Tunachezewa sana, Serikali irudishe tozo zetu

Tunachezewa sana, Serikali irudishe tozo zetu

Freyzem

JF-Expert Member
Joined
Jun 29, 2013
Posts
10,180
Reaction score
24,798
Bunge lilipitisha tozo batili kwenye miamala kwa kisingizio cha serikali kujionezea mapato ili kuboresha miundombinu na kujenga madarasa!

Happ awali ile miezi kama miwili baada ya tozo kuanza tulielezwa ni kiasi gani kimepatikana na kilienda wapi, lakini baada ya hapo kukawa na usiri mkubwa wa kiasi kilichopatikana na matumizi yake. Hivi sasa eti tozo zimefutwa, na wale waliopitisha huu ubatili wanashangilia. Serikali imefeli kwenye hili, kwanza itueleze kwa mwaka mzima waliochukua tozo walikusanya kiasi gani na zimetumikaje!

Kama ni kujenga madarasa mbona bado kuna shule kibao tu wanafunzi wanakaa 90 darasa moja?
Kama wameboresha miundombinu ya barabara mbona barabara zipo nyingi, tu hawajui hata kama kuna kitu kinaitwa gari, wanatumia punda na ng’ombe kuvuta maguta? Barabara za huko ni mbaya na wabunge wa huko ni wale waliopiga makofi wakati wa kupitisha tozo?

Huu umefika wakati wa umma kuipigia kelele serikali kama ilivyo kwa huu mkataba wa DP na kuitaka iwarejeshee wananchi wote zile pesa walizokatwa baada ya tozo hizi kuonekana ni haramu na kufutwa!

Wanasheria, mawakili na wananchi kwa ujumla twendeni mahakamani tukafungue kesi dhidi ya huu wizi! Mahakama iamuru serikali iwarudishie wananchi tozo zao na interest ya asilimia 1000!
 
Kuna aliyetuma hela ikawa kama zamani? Aje atupe ushuhuda

Ni uwongo tozo bado zipo, nimedraw leo!
Naona Nchemba ameondoka na chake wanatuhadaa tu hawa!!
IMG_1473.jpg
 
Wametoa tozo kwenye miamala ya kutuma tuu napo transaction fee inabaki kama mwanzo.. also kwenye withdrawing, hawajatoa tozo hivyo utakatwa withdrawing fee+tozo yenye ongezeko kama kawaida.. so ni sawa na kutoa pesa mfuko wa kishoto na kupeleka kulia afu ukajisifu umesaidia
 
Wametoa tozo kwenye miamala ya kutuma tuu napo transaction fee inabaki kama mwanzo.. also kwenye withdrawing, hawajatoa tozo hivyo utakatwa withdrawing fee+tozo yenye ongezeko kama kawaida.. so ni sawa na kutoa pesa mfuko wa kishoto na kupeleka kulia afu ukajisifu umesaidia
Asee
 
Nilidhani wanajiandaa kwa uchaguzi, sasa wanaondoa yale mambo ambayo yaliwaudhi wananchi, ili 2025 wapite kwa kitonga; Baada ya hapo - mambo yarudi kama kawaida.
 
Back
Top Bottom