Wakati najiandaa kuandika waraka nilioupa jina "Msajili wa vyama vya siasa unataka nini tukusaidie" nikakutana na taarifa ya ofisi ya Chadema kuchomwa moto huko Tunduma. Naomba niyajadili yote kwa pamoja na kwa ufupi.
Pamekuwa na tuhuma na kuandikiana barua na kujibishana kati ya Chadema na Msajili wa vyama vya siasa. Ukichunguza kwa umakini tuhuma wanazotuhumiwa unaona ya kuwa sio wao wa kwanza kuzitenda lakini wamekuwa wa kwanza kuandamwa na kuandikiwa barua lundo. Chama kikongwe cha siasa kupitia wasemaji wake na waenezi wamewahi kutamka matamko makubwa na makali lakini hatukusikia kuandikiwa wala karipio.
Hapa ndipo ulipo msingi wa swali langu kuwa ni kipi akitakacho Msajili toka Chadema, tunaweza kumsaidia. Kama dhamira ni kukidhofisha njia zipo nyingi na mojawapo ni kutumia sheria zilizopo au kutunga mpya ambazo kwa hulka na mwenedo wa Chadema watanasa haraka (Uzungumzaji wa Lissu, misimamo ya Kigaila na wengine).
Jambo la pili ni kutumia kigezo cha maendeleo kama ambavyo kimetumika kuzima mijadala ya Katiba mpya.Bunge lina wawakilishi wengi kutoka chama kimoja na ni rahisi kupitisha miswaada kwa kadri watakavyo.I pitishwe sheria ya kusitisha shughuli za kisiasa kwa miaka mitano ili kuipa serikali muda wa kufanya maendeleo.
Uchomaji wa ofisi na ukamataji wa wanachama wa Chadema. Hili limeanza kuwa jambo la mazoea sasa, Dodoma ilitokea,huko Mwanza na leo huko Tunduma na walio na mawazo mafupi wanaamini ya kuwa itatisha watu. Ni kweli imetisha na itatisha lakini ni kwa muda gani Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye.
Hao watakaoogopa kutishika siku wakayoamua kuacha kuogopa watafanya nini,Mwenyezi Mungu ndiye ajuaye lakini naamini hakitakuwa kipindi kizuri.
TUTAFAKARI KWA PAMOJA