni kazi tu" kazi kwa wananchi zipo?
Ni jambo zuri sana kutokomeza vyanzo na mazalia yote ya rushwa nchini, lakini hali yetu ilivyo sasa hairuhusu kabisa kuiondoa rushwa kwenye jamii. Jamii yetu haijaandaliwa kuishi bila kutoa na kupokea rushwa kutokana na uhaba mkubwa uliopo wa rasilimali watu, vitu na fedha. Watu wachache wanaiba fedha, vitu, na muda wa waajiri wao ili kujihudumia na kuwahudumia watu wengine walio wengi ndani ya jamii. Mishahara ya watumishi ni midogo saana, wakulima wanalima kidogo sana, wafugaji wanafuga kidogo sana, wavuvi wanavua kidogo saana tena bila ya utaalamu wa aina yoyote. Vyuo na hospitali za watu binafsi nchini huwa pia vinategemea sana majizi yanayoiba muda wa mwajiri wao (serikali) na kwenda kufundisha na kutoa huduma kwenye taasisi hizo za private (part-time).

Hivyo, majizi ya fedha, mali na muda wa waajiri ndo wanaokwapua mali, muda na fedha walivyoiba na kuzipeleka kwa wananchi wa kawaida kwa njia mbalimbali kama vile kutoa huduma, kutoa ajira kwa wananchi pale wanapotumia pesa za wizi kujenga majumba, kulima mashamba, kununua magari, kufanya biashara, kunywa bia na nyama choma kupita kiasi na kuwahudumia ndugu zao walioko vijijini.

Unapokomesha rushwa na ubadhilifu maana yake unakomesha pia ajira kwa mafundi washi, rangi, mbao, umeme, madereva, hivyo utawanyima fedha pia mama ntilie, wazazi vijijini, wauza njama, mchele na vifaa vya ujenzi. Hii maana yake nini? Maana yake mzunguuko wa hela ndani ya jamii utapungua sana hivyo ujazo wa fedha kwenye jamii utapungua pia. Maana yake nini? Ukosefu wa pesa utasababisha wanunuzi wawe wachache, hivyo bidhaa zitashuka bei, ada za shule na matibabu hazitalipwa na watu watalazimika kutafuta mbinu zingine za kuishi. Mbinu hizo ni kama zipi? Miongoni mwa mbinu hizo ni pamoja na kufanya kazi kwa bidii ili kuongeza kipato, kurudi vijijini na kulima/kufuga/kuvua/kuchimba madini/kuchoma mkaa, kuacha kusomesha watoto wao na kujiingiza kwenye vitendo vya uhalifu kama vile wizi na ujambazi.

kuziba mianya ya rushwa nchini lazima kuende sambamba na kuongeza fursa za ajira kwa vijana, kuongeza mishahara ya watumishi ili ikidhi kuhudumia familia na wazazi walioko vijijini wanaowategemea watoto wao na kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo, ufugaji na uvuvi na masoko ya bidhaa zao na kuzalisha wataalamu wengi sana katika fani mbalimbali. Vinginevyo tutachemsha tu, nchi hii ilishavurugwa sana na lile azimio la zanzibar. Hivyo taifa lazima tupambane na wezi wa mali za wengi lakini pia tusisahau kujipanga kukabiliana na ombwe litakaloachwa na kuzibwa kwa mianya ya ukwepaji kodi, rushwa na wizi wa muda na mali za waajiri.

ole wenu. Jaribu uone katika awamu hii.
 
Mleta mada kaweka angalizo tu.... sio kwamba anakubaliana na wizi..... think outside the box wandugu.....
 
Kumbuka Serikali inapobana mianya na Rushwa na kukusanya Kodi inavyotakiwa ,hiyo hela hurudi tena kwenye kufanya huduma za jamii kama kujenga barabara,huduma za afya shule nk.Huo ndo mzunguko chanya ambao unakua na impact ya moja kwa moja kwa jamii nzima.Hakuna taifa limeendelea duniani kwa kutegemea wala rushwa walete hela izunguke.

Kama hao wala rushwa wangekua wanajenga barabara hapo ningekubaliana na wewe.Chukua mfano wa safari za nje za bajeti mbili zilizopita tiketi za ndege tu ilikua Tsh bilioni 150,hapo waliofadika na mashirika ya ndege kama Emirates,maana yake hela ilienda uarabuni.Sasa tumezuia safari za nje,hiyo hela itabaki Tanzania kuendeleza nchi.Acheni majibu yatumbuliwe .
Hela iliyookolewa hapo isipomuwezesha mwananchi wa kijijini kupata milo angalau 2 kwa siku itakuwa haina maana kwao. Maana hata kwenye hizo safari watu walikuwa wanapata posho ambazo wakirudi nyumbani wanazitumia kwa kulipia ada za watoto wao na pengine kutoa ajira kwa vijana kwa njia ya kupelekwa airport na kujenga nyumba zao. Je, mishahara ya watumishi kama ilivyo sasa inatosha kutoa ajira hata kwa watu 5 kwa njia ya kulipa vibarua wanaojenga nyumba zao? mishahara yao inawawezesha kumiliki magari na kujenga nyumba? inatosha hata kumlipa vizuri house girl?
 
Mleta mada kaweka angalizo tu.... sio kwamba anakubaliana na wizi..... think outside the box wandugu.....
Wanakurupuka tu hawasomi mada. Kila jambo lina uzuri na ubaya (opportunity cost) ni jukumu lako kuchukua tahadhari, usichukuliwe na mihemko tu, fanya uchambuzi
 
Ndio maana kila siku huwa nasema JF imeingiliwa hata wasio jua mambo wako humu mfano halisi ni huyu mleta mada. kwake yeye anaona rushwa ni jambo jema na kwa mawazo yake rushwa ikifutwa yeye atafanya ujambazi!! inawezekana yeye yupo kwenye kitengo kinacho pokea rushwa na ana uwezo wa kuwa jambazi, tukutakie kila la heri kwenye ujambazi wako halafu uone utadumu muda gani.
 
Back
Top Bottom