Tunaenda tukiwa washindi hatuendi kushindana

Tunaenda tukiwa washindi hatuendi kushindana

activisty

JF-Expert Member
Joined
Apr 1, 2012
Posts
315
Reaction score
107
Uvumilivu una mwisho wake.tumewapa kazi zaidi ya miaka 50 sasa, kila uchaguzi ukifika tofauti tunayoiona ni rais kumaliza mda wake kwa kutuongezea vile vikwazo vya maendeleo toka vitatu alivoviacha mwalimu. Sasa ni ujinga,maradhi, umasikini, rushwa, ufisadi, njama, hila, unafiki, tamaa, uchawi na mabavu katika uongozi.

Shkamoo mzee wa kila kitu free , shkamoo mzee wa malofa, shkamoo mzee mambo ya pwani...

Mlifanya kazi lakini si toshelezi hata kidogo...mlikua na nafasi ya kufanya zaidi...

Mmetengeneza na kutuachia serikali dhoofu zaidi kuwai kutokea kwa takribani miaka 30 mliyofanya kazi.

Sasa kisayansi na kiutaalamu mmetutengenezea wapinzani ushindi kwani kila sehemu tunayogusa mliwaumiza raia.na kwa kushindwa kwenu kutatua matatizo ya wananchi kwa miaka yote hiyo, mnatufanya tuende kwenye uchaguzi tukiwa washindi na hatuendi kushindana.

By mpinzani huru
 
Afadhali umewaambia. Magufuli anakomaa nayo kwa kupotosha watu. Hatusemi hakuna kilichofanyika.tunasema kilichofanywa hakilingani na kile kilichostahili kufanywa.ee!! Hawa watu vp!!

Kabisa kilichofanywa ni kidogo sana kulinganisha na kile kingeweza kufanyika
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom